Toyota Premio: inafaa kwa Taxi?

Toyota Premio: inafaa kwa Taxi?

Wakuu kama mjuavyo vyuma vimekaza Kiukwel. Nafikiria kujiongeza kwenye biashara ya Taxi je Toyota Premio (pichani) inafaa kwa shughuli tajwa? Ulaji wake wa mafuta, spea n.k. natanguliza shukrani.
1790cc....engine...DBA TR.
**Toyota Premio (si Premier)
hiyo haifai tafuta engine vvti
 
Usiweke tax mzee,iweke uber ina pesa zaidi na ipo kidigitali,utafaidi mwenyewe! Miezi 10 tu tayari umesharudisha hela ya gari ambapo unaweza kununua jingine jipya!! Kama upo nalo nipm nikupe dereva aliesajiliwa uber
Mkuu kwani kuna tofauti gani hapo? kitu ni kilekile tofauti ni namna ya uendeshaji tu, kwa uelewa wangu.
 
Hebu dadavua boss mkuu
1. Tax lazma uende ukasajili na kupaka rangi ule mkanda kutokana na wilaya uliopo,unalipia manispaa na kwenda kupaka rangi veta,while uber hamna kitu kama hicho.
2. Tax lazma ulisajili kama gari la biashara while uber sio lazima.
3. Tax lazima uwe una kijiwe chako specific daily na hapo ni mwendo wa kupiga miayo tu hamna biashara while uber hauna kijiwe specific we popote pale unachill iwe posta,masaki,oysterbay,mikocheni,mbezi beach au msasani.
4. Tax lazma upige debe ndio upate abiria while uber hamna ndio kwanza unachat pm na mrembo wa jf huku unskilizia request za ride.
5. Tax bei ghali na si kila mtu anaweza kuafford while uber kuna cheap ride kuliko hata bodaboda na bajaj.
6. Tax mpaka upate wateja ushapiga miayo sana while huku kwingine ni fasta tu chap ushapata request.
7. Tax risk ya kuibiwa gari au kukabwa na kutupwa mabwepande ni kubwa kwa wote either dereva au abiria while huku kwingine ni risk free totally 100% hata iwe saa nane za usiku uko safe.
8. nimechoka kuandika
 
yote kwa yote kama nilivyosema tufauti ni za kiuendeshaji lakini kwa maana kuu hakuna tofauti.
 
Back
Top Bottom