Voltz nimesikia inasumbua sana alternator. Nilitaka kuchukua nikaogopa hiyo challenge. But still na hitaji. Naomba maelezo zaidiMkuu nakushauri ununue IST achana na ractis kwani vitu vyake vingi vinatumia umeme na vinasumbua hasa kwa mafundi wetu.Kama uko vizuri bora uongeze kidogo ununue toyota voltz
Mkuu hebu funguka hapo kwenye issue za umeme kwa kina zaidi na naomba nipe sifa Toyota voltz in details
local dealers wanacheza na odometer na mara nyingi hununua gari za bei ya chini sana katika minada huku japan , halafu hapa nyumbani huuza kwa bei ghali . so its better ununue gari direct from japan kwanza unasevu pesa kiasi na unapata kitu unachotaka katika ubora uutakao.Mkuu toa maoni yako kuhusu kununulia gari kwenye local dealers hapo bongo?
Mkuu nahitaji hilo gari Ractis wapi tuonane...?Toyota Ractis ni gari zuri tu actually ni jamii moja na akina belta, ist, vitz. Vilevile lina space kubwa ndani na hata dashboard yake imekaa vizuri na ulaji wa mafuta uko vizuri. Hizi gar ni new model ya Funcargo. Yako ya cc 1300 na 1500 na mengi yana injini za VVTI injini ambazo mafundi wengi wa kibongo wanamudu kirahisi kuzitengeneza na vilevile zimeprove kibongobongo kuwa ni nzuri.
Ushauri wangu ni kuwa tafuta ractis yenye kilometer zisizozidi 50,0000 na kama utaagizia toka japan nunua toka makampuni ya autorec, cardeal, na japanesevehicles.com/trust. vilevile sisitiza kampuni za ukaguzi kama JEVIC kuna moja inaitwa East African MotoVehicles .....hii ikatate kabisa isifanye ukaguzi wa gari lako pesa yako watakula na hakuna ukaguzi wowote wa maana watakaoufanya na once gari ukishalipata utashangaa linaanza kukusumbua.
Mi ninalo hilo namba DDE lina km chini ya 50,000 liko vizuri nipm nione offer yako! kama una maswali mengine kulihusu hilo uliza!
Mkuu huwa sishauri sana kununua kwa hawa local dealers hii ni kwa sababu wengi wao ni malaghai kupindukia.Kwa hiyo magari yao mengi si ya kiwango cha juu kiubora ingawa nina rafiki zangu wachache wao huwaelezi kitu kwa hawa local dealers! ni very fortunate naona magari wanayodrive yako poa! kuna mmoja ana Toyota wish na mwingine ana Toyota brevis na wote siyo magari yao ya kwanza kununua bongo! washanunua kadhaa wakayatumia kwa muda mrefu tu! Huyu wa brevis anadai kuna kibabu cha kipemba kinauza magari na ni kiaminifu sana! na anadai huwa analipa kwa installments! na huyu wa wish kuna kampuni inajiita yokohama hapo ndiyo yeye hununua!Mkuu toa maoni yako kuhusu kununulia gari kwenye local dealers hapo bongo?
local dealers wanacheza na odometer na mara nyingi hununua gari za bei ya chini sana katika minada huku japan , halafu hapa nyumbani huuza kwa bei ghali . so its better ununue gari direct from japan kwanza unasevu pesa kiasi na unapata kitu unachotaka katika ubora uutakao.
Mkuu huwa sishauri sana kununua kwa hawa local dealers hii ni kwa sababu wengi wao ni malaghai kupindukia.Kwa hiyo magari yao mengi si ya kiwango cha juu kiubora ingawa nina rafiki zangu wachache wao huwaelezi kitu kwa hawa local dealers! ni very fortunate naona magari wanayodrive yako poa! kuna mmoja ana Toyota wish na mwingine ana Toyota brevis na wote siyo magari yao ya kwanza kununua bongo! washanunua kadhaa wakayatumia kwa muda mrefu tu! Huyu wa brevis anadai kuna kibabu cha kipemba kinauza magari na ni kiaminifu sana! na anadai huwa analipa kwa installments! na huyu wa wish kuna kampuni inajiita yokohama hapo ndiyo yeye hununua!
Ila mimi kwa kweli hawajawahi nishawish kabsaaa!
Ishu ni kwamba gari nyingi za local dealers huwa zimetoka uarabuni! na si japan kama wanavyowadanganya wateja! car dealers wa uarabuni wananunua gari hizo japani zikiwa zimechoka mbaya na nyingine zikiwa zimepata ajali za kufa mtu! hapa ina maana wananunua kwa bei karibu na bure infact wanaisaidia japan kutoa taka kuzipeleka nje ya japan sasa pata picha hapo huwa wananunua japan kwa bei gani! then magari haya yakishafika arabuni wanayafanyia recondition ikiwamo kurudisha mileage nyuma, then baada ya hapo ndiyo sasa zinaletwa kwenye vinchi vyetu then wanawabamiza wateja bei nzuri tu!
Ndiyo maana si ajabu kukuta vigari hivi baada ya muda rangi inafubaaaa hatari! au unakuta mlango/milango ni kama vile inapishana kwa mbaaali wakati wa kuifunga/kufungua! ujue hapo imenyooshwa we mpaka!
So in short buyer beware!!!!!
Mkuu hao siwafahamu. Ila kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo wadau wamekuwa wakichangia hapa jamiiforums mwisho wa siku ukitulia na kuwasoma hao utajua tu kama magumashi au wana vitu vya ukweli!Shukran kwa darasa mkuu
Vipi kuhusu Hawa Japaneseusedcar.com??
Manake SBT nasikia ni wabambikiaji
Excellent explanationsMkuu sasa hapo inategemea wewe mahitaji yako hasa ni nini. Kwa mfano kama una familia inayozidi watu watano wish itakufaa maana nadhani ina seat 7! lakini kumbuka ulaji wake wa mafuta utakuwa uko juu kidogo ya ractis maana cc za ractis ziko chini. Vilevile wish litakufaa kama wewe ni mtu wa kupiga masafa marefu mara kwa kwa mara ila kama ni ni mara chache kwa mwaka ractis itakufaa.
Ila kama uko mji kama Dar na unafanya shughuli zako mahali ambapo kuna vurugu za parking kama mjini katikati/kariakoo then parking kwa gari aina ya wish ni shida kiduuuchu maana wish refu lile!
Ila kama una familia kubwa mi naona bora ununue noah old model ile yenye roho ya paka maana ipo juu kuliko wish ambayo iko chini.
Vilevile unaponunua gari kumbuka sana kutumia oil sahihi na spare parts origino maana hii itasaidia sana kurefusha maisha ya engine ya gari lako.
Nakutakia kila la kheri, upate gari zuri ambalo halitakufanya kufunga ndoa na gereji! maana unaweza pata gari wewe kila mwezi inabidi utenge pesa ya kulikarabati, maana kila likitembea kidogo gari liko gonjwa! utafikiri linaumwa mdudu na linatakiwa litumie dawa za kurefusha maisha!