Toyota Raum zinatumia oxygen sensor?

Hivi mtaalam kazi ya hii oxygen sensor ni nini?? Ina umuhimu gani kwenye Gari?? Ikiharibika au kufa Gari litapata athari zipi?
🤣🤣🤣

Eti mtaalam.

Ili "combustion" itokee humo ndani ya engine, "oxygen" lazima "imixiwe" na mafuta. Kama ulivosoma Form IV "Hydrocarbon, Combustion Reaction".

Sasa hiyo "Oxygen Sensor" inapima/inaangalia kiwango cha oxygen iliyopelekwa kwenye iyo "reaction" na kumuambia "Car computer" kama ipo kiasi kidogo au kingi zaidi ya kinachohitajika.

Inapimaje, kwa kuangalia ule moshi au "byproduct" ya huo mlipuko ndio maana unaona ipo kwenye catalytic converter karibu na exhaust pipe.

Ikiwa inasoma vibaya (ikiharibika) inamaana gari hlitakua na kiwango sahihi cha oxygen na utaona Accerelation imekua poor, "shaking na stalling" pia.

Ila unaweza endesha gari fresh tu bila iyo sensor, sema unaweza jikuta unatumia mafuta mengi zaidi, pia utaua catalytc converter.
 
Gari yangu ni Toyota Raum, ningependa kujua kama zinatumia oxygen sensor, kama ndio zinakuwa sehemu gani?

Be specific Raum model gani?

Oxgen sensor zote zinafungwa linapoanzia Bomba la moshi. Hakuna sehemu nyingine.
 
Hivi mtaalam kazi ya hii oxygen sensor ni nini?? Ina umuhimu gani kwenye Gari?? Ikiharibika au kufa Gari litapata athari zipi?

Oxygen sensor zipo za aina mbili kwenye gari. Kuna upstream na downstream hata ufanyaji wake kazi haufanani.

Upstream inaregulate supply ya mafuta wakati downstream inaangalia ufanyaji kazi wa catalytic converter.
 
Asante sana mkuu
 
Ubarikiwe nimeelimika. Maana Kuna tatizo Hilo nimelipata.
 
Ahsanteni sana kwa coments, pia samahani sana kwa kutuma tatizo bila kusalimia ikiwa ni memba mpya pamoja na kua mfuatiliaji sana wa huu mtandao- tuko pamoja
Msamaha hatujakubali. Tuite Bar tunywe tukikufikiria namna ya kukuwajibisha
 
Wale wezi wa catalytc converter uwa wanaiacha kweli oxygeny sensor mkuu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…