SoC01 Tozo kubwa miamala ya kifedha na makakato ya simu kama kikwazo cha maendeleo ya kidigitali Tanzania

SoC01 Tozo kubwa miamala ya kifedha na makakato ya simu kama kikwazo cha maendeleo ya kidigitali Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Tangu kuanza kwa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia za simu za mkononi huduma hizi zimekuwa maarufu sana na kuchangia kurahisisha maisha ya watu hasa wale wa kipato cha chini tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2008 ambapo M-pesa ilizinduliwa rasmi. kupitia huduma hizi mwananchi anaweza kulipa bili, kutuma fedha, kupokea fedha na kukamilisha miamala yote liyowezeshwa huhuma hiyo. Hata hivyo huduma hizi huenda zikawa chungu kutokana na kupanda maradufu kwa tozo za serikali kwa watumiaji wa huduma hizi. Wakati serikali ikiinadi njia hii kama chanzo kipya cha mapato lakini madhara haya yanaweza kujitokeza,

Mosi, Kuporomoka kwa uchumi wa kidigitali; Kutokana na tozo hizi mpya huduma hizi za kifedha hazitawavutia tena watu wengi kutokana na kuwa na gharama kubwa. Tangu kuanzishwa kwa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi watumiaji wake wamekuwa wakiongezeka kila siku. Katika miaka hii 16 tangu kuanzishwa kwake makampuni na taasisi nyingi za kiserikali zimekuwa zikikusanya malipo kwa njia kwa njia za miamala simu ambapo mtu anaweza kufanya mal ipo akiwa sehemu yeyote na akapata huduma lakini makato haya yanaenda kupunguza ufanisi wa teknolojia hii kwani watumiaji ya wateknolojia hii watapungua.

Pili, Usalama wa fedha utapungua; Kutokana na gharama kubwa niwazi watumiaji wa huduma hizi za kifedha watatumia njia mbadala katika kuweka, kulipa, kusafirisha fedha zao hivyo usalama wa hizo fedha utapungua kuliko wangetumia njia za simu katika kufanya miamala hiyo.

Tatu, Mapato kwa kampuni zinazotegemea njia hizi kukusanya fedha yatapungua; Zipo kampuni mbalimbali zinazotegemea njia za malipo ya kupitia simu katika kuendesha shughuli zake mfano wa makampuni haya ni, makampuni ya michezo ya bahati nasibu, taasisi za kiserikali, maji, na umeme. Ambapo kwa namna yeyote ile watumiaji wake watakwepa kutumia miamala ya simu iliyo rahisi na iliyozoeleka katika kufanya malipo yao na hivyo kusababisha kuchelewa ama kutokuwepo kwa malipo kupitia huduma za kifedha kupitia simu.

Nne, Kupungua ama kufa kabisa kwa teknolojia hii hapa Tanzania. Kufikia leo huduma kama M-mpesa kwa mujibu wa wiki pedia inafanya kazi katika nchi za Kenya, Tanzania, South Arfica, Afghanistani, Lethotho, Drc,Ghana, Mozambique, Egypt, na Ethiopia huku ikijizolea watumiaji lukuki wanaovutiwa na unafuu na urahisi wa huduma hii lakini kutokana na kuanza kuwepo kwa gharama kubwa huenda watumiaji wakatafuta njia mbadala na kusababisha kudhoofu kwa makampuni ya simu ambayo ndio hutoa huduma hizi.

Nini kifanyike? Pamoja na kuwa tozo hizi zinalengo lakuongeza mapato ya nchi, gharama zilizowekwa nikubwa sana na zinaweza kuua mapato mengine hivyo nivyema suala hili likaangaliwa upya ili kufanyika kwake kusiathiri nyanja nyingine kiuchumi.
Pendekezo, Serikali na mamlaka husika zinaweza kupitia jambo hili na kuona ikiwa inafaa kulifanya kuwa hiari kwa watumiaji wasimu ili iwe hivyo au kupunguza gharama ili kuondoa hizi athari.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom