Alisikika Mh. Rais kuwa tozo kwenye miamala ya simu zimeridhiwa na wananchi kwa maslahi yao.
Mapema aliwahi kusikika Dkt. Mwigulu akisema tozo zenyewe ni ndogo tu.
Bila shaka msomi huyu alisahau kuwa chochote cha zaidi kwenye nyingi zilizopo, hakuufanyi mzigo wa tozo zote kwa watu kuwa mwepesi.
View attachment 1889245
Kwamba bado kimeumana. Yuko wapi Mwigulu? Wako wapi wananchi walio zi-ridhia?
Wako wapi Mataga kuonyesha kwa vitendo namna ya kuunga mkono hoja mbili hizi?
Hawa kikundi cha utawala hawasikii maumivu yeyote ya tozo na kodi lukuki kwa watawaliwa bila kujali hali ya kipato. Ndiyo maana watu wote wakawekwa kapu moja bila kujali kipato. Watawala wanaishi "0" grazing kwa kodi za watawaliwa.
Usafiri gari na mafuta ni free, mawasiliano ni free, chakula free, nyumba na malazi free, maji free, umeme free, ulinzi free, wasaidizi nyumbani free, akitaka kwenda nje.ya nchi kwa kikazi au binafsi free nk.
Sasa hawa wabunge, mawaziri, ma RC, ma DC, na genge lote la watawala ukiwaambia tozo zinaua na ni maumivu makubwa hawakuelewi kabisa na wanatuona wachochezi.
Fikiria mtu mnyonge kabisa ana mtoto shule ya kata ila mbali na nyumbani na anakaa hukohuko kwenye bweni lililojengwa kwa nguvu za wananchi. Mzazi anauza kuku 1 tshs. 10,000/= anatuma kwa m pesa kwa mtoto ili apate matumizi. Mzazi anakatwa 750 hivyo zinabaki 9,250/= akituma mtoto anakatwa 1'750/=.
Hivyo muamala wote unakatwa 2,500/= na bakaa ni 7,500/= Kwa hawa wakubwa ni pesa kidogo sana, ila kwa mzazi na mwanafunzi ni balaa kabisa na ni kilio kwa familia yote.
Ongezeko la tozo za miamala kwa lengo la kuongeza makusanyo ya kodi ni jambo halikubaliki kabisa haswa kipindi hiki cha COVID 19 halikubaliki kabisa na ni kuua kabisa uchumi wa mwananchi mnyonge. Ila kwa vile watawala wameamua kutukomoa! No way out. But God is with us.