BrainyChuo
Member
- Sep 20, 2013
- 5
- 0
Wigo Wa Kodi Uongezwe Kuelekea Wapi?
Kwa miaka mingi tumekua tukiilalamikia serikali iongeze wigo wa kodi na isiangalie vyanzo vile vile vilivyo zoeleka kama vinywaji baridi, pombe, sigara na mafuta ya petroli. Kwa bahati sasa hivi vitu vile vilivyozoeleka vingi havijaguswa na vingine vimeingia kasoro kama mafuta ya petroli yaani havigusiki hivyo ni ngumu kuongeza kodi upande huo.
Ukiangalia kodi zilizotajwa hapo juu utagundua kwamba kodi nyingi zimelenga makundi machache sana ya wanaopaswa kulipa kodi yaani wanywaji, wavuta sigara, watumia bidhaa za mafuta ya petroli.
Mbali na maeneo hayo, makundi mengine yaliyokuwa yanaangaliwa sana ni waajiriwa na wafanyabiashara. Hivyo malalamiko mengi ya kuongeza wigo yametoka kwa makundi hayo yanayolipa kodi pamoja na wachumi na wanasiasa.
Kwa upande wa wananchi ambao hawapo kwenye makundi yale yanayolipa kodi walikua wanapenda sana kodi iongezwe na sheria ziwe kali zaidi kwa wale wanaopaswa kulipa kodi. Wale wanaolipa kodi mara nyingi malalamiko yao yalikua yanaonekana hayana msingi wowote mbele ya makundi yale yasiolipa kodi.
Ila cha kujiuliza ni kwamba, kama maeneo yale yaliyozoeleka hayajaguswa, huku maisha yamepanda, bajeti ya serikali imepanda, maana yake serikali itakua na upungufu kwenye makusanyo yake hivyo ni lazima iangalie vyanzo vingine vya kodi au kwa maneno mengine waongeze wigo wa kodi.
Serikali imeona iongeze wigo wa kodi kwa kuweka tozo kwenye miala ya simu na bank. Inavyoonekana pamoja na sababu nyingine tozo zilizoongezwa ni rahisi kukusanya na pia inamgusa kila mwananchi awe waziri, mwanasiasa, mkulima, mfanyakazi ama mfanyabiashara. Yaani inawagusa hata wale ambao walikua hawaguswi na kodi yeyote kwenye hii nchi.
Yaani tozo inamgusa kila mtu na pia ni rahisi sana kukusanya.
Kisa cha kuandika haya yote ili yawe msingi wa ushauri wangu kwa wananchi wenzangu, wanasiasa na wataalamu tunao lalamika, mbali na kulalamika tuweze kuishauri serikali ikotoa tozo iongeze wigo wa kodi kuelekea wapi yaani kwenye maeneo gani? Kwa kuwa serikali piga ua inahitaji pesa.
Ushauri Mzuri Kutoka Kwa Wadau
Baadhi ya maoni ya wadau ambayo ni ni ya msingi serikali iyafanyie kazi ni yafuatavyo
- Serikali ibane matumizi, pamoja na kuacha ununuzi na matumizi ya magari ya kifahari
- Ikusanye mapato vizuri na kuziba mianya ya upotevu wa mapato kwenye vyanzo vya sasa kama vile bandari.
- Iimarishe mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali ili isisumbue walipa kodi
- Kuangalia sheria za kodi ambazo hazitekelezeki, maana huko nyuma tumekua na tabia tukishindwa kukusanya kodi kwa kutumia sheria iliyopo tunaongeza sheria nyingine matokeo yake tumekua na kodi nyingi sana kwenye chanzo kimoja - mfano kwenye utalii na mafuta kuna utitili wa kodi.
Wanaotuongoza ni binadamu kama sisi, wanapokea ushauri hivyo malalamiko peke yake hayawasaidii. Sasa basi, kwa upange wako kama unaona tozo zifutwe ungependa serikali iongeze wigo kodi kuelekea wapi? au kwenye maeneo gani?