Tozo ya majengo inayolipwa kupitia Luku inakatwa kila mwezi au kila ukinunua umeme?

5418 3826 368

Nimelipa Tsh 4,000/= muda huu halafu nimepata umeme wa Tsh 1,000/=.
Maana yake Tsh 3,000/= haipo
Mwezi uliopita nilikatwa Tsh 2,000/=, sasa naomba unifafanulie lipi ni kosa langu

TANESCO njoo uone maajabu yenu huku maana ninyi mwa kufanya maajabu dunia inawatambua
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu!

Kama ambavyo Serikali ilivyotangaza kuwa kodi ya majengo italipwa kupitia manunuzi ya umeme hivyo basi zoezi lilianza Mwezi wa nane 2021 ambapo wateja walikatwa makato ya mwezi wa Saba (Tsh 1000) na wa nane ( Tsh 1000) jumla Tsh 2000 kwa miezi miwili.

Kwa wateja ambao hawajakatwa kodi husika Mwezi wa Saba na wa Nane watapaswa kulipia kiasi cha Tsh 3000 ili kulipia kodi ya majengo ya mwezi wa Saba, Nane na Tisa 2021.

Wateja ambao hawajakatwa miezi hiyo wanashauriwa kununua umeme wa zaidi ya shilingi 3000 ili waweze kupata token

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

Makao Makuu
 
Tanesco wameshafanya maajabu yao kama kawaida yao,
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Tozo juu ya tozo katikati ya janga la Corona kwa hakika ni Tanzania tu.

Sawa na wasimamishe uchumi wao kwanza.
Umesema jambo la maana sana, nchi nyingi zimejaribu kupunguza makali ya maisha kwa wananchi kwa kugawa chakula na pesa kwa wananchi wao. Je Tozo hazikuweza kusubiri hili janga la korona lithibitiwe.
 
Kwahiyo mnakata mwanzo wa mwezi! Nikinunua tar.25 mnakata na nikinunua tena tar.3 mnakata!
 
Ndio ni kila mwezi
Maana inatakiwa iwe jumla 12,000 kwa mwaka hivyo ni buku buku kila mwezi hadi mwaka kuisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…