Tozo za miamala zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025. Uzalendo zaidi unahitajika

Tozo za miamala zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025. Uzalendo zaidi unahitajika

Sisi tunaokaa vijijini ndio tunaelewa maana ya Zahati ya kijiji, Shule ya kijiji au kata, Sisi ndio tunajua adha ya maisha,

Mnaopinga ni nyie mnaoishi mjini na ndio maana mnamiliki hata simu,

Njooni mtuhoji hukuvijiji nasisi,

Sisi tunataka shule, zahati na barabara mengine ya tozo tutavumilia
Kwa hiyo tuporwe kila kitu hata kula tushindwe tupate utapiamlo na vidonda vya tumbo...kesho na kesho kutwa nani atalipa hiyo kodi ya kuwajengea hizo Zahanati wakati Walipaji watakuwa hawana tena uwezo wa kutengeneza kipato?.

Hoja hapa ni kumkamua Ng'ombe huku naye anakula.

Kumwambia Ng'ombe sasa ale Mlo mmoja tu eti familia inataka kuboresha maisha ni kauli ya Mfugaji punguani.
 
4448E036-6CE0-40BE-9EC0-F73801ADA3C3.jpeg
9FE9B6C4-E6EB-4143-9361-C690EEE8D902.jpeg
 
HIZI HAPA FAIDA ZA TOZO MPYA KWA WATOTO WA MASIKINI WA NCHI

Tupige moyo konde, najua pesa hakuna,najua mzunguko wa pesa hakuna ila tuwaache wenye pesa wasaidie Taifa lao kwa faida ya watoto wetu kesho.

Tuache harakati kwenye maendeleo ya watu, hayupo Mjomba wala shangazi wakutujengea barabara, shule,Zahanati,Hospitali kwaajili yetu na kwaajili ya watoto wetu na watoto wao ila ni sisi wenyewe.

[Hebu angalia faida za tozo kwenye sekta mbili tu za Afya na Elimu]

1. UJENZI WA VYUMBA 10,000 VYA MADARASA

Tunaweza kujenga shule 2,000 za O'level au shule 2,500 za A'level au Shule 1,428 za kidato cha ( I-VI) au Shule 1,250 za Msingi hii ni sawa na katika kila kata 2 itajengwa shule mpya 1 kwenye kata zote 3,956 au nisawa nakusema katika kila jimbo la uchaguzi kwenye majimbo yote 264 zitajengwa shule mpya 8 za Mama Samia likiwemo Jimbo la kaka yangu, "Thadei Ole Mushi " Nakwarejea tu,Tanzania tuna shule 5,330 tu za sekondari,Shule mpya nikaribu nusu ya shule zote za sekondari zilizowahi kujengwa tangu Uhuru,

Nakama tozo hii itaenda mpaka 2025 Mama Samia atajenga shule mpya zinazofikia 10,000 hii ni sawa na kusema karibu kila kijiji kitakuwa na shule mpya ama ya sekondari ama ya msingi kupitia tozo za e-money.

2. UJENZI WA ZAHANATI MPYA 900

Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano alijenga Zahanati 1,198.Leo Mama Samia kwa kutumia Tozo ya Uzalendo atajenga Zahanati mpya 900 kwa mwaka 1 wa fedha|FY 2021/22.Hii ni sawa na Zahanati mpya 4,500 kwa miaka 5 yaani kila Jimbo zitajengwa Zahati mpya 4 katika kila mwaka wa fedha ni sawa na Zahanati 20 kwa miaka 5 ya kwanza ya Mhe Samia Suluhu na hii ni kwamajimbo yote 264,Kwa lugha rahisi ifikapo 2025 kila kata itakuwa na Zahanati Mpya 2 za Mama Samia,

3. UJENZI WA VITUO 114 VYA AFYA

Hyt Rais Magufuli kwa miaka 5 alikarabati na kujenga jumla ya vituo vya afya 487,Leo Mhe Rais Samia Suluhu kwa kutumia Tozo ya e-money atajenga vituo vipya 114 kwa mwaka 1 sawa na vituo 570 kwa miaka 5 ya awamu ya kwanza,Kwa lugha rahisi mwaka 2025 kila Wilaya itakuwa na Vituo vipya 4 vya afya vya Mama Samia vitakavyohudumia watoto wa masikini

Itaendelea, kazi iendelee...

C&P
Source?
 
Haya mahesabu yangefanywa kwenye ile gharama ya lile sanamu..
 
Hayo ni mawazo yako au ya mama samia au serikali yetu kwa ujumla?
 
Kama MO, BAKRESA na GSM watalalamika namimi nitalalamika ila nashanga mtu anakatwa 4,200 analialia hajua hawa matajiri kwa siku wanakatwa mamilioni na hawana kelele, Masikini hana jema.

Shida sio makato shida Magufuli alitupiga kiuchimi balaaaaa, elfu 4,200 inaumaa
Mpaka anakatwa mamilion nikwamba nayeye kaingiza mabilioni huo ndo utaratibu.
 
Tatizo la Uhuru ni nini?

Wao wameandika alichosema waziri,
Uhuruuuu...!!! Baada ya heading hii, Samia Suluhu Hasani akija na MABADIRIKO, NAO WATABADILI HEADING... mama kasikia kilio, ni msikivu, TOZO ilikuwa haramu...!!
Tatizo la Uhuru ni nini?

Wao wameandika alichosema Waziri Ummy,

.
 
Katika watu ambao ni wapuuzi basi ni Hawa viongozi wa sasa, yaani badala ya kutoka kuwaeleza watu tozo hizo zimewekwa kwa ajili gani na zitafanya nini yamekaa kimya yanawaacha machadema yanatamba.

Wanao umia kwenye kukosa hizo huduma ni hao hao wanaojiita maskini ndio watoto wao wamerundikana kwenye madarasa,ndio hawana bima na wanazalia chini kwenye hospital chache zilizopo,hawana maji na mbaya zaidi barabara za uhakika hakuna.

Hao ndio Mtaka aliwaambia watoto wao wanatembea km 50 zaidi kwa wiki ila hawataki kuumia sasa ngoja waendelee kusugua zaidi tuone kama wakibaki na hivyo vihela watatoka kwenye umaskini.

Unawasikiliza wapuuzi wa CDM hawajawahi Jenga shule hata moja ya mfano kusaidia jamii wanaishi kwa ruzuku za serikali na misaada ya wazungu,wewe unaehaso eti unacheza ngoma yao?
Hivi wewe uko nchi gani? Maana kama ni tanzania lazima uone kuwa maumivu na malalamiko hayatoki chadema yanatoka kwa wananchi ambao ndio hao wanaitwa wanyonge. Usijitie upofu na ushabiki tozo sio rafiki full stop.
 
Sisi tunaokaa vijijini ndio tunaelewa maana ya Zahati ya kijiji, Shule ya kijiji au kata, Sisi ndio tunajua adha ya maisha,

Mnaopinga ni nyie mnaoishi mjini na ndio maana mnamiliki hata simu,

Njooni mtuhoji hukuvijiji nasisi,

Sisi tunataka shule, zahati na barabara mengine ya tozo tutavumilia
Kwa hiyo hamkujengewa hivo vitu kabla kwa kuwa hakukuwa na tozo? Kwa hio bila tozo hizi haiwezekani kujengewa?. Ewe mtu wa kijijini unaemiliki simu?.
 
Hivi wewe uko nchi gani? Maana kama ni tanzania lazima uone kuwa maumivu na malalamiko hayatoki chadema yanatoka kwa wananchi ambao ndio hao wanaitwa wanyonge. Usijitie upofu na ushabiki tozo sio rafiki full stop.
Kuna kodi isiyouma?
 
Tulipe kodi, mbona sio hela nyingi, tena ukilinganisha na nchi za wenzetu, kodi yetu ya miamala iko chini nitaweka data hapa, watanzania hawana utamaduni wa kutaka kulipa kodi, watumishi wa umma na sector binafsi ndio walipaji wakubwa wa kodi.

Ila wafanya biashara huwa hawataki hata kusikia 1% ya kodi imeongezeka. Watumishi wa umma hulipa hadi 30% ya makato yote ya mshahara. Ila mfanyabiashara akisikia hata 3% ya kodi imeongezeka, ni kelele na hawataki kusikia. Tulipe kodi plz
Hizi tozo sio kodi ni Wizi..
 
Kodi zilizokuwa zinakusanywa hapo awali zilikuwa zinafanyia nini?
Elewa maana ya Bajeti ya nyongeza,

Hii basket fund niekwaajili yaemaendeleo vijijini tu,

Budget zingine zitaendelea kama kawaida
 
Mkuu hayo mazahanati na vituo vya afya havisaidii kitu, wangesema hospital zote za mikoa au wilaya zitakuwa na madktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ikiwemo na vifaa tiba kama CT scan, MRI nk hapo ingekuwa sawa, kwenye vituo vya afya na zahanati waganga wanatibu kwa kutabiri tu matokeo yake vifo visivyo vya lazima vinakuwa vingi.Hivi CT scan ni sh ? kwann haipo kila mkoa? mgonjwa ulazimika kwenda km 300 kupata huduma hiyo hamuoni kama ni umbali mlefu sana? nako akienda hiyo gharama sasa!!!! kama sio mtumishi wa huma mwenye bima ya afya anakufa wanamwangalia tu. Hizo tozo zingelenga hapo, vituo vya afya wananchi wanaweza kujenga wenyewe kwa nguvu zao na serikali ikachangia kidogo.
 
Back
Top Bottom