HIZI HAPA FAIDA ZA TOZO MPYA KWA WATOTO WA MASIKINI WA NCHI
Tupige moyo konde, najua pesa hakuna,najua mzunguko wa pesa hakuna ila tuwaache wenye pesa wasaidie Taifa lao kwa faida ya watoto wetu kesho.
Tuache harakati kwenye maendeleo ya watu, hayupo Mjomba wala shangazi wakutujengea barabara, shule,Zahanati,Hospitali kwaajili yetu na kwaajili ya watoto wetu na watoto wao ila ni sisi wenyewe.
[Hebu angalia faida za tozo kwenye sekta mbili tu za Afya na Elimu]
1. UJENZI WA VYUMBA 10,000 VYA MADARASA
Tunaweza kujenga shule 2,000 za O'level au shule 2,500 za A'level au Shule 1,428 za kidato cha ( I-VI) au Shule 1,250 za Msingi hii ni sawa na katika kila kata 2 itajengwa shule mpya 1 kwenye kata zote 3,956 au nisawa nakusema katika kila jimbo la uchaguzi kwenye majimbo yote 264 zitajengwa shule mpya 8 za Mama Samia likiwemo Jimbo la kaka yangu, "Thadei Ole Mushi " Nakwarejea tu,Tanzania tuna shule 5,330 tu za sekondari,Shule mpya nikaribu nusu ya shule zote za sekondari zilizowahi kujengwa tangu Uhuru,
Nakama tozo hii itaenda mpaka 2025 Mama Samia atajenga shule mpya zinazofikia 10,000 hii ni sawa na kusema karibu kila kijiji kitakuwa na shule mpya ama ya sekondari ama ya msingi kupitia tozo za e-money.
2. UJENZI WA ZAHANATI MPYA 900
Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano alijenga Zahanati 1,198.Leo Mama Samia kwa kutumia Tozo ya Uzalendo atajenga Zahanati mpya 900 kwa mwaka 1 wa fedha|FY 2021/22.Hii ni sawa na Zahanati mpya 4,500 kwa miaka 5 yaani kila Jimbo zitajengwa Zahati mpya 4 katika kila mwaka wa fedha ni sawa na Zahanati 20 kwa miaka 5 ya kwanza ya Mhe Samia Suluhu na hii ni kwamajimbo yote 264,Kwa lugha rahisi ifikapo 2025 kila kata itakuwa na Zahanati Mpya 2 za Mama Samia,
3. UJENZI WA VITUO 114 VYA AFYA
Hyt Rais Magufuli kwa miaka 5 alikarabati na kujenga jumla ya vituo vya afya 487,Leo Mhe Rais Samia Suluhu kwa kutumia Tozo ya e-money atajenga vituo vipya 114 kwa mwaka 1 sawa na vituo 570 kwa miaka 5 ya awamu ya kwanza,Kwa lugha rahisi mwaka 2025 kila Wilaya itakuwa na Vituo vipya 4 vya afya vya Mama Samia vitakavyohudumia watoto wa masikini
Itaendelea, kazi iendelee...
C&P