tozo za simu, Ikulu yafunguka

Sijui na mie sijawaelewa?! Kwa hayo makampuni ya simu kukutana, ina maana warekebishe humo humo kwenye sekta ya mawasiliano (ambayo haitakuwa tofauti na tozo la sim card), au wawatafutie chanzo kipya?! Aiseee......choka kabisa.

Kama hawazitegemei kampuni za simu kujua sehemu nyengine mbadala wa serikali kupata mapato yake, ina maana wanataka hiyo kodi ibadilishiwe sehemu iingizwe huko huko kwenye kampuni za mawasiliano

Sasa umesikia wapi kampuni ikasema tutozeni sisi extra kodi ili wateja wasipate udhia?

Maana yake ni kwamba kodi hiyo tutailipa sisi wananchi kupitia mawasiliano kwa njia moja ama nyengine
 

Exactly.....kwa hiyo sioni tofauti kwa sababu kama inatolewa kwenye simcard, basi labda tutakutana nayo kwenye airtime! Tofauti iko wapi?
 
Kazi kubwa, ngoja tungoje itakuwaje. Na sisi wamiliki wa magari itabidi tukamuone ilia aangalie jinsi ya kupunguza insurance na road licence maana itatuua.
 
mie sion sababu ya wananchi kuto kulipa kodi nchi zote ambazo zinaitaji kuendelea ni lazima wananchi walipe kodi isipokuwa kodi hiyo buku kwa kila mwannchi ni kubwa sana kwa mtu wa kipacho cha chini ili nchi iendelea wanapaswa kulipa ksema wannchi wanaona pesa zao zinazolipwa kodi zinaenda kufichwa uswiz wakati watu njaa hadi mfukoni
 
binafsi kinachonisismua ni namna serikali moja inavyokuwa na na mbinu hafifu za kukabiliana na changamoto hafifu kama hii !
kila mtu serikalini anasema lake, hatuelewi hata nani wakumuamini !
 
Mwezi huu mwanzoni gharama za mawasiliano ziliongezwa kinyemela! Kwa mfano nilikua nikinunua kifurushi cha maongezi cha wiki moja kwa shilingi 4999/- na kupata dakika 210,lakini siku hizi kwa fedha hiyo hiyo napata dakika 150 tu!

Kwa mawazo yangu nlijua wameanza tozo tayari maana tuliahidiwa punguzo katika mawasiliano, wakapunguza kisha wakaongeza!

Je watakapofuta hii kodi kisanii kwa jina kisha kubakiza makato katika simu zetu kama kawaida itakuje?
 
wazimu mtupu, kampuni za simu ndiyo moja ya zisizolipa kodi ipasavyo,ninauhakika serekali wakiacha rushwa rushwa zao na wakakusanya kodi ipasavyo kwenye hizo hizo kampuni za simu tu watapata pesa zaidi ya hiyo 178 billion.

Una uhakika?? Home
 

wazo lako ni zuri sana. Swali ni je, matumizi ya serikali kutoka hata hayo mapato kiduchu yanazingatia mahitaji halisi ya wananchi? Hakuna asiyepennda kulipa kodi, lakini je matumizi ya kodi hiyo yanawekwa wazi na mwananchi anaimani kuwa kodi yake inatumika vizuri? Napendekeza wanaharakati watafute namna ya kupata fedha halafu waendeshe utafiti kwa kuuliza wananchi kama wanaridhika na mapato na matumizi ya serikali yao sikivu. Waweke na mapendekezo.
 

Ndiyo maana mimi nashangaa tunavalia njuga swala la 1000 (SIM CARD). Kelele hizi zipigwe kwenye kodi zote zilizowekwa kwenye matumizi ya simu za mkononi, mafano kutuma na kupokea fedha, muda wa maongezi, internet etc.
 
True mimi nadhani tuongeze bidii katika kukusanya mapato na kuzisimamia vizuri sheria na sera za matumizi ya kodi za sisi wananchi
 
Saa hizi serikali imejifunza...wabongo wamekua wajuaji sana.sasa kodi zitakatwa kimyakimya.
Wao wangekua na uhakika pesa itakayopatikana itafanya kitu cha kuonekana wangekazia hapohapo,lakini wakiachia ndo kila kodi itakayowekwa kwa raia,wataikataa.
 
Hii habari inanikumbusha enzi za darasa la tatu la miaka hivyo na vitendawili...

Hapa huwezi kukwepa kuona kuwa ndani ya hii serikali ni mwendo wa "wafu wanakokotana....."!
 

Nimesikitika sana, eti Rais anaomba makampuni ya simu nayo yashiriki kutafuta vyanzo mbadala vya kuziba pengo hilo??

Hii ni level ya juu sana ya kutokuwajibika...
 
Kwa kwa uzembe wa mamlaka zetu, yaani hizi hela zitawanufaisha sana makampuni ya simu!!!!! Yaani wanaomba Mungu isipingwe maana fasta watagawana na serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Katika hicho kikao mbona sijasikia na wawakilishi wa wananchi kupitia vyama vya walaji wako? Yaani Consumer Consultative Council? Yaani kweli unaita one part unategemea majibu yaweje? The meeting was not representative at all. Ni mabavu na udikteta as usual tu naona hapa.
 
Nimesikitika sana, eti Rais anaomba makampuni ya simu nayo yashiriki kutafuta vyanzo mbadala vya kuziba pengo hilo??

Hii ni level ya juu sana ya kutokuwajibika...

Hiyo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nayo ovyo habisa

Hawana hata akili ya kuchagua cha kukisema

Maana hii ni fedheha kwa serikali nzima
 
Sasa wanategemea kampuni za simu ziiambie serikali mahali pengine pakupata mapato yake?
Yaani wanampa fisi ulinzi wa bucha ya nyama.

Hapa ndipo namshangaa sana rais wetu, yeye hajawa sehemu ya suluhu hata siku moja. Anachopenda ni kukaa katikati ili aonekane mzuri. Bajeti imeandaliwa na serikali yake halafu makampuni ya simu eti ndiyo yachukue dhamana ya kutafuta vyanzo vya mapato.

Jamani hii miaka 3 itaisha lini? Ukisikia kiongozi asiye na vision au mission na kiongozi dhaifu sana basi JK ni mfano mzuri.

Yaani aibu tupu, tena barua ipo katika nembo ya taifa. Shame on you Mr President, this is too low and disgusting.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…