Hiyo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nayo ovyo habisa
Hawana hata akili ya kuchagua cha kukisema
Maana hii ni fedheha kwa serikali nzima
Wenyewe wanajua kuwa mzee anapata sifa kwa kusikiliza manun'guniko bila kujua wanamwanika.
Rais wa nchi unapata tatizo kama hili unapoita viongozi unakuwa na maagizo, majibu, maelekezo na amri.
Huwezi kwenda kuwaomba Vodacom na Tigo waisadie serikali yako kutafuta vyanzo vya mapato!
Ni aibu kubwa sana kwa taifa.
Wala hakukuwa na sababu ya rais kuwaita kwasababu hakuwa na suluhu, si afadhali angemtumia katibu mkuu kwasababu barua hiyo kila mtu anajua inatoka Ikulu, maudhui na tija yake havifanani kabisa na Ikulu. Ni aibu sana!
Mwasiliano Ikulu hii ni aibu, aibu kwa taifa. Tena afadhali ni ya kiswahili maana ingekuwa kiingereza wanachoelewa wenzetu wa nje wangeendelea kutucheka na kutuona mbuzi tu.
Aibu sana
Wale vinara waliomwandikia barua Obama akina January sasa hivi wamejificha. Wanasubiri baada ya muda waje na unafiki wa maendeleo na miradi. Wabunge wa CCM waliopitisha huu uzembe wamejificha, hakuna anayesimama na kutoa msimamo.
Aibu sana taifa, na aibu hii inatoka kwa wabunge wa CCM, Mwenyekiti na serikali ya CCM. Ni aibu, someni barua hiyo mujiridhishe kama ni kitu cha kuweka hadharani.
Barua imemdhalilisha sana rais wa JMT, huwezi kuwa na uongozi kwa mfumo wa Private public partnership (PPP)
Uongozi wa nchi siyo enterprise ambayo entrepreneur wanashiriki kama alivyofanya rais wa JMT.
Huwezi ku commission shughuli za taifa kama mawasiliano kwa Vodacom na Airtel au Tigo! Who are they!
Hawa ni sehemu gani ya utawala wa nchi Mr president.
Ikulu mawasiliano tokeni muombe radhi maana kitendo mlichokifanya ni kumwacha mzee dah...
Aibu kubwa sana
Rais wa Tanzania aomba ubia wa kuongoza taifa na mameneja wa makampuni ya simu! Mungu tusaidie, mungu tuangalie!