tozo za simu, Ikulu yafunguka

Hiyo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nayo ovyo habisa

Hawana hata akili ya kuchagua cha kukisema

Maana hii ni fedheha kwa serikali nzima

Bahati nzuri hatuna culture ya kuwafuta watu kazi.....

Ila hapa mtu akiamua kufanya kweli, where will the buck stop?

Kinachoendelea ni sawa na kumkabidhi mgoni wako akutunzie famili....
 

Kweli mkuu....

Viongozi wetu wa siku hizi hawana maono kabisa....ndiyo maana ni wachache sana ambao wanaweza kuandika hata article ya kurasa 2 kwenye gazeti.....hapo hujaongelea vitabu kama vya akina Nyerere!

Hawana political philosophy hata chembe...
 
Bahati nzuri hatuna culture ya kuwafuta watu kazi.....

Ila hapa mtu akiamua kufanya kweli, where will the buck stop?

Kinachoendelea ni sawa na kumkabidhi mgoni wako akutunzie famili....

Serikali ibane matumizi yake kwa kutimulia mbali watu kama hawa wa kurugenzi ya mawasiliano

Matumizi ya serikali ni makubwa na matokeo yake ni utumbo mtupu

Wabane matumizi tu, makampuni ya simu haijawahusu hata kidogo pa kuzitolea fedha za bajeti
 
Hiyo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nayo ovyo habisa

Hawana hata akili ya kuchagua cha kukisema

Maana hii ni fedheha kwa serikali nzima
Wenyewe wanajua kuwa mzee anapata sifa kwa kusikiliza manun'guniko bila kujua wanamwanika.

Rais wa nchi unapata tatizo kama hili unapoita viongozi unakuwa na maagizo, majibu, maelekezo na amri.
Huwezi kwenda kuwaomba Vodacom na Tigo waisadie serikali yako kutafuta vyanzo vya mapato!
Ni aibu kubwa sana kwa taifa.

Wala hakukuwa na sababu ya rais kuwaita kwasababu hakuwa na suluhu, si afadhali angemtumia katibu mkuu kwasababu barua hiyo kila mtu anajua inatoka Ikulu, maudhui na tija yake havifanani kabisa na Ikulu. Ni aibu sana!

Mwasiliano Ikulu hii ni aibu, aibu kwa taifa. Tena afadhali ni ya kiswahili maana ingekuwa kiingereza wanachoelewa wenzetu wa nje wangeendelea kutucheka na kutuona mbuzi tu.
Aibu sana

Wale vinara waliomwandikia barua Obama akina January sasa hivi wamejificha. Wanasubiri baada ya muda waje na unafiki wa maendeleo na miradi. Wabunge wa CCM waliopitisha huu uzembe wamejificha, hakuna anayesimama na kutoa msimamo.

Aibu sana taifa, na aibu hii inatoka kwa wabunge wa CCM, Mwenyekiti na serikali ya CCM. Ni aibu, someni barua hiyo mujiridhishe kama ni kitu cha kuweka hadharani.

Barua imemdhalilisha sana rais wa JMT, huwezi kuwa na uongozi kwa mfumo wa Private public partnership (PPP)
Uongozi wa nchi siyo enterprise ambayo entrepreneur wanashiriki kama alivyofanya rais wa JMT.

Huwezi ku commission shughuli za taifa kama mawasiliano kwa Vodacom na Airtel au Tigo! Who are they!
Hawa ni sehemu gani ya utawala wa nchi Mr president.

Ikulu mawasiliano tokeni muombe radhi maana kitendo mlichokifanya ni kumwacha mzee dah...
Aibu kubwa sana

Rais wa Tanzania aomba ubia wa kuongoza taifa na mameneja wa makampuni ya simu! Mungu tusaidie, mungu tuangalie!
 
Kiini macho hicho. We hushangai wadau wa makampuni ya simu nao wameshirikishwa kwenye hyo team

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Akili ndogo inaongoza akili kubwa... Msigwa
 
Nimevutiwa na hii kitu

Nahisi kila kitu kwenye hiyo barua ni usanii mtupu. Angalia heading na underline yake...usanii mtupu. Aliye andika hiyo barua sidhani kama anajua kazi yake au la hafanyi kazi huko ikulu...
 

...point nzuri sana...Consumer Consultative Council haijawahi sikika katika chochote, sishangai hata katika ukandamizaji wa kiasi hiki hawajasikika...
...vikao visivyo na dira haviwezi kuleta maamuzi yenye mantiki. Hii ni 'funika kombe mwanaharam apite'...Kwa namna hii nakosa maana halisi ya 'serikali' hapa naona kikundi cha walaji kinatafuta namna ya kukaa madarakani...(stupid)
 
Pandisheni kiwango cha gawio kutoka migodi ya dhahavu kwa asilimia 0.1 na hili tatizo litamalizwa. mwekezaji wa migodi ya dhahabu ambaye ahatake aondoke. hakuna tatizo kabisa hapo na wala hiyo tarakimu mya 178 billion isiwe kutishia watu nayo.


Ikulu ya Kikwete, Waziri mkuu, Waziri wa Fedha ni mkinzano mtu

 
Email ya Ikulu, I mean Ikulu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni ikulumawasiliano@yahoo.com. Haiinii akilini! Hii inaweza kuingia kwenye maajabu kumi mapya ya mwaka huu. Ikulu ya nchi inatumia domain ya yahoo kwa mawasiliano? Kuna vi- NGO vidogovidogo tu humo mitaani vina domain zake binafsi, halafu Ikulu ya nchi inatumia yahoo?

Lakini nikigeukia hoja ya msingi, hivi Kikwete anataka kumhadaa nani? Au anataka kutuaminisha kwamba hiyo bajeti ya nchi aliliandaa Mgimwa peke yake? Aache kutuchezea akili huyu Kikwete. Ni nini asichokijua hadi aje ajifanye eti kuhamasisha watu fulani kutufuta suluhu? Wakati inpendekezwa hiyo kodi yeye alikuwa wapi, ilihali ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri?
 
Nahisi kila kitu kwenye hiyo barua ni usanii mtupu. Angalia heading na underline yake...usanii mtupu. Aliye andika hiyo barua sidhani kama anajua kazi yake au la hafanyi kazi huko ikulu...
Iko kama press release inapoanza,
afu ghafla inabadilika kuwa kama ripoti tu ya mwandishi fulani akiripoti tukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…