Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Meanwhile in Rwanda.
Screenshot_20210823-085812_Twitter.jpg
 
Jana asubuhi namtumia pesa mdau kijijini akiwa na line ya voda mi nikiwa na tigopesa niliona hii issue ni sio,ni WIZI kama wizi mwingine ambapo Serikali ikishirikiana na sekta binafsi(Banks na Makampuni ya simu) Kuwaibia wanyonge.Nilikuwa nimtumie mdau kama laki 1 (100,000 tsh) . Mi asubuhi kucheck sina pesa kwenye tigopesa hivyo ikabidi nihamishe 110,000 toka CRDB kwenda tigopesa.

Kucheck gharama ya muamala huo kwa benk ni tsh 6500 hv. Yaani 5400 na VAT 940. Sasa ikafika hatua ya kutuma tigo pesa kwenda mpesa ikanicost tena tsh 4500. Hapo jumla sh 11,000. Kama gharama ya kuhamisha benk CRDB to tigopesa na tigopesa kwenda Mpesa. Ilibidi nitume 106,000 ili naye aweze kutoa hiyo 100,000.

So jumla ya kuhakikisha mdau anapata 100,000 nilitumia 11,000 ya awali na 6000 jumla 17,000. Hii ni zaidi ya riba ya kukopeshana kwenye mabenki kwa mwaka mzima. Gharama nilioingia ni 17% ya laki 1 ndani ya dk 2 tu za kufanya muamala huo. Wakati mtu angekopa laki 1 angelipa laki 1 na riba elfu 15 ndani ya mwaka mzima.

Kwa hili hatari iliyopo ni kwamba watakaothirika ni ndugu zetu ambao wanatutegemea kwa namna moja au nyingine. Mfano ikiwa Huna pesa kabisa ingebidi ubalance hiyo laki itoshe kila kitu. So huenda yule mdau angepokea 83,000 na kushindwa kutimiza lengo na kama lengo ni matibabu, ada ya shule n.k hapo inakuwa hatari zaidi.

Hatari nyingine ni kwamba tunarudi nyuma miaka 20 hivi. Maana itabidi watu waingie ndani benki kutoa akaunti moja na kuingiza akaunti nyingine na hivyo hatari ni kuwa lengo la kujenga zahanati, madarasa halitatimia kwa kuwa miamala hiyo haina tozo na mwakani itabidi turudi kufuta hili.

Najua kukosea huwa kupo kwa kilabinadamu Including serikali. Wangesawazisha hili mapema kwa kukusanya kidogo mfano 1000 au 500 kwa transactions na namba ya miamala ingekuwa mingi miamala ambayo inafanyika na lengo lingetimia bila kumuumiza mtu wa chini. Hili hawajachelewa ila wakiendelea hivi watapoteza vyote ikiwemo trust kwa wananchi na pesa wanaotegemea kukusanya.
 
Habari wakuu,
Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema...
Hii ni Tozonia au Tanzania ??!!
 
Hii Nchi imeshakua tayari ya moto! Ingawa kwa sisi watumishi wa umma, kitambo haya maumivu tulishayazoea.
Bado mna maumivu? Nilisikia shangwe za umma, wake kwa waume, walio ajirani na kutoka kwa wenye wenza ajirani, wakisifu na kushangweka kuwa baada ya miaka 5 migumu, hatimaye madaraja yamepanda, wamelipwa malimbikizo, paye imepunguzwa n.k

Imekuaje tena hii kauli ya kuzoea maumivu mtalaamu?
 
Back
Top Bottom