Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Mbona wanakata tokea tozo zitangazwe... NMB nina experience nayo kwenye hili
 
Habari wakuu,
Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema.

Kwanini Serikali wasingetumia pesa za kununulia ndege zisizozalisha na gharama za kufanya royal tour kufanya yote wanayotaka kufanya. Ni muda wa kufikiria kupunguza matumizi badala ya kututoza kodi mara mbili mbili kuongeza mapato kufanya matumizi yasiyo na kipaumbele au umuhimu.

View attachment 1926880
Jenga nchi acha malalamiko kijana
 
Mama yenu huyo, mlishangilia kifo cha pjm mtamkumbuka, sasa hivi ni mwendo wa kuzurula tozo ni mwendo wa safari. Mlivyokuwa wajinga mnashangilia.
 
Bado mna maumivu? Nilisikia shangwe za umma, wake kwa waume, walio ajirani na kutoka kwa wenye wenza ajirani, wakisifu na kushangweka kuwa baada ya miaka 5 migumu, hatimaye madaraja yamepanda, wamelipwa malimbikizo, paye imepunguzwa n.k

Imekuaje tena hii kauli ya kuzoea maumivu mtalaamu?
😅😅😅😅😅😅 walishabikia kuongezwa elfu 50 kwenye mshahara? Upuuzi mtupu
 
Hamia nchi masikini zaidi ya Tanzania kama unataka unafuu wa kodi na tozo...
Ndiyo faida ya kuwa nchi yenye wananchi mafala. Viongozi wanatumbua na wananchi wanakamuliwa! Tutakiona cha mtema kuni kama hatutakuwa wakali.
 
Ndani ya MUDA MFUPI UJAO watanzania watayaona MABADILIKO MAKUBWA MNO KIJAMII NA KIMAENDELEO.....

Majibu ya hizi TOZO yatawashangaza haswa na wataielewa VYEMA serikali sikivu ya AWAMU YA 6....ni muda tu.....

#SiempreJMT
#TozoKwaMaendeleoYetuWenyewe
 
Tatizo sio kulipa kodi ambayo ilikuwa tayari inalipwa kisheria kama VAT ila wameona haitoshi wameleta kitu Tozo ok utasema nalo sawa sio tatizo lakini shida inakuja kiwango ni kikubwa sana unaweza ukasema ok sawa tatizo sio kiwango tu muamala huo mmoja unalipiwa tozo mara 4 sijui mpaka ukimfikia mlengwa ni almost 17% huu ni wizi wa wazi kabisa. Watu bado maskini sana serikali kama kweli walikuwa wana nia njema basi muamala mmoja ungelipiwa labda na mtumiaji tu sio anayepokea na kutoa tena huu ni ujangili. Badala ya kujikita kuongeza mzunguko wa pesa kwa wananchi ndio kwanza wanawabana kila leo eti tunajenga madarasa sijui zahanati kwa gharama ya kuuwa sector muhimu ya pesa.
 
Back
Top Bottom