Ego is the Enemy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 8,201
- 16,246
Habari zenu wanajukwaa.
Hili suala napenda lifike mamlaka zinazohusika.
Jamani tuliambiwa michango inajenga madarasa n.k Ila Cha kushangaza tunaanza kuibiwa kuwa tuchangie hela ya ujenzi.
Hebu afisa elimu mkoa wa mwanza ,afisa elimu wilaya,karibu elimu kata na wizara mwenye dhamana unalijua kuwa wasaidizi wako huku wamejiwekea namna ya upigaji kwa mgongo sijui wa kujifanya Kama wao wanaoipenda hii nchi.
Tozo, mafuta, hela za chanjo hazitumiki vizuri, kumbuka sie ni machinga na saivi tumefukuzwa tumepelekwa maeneo ambayo hayana wateja wanadai kufikia uchaguzi tutakuwa tumezoea. Hatuuzi kabisa hapa tulipo. Mnaanza Tena kutuletea kuwa tuchangie ujenzi wa shule kwani serikali imeshindwa kufanya wajibu wake kwa wananchi kweli Raisi Samia Hassan suluhu.
Shule zetu pendwa zimeanza michango ambayo Haina mbele Wala nyuma.
Hii shule mwezi uliopita waliomba mchango wa shilling Elfu tano (5000/=) kwa kila mwanafunzi wa darasa la sita kwa kila mwezi mpaka wanamaliza la Saba.
Mpaka la Saba Ina Mana tutakuwa tumechangja Ada ya shule jumla ya ~60k
Eti la kuwafundisha masomo ya jioni ili wakiingia sekondari wawe wanajua kusoma kabisa kabisa. Yaani wao hawawezi kufundisha kwa kazi waliyoajiriwa nayo, wamezoea mshahara wanaona ni mdogo, yaani wao hawana wito wa kufundisha mpaka wabustiwe, hawawezi kuwaza miradi mingine nje ya kufundisha wanabaki kutuumiza.
Wao wanawapenda Sana watoto wetu mpaka wanaomba kulipwa ili kuwafundisha.
Kama wanajua kuwa kusoma twisheni ndo kufaulu sijui wao ni kwa Nini hawakusoma iyo twisheni ili wafaulu matokeo Yao wakaishia kidato pendwa.
ombi langu kama walimu wanataka kufundisha twisheni basi iwe hiari kwa mtoto ama mzazi wake.
Sasa cha kushangaza MTT asipopeleka wanamchapa na kumrudisha nyumbani. Muacheni asome yale yale masomo ambayo serikali ilikuajiri uje kufundisha.
Yaani mie hapa nalia na hapa nilipo nina siku nne siuzi matunda yangu yameoza afu naombwa mchango wa ujenzi wa shule na huku tuliambiwa kuwa hela zetu zimetolewa kwa ujenzi wa madarasa manne manne kila shule.
Enzi za JPM hii michango iliisha.
Natumaini andiko langu litawafikia walengwa
Naomba niambatanishe na ushahidi kabisa