The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Ndugu The Sunk Cost Fallacy nani anatetea uzembe hapa? Ni mimi na wenzangu au wewe...?Uamzi wowote unaofanywa na Serikali sikivu ya awamu ya 6 unakuwa umefanyiwa tathmini ya athari zake vs faida..
Hakuna mtu anaweza kukata salary ya mfanyakazi kwa hivyo mnavyosema nyie,acheni kujitungia mambo ambayo hayana realistic Ili kutetea uzembe.
Sisi tunakemea uzembe wa viongozi wa serikali yako ya CCM wa kutotumia akili zao vyema ktk kubuni njia sahihi za kuingizia mapato halali nchi kwa ajili ya maendeleo na badala yake wanatumia njia za wizi wa kidola kwa kuwaibia wananchi wake hela zao kwa jina la kodi au tozo kwa kisingizio cha "..ni kwa maendeleo ya wananchi..."
Tuna rasrimali nyingi sana. Lakini viongozi wa serikali yenu ya CCM akili zao zimekufa, hazifanyi kazi tena kwa sbb ya kulewa madaraka...
Hawajui ni kwa njia gani wanaweza ku - exploit rasrimali hizi, kisha ziwe converted kuwa fedha ili wazitumie kwa matanuzi yao ya anasa na familia zao...
Badala yake, wameamua kutumia "u - Magufuli" kuwaibia wananchi wao vihela kwa njia "double taxation...."
Hii siyo sahihi wala si haki. Hii haikubaliki ndugu The Sunk Cost Fallacy...!
Jaribu kuelewa hata kwa leo tu kisha jiunge na sisi ili kukemea tabia hii mbaya ya serikali hii...
Acha kujilambia asali itakayokwisha kesho na kusahau kesho kutwa na kizazi chako...!!
Think Big. Think about your children and grandchildren's future. Usidhani kuwa, kwa sababu wewe unashiba leo, basi na watoto wako watakuwa ktk hali hiyo. Never.
Kemea na pinga ubaya leo ili usiwaathiri watoto wa watoto wako huko mbeleni...!!