Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Wengi unaobishana nao hapa walikuwa mataga wenye nyodo na kebehi kama za kwako. Musiba alifikia kusema hadi tuanzishe World Bank ya Africa.
You're disgrace to our country.
Serikali huwa haibembelezi watu kulipa Kodi.
 
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za Serikali. Hii ni kanuni mama ya kodi.

Kanuni kuu ya pili, mapato yalikwishalipiwa kodi, tozo au ushuru hayastahili kulipishwa tena kwa mara ya pili. Double taxation inazuiwa.

Wizi ni kuchukua kitu chochote ambacho siyo stahili yako. Wizi huu unaweza kuwa wa mtu mmoja dhidi ya Serikali, taasisi, mtu mwingine au kikundi au Serikali dhidi ya wananchi wake au dhidi ya mwananchi mmoja.

Serikali inapomtoza mwananchi kodi zaidi ya kiwango halali au zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, huo ni wizi wa dola dhidi ya mwananchi.

Maswali muhimu ya kujiuliza:

1) Kwa mfano, mfanyakazi au mfanyabiashara amepata mshahara au pesa ya mauzo, ameilipua kodi tayari, ikawekwa benki, benk amelipia gharama ya huduma, na benki inalipa kodi kwa mapato yanayotokana na utoaji huduma, huyu mteja anapotaka kuichukua pesa yake, akatozwa tena na Serikali, ni mapato gani ameyapata kule benki?

2) Kwa mfano, mfanyakazi, kwenye mshahara wake amekatwa PAYE, pesa imeenda benki, anatoa kwenye ATM, anakatwa kodi kwa mara ya pili, anaweka kwenye simu, pesa ile ile anaituma kwa mama yake kijijini anakatwa kodi, mama yake anaenda kwa wakala kuchukua ile pesa, anakatwa kodi.

Pesa siyo chakula, lazima huyu mama ataitumia, anaenda kununua chumvi anakatwa kodi. Yaani makato mara 5 kwa mapato yale yale, hii ni halali? Lakini ikumbukwe kwamba, benki kutokana na mapato yake yanayotokana na utoaji huduma imekatwa kodi, mtandao wa simu kutokana na mapato ya utoaji huduma ya usafirishaji fedha, nao umekatwa kodi, na muuzaji wa chumvi naye amekatwa kodi.

Tax regime ya Tanzania ni lazima iangaliwe upya. Siyo regime rafiki kwa wananchi wala wawekezaji.

Siku zote kodi utitiri au kubwa huua uwekezaji. Hakuna nchi hata moja Duniani iliyokuwa maskini ambayo iligeuka kuwa tajiri kwa haraka kwa kuwa na kodi utititiri au kodi kubwa.

Dubai, ilipata maendeleo makubwa, na kubadilika kabisa ndani ya miaka 15 tu kwa kufuta kabisa kodi nyingi na kubakia na kodi chache sana. Mpaka leo Dubai ni kituo cha biashara Duniani.

Anayehamasisha Tanzania kuwa na kodi utitiri na kodi kubwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu.

Nchi hii inahitaji sana uwekezaji ili watu wetu wapate ajira, na Serikali iwe na vyanzo vingi vya mapato, na siyo kuongeza kodi kwa vyanzo vile vile.

Wazalendo wa nchi hii, wanaoitakia mema Tanzania tukatae mambo yote yanayoua uwekezaji katika Taifa letu.

Tukiwa na sera na sheria ambayo inachochea uwekezaji kivitendo, kama uwekezaji utasababisha japo watanzania milioni 15 kupata ajira za uhakika, na hao milioni 15 angalao kila mmoja kwa wastani akalipa kodi ya sh milioni 4 kwa mwaka, PAYE pekee yake itaipatia Serikali 4,000,000×15,000,000 = 60,000,000,000,000 (trillion 60).

Haya ni mapato ambayo ni karibu 50% ya makusanyo ya Serikali kwa sasa. Na haya ni mapato ambayo Serikali itayapata, na huku mlipa kodi akifurahi kwa kuwa ana ajira inayompa kipato cha uhakika.
Eee bhana hebu mcheki Kibatala iwapo tunaweza kufungua jalada la kesi kwa mambo haya
 
Kodi au tozo haziwahi kuwa wizi ndio maana nilikuuliza kama ni wizi hizi pesa zinaenda kutumika wapi? Hukujibu..pesa inatumika kuboresha huduma mbalimbali kama hizi [emoji116]

Kwa hiyo mkuu unataka kusema hata kesho serikali iseme mishahara ikatwe nusu kwa watumishi wote itabidi watumishi wafurahie tu kwa vile zinaenda kutumika huko?

Nadhani uelewe mantiki ya mtoa mada, hakuna anayekataa kulipa kodi wala tozo.

Kinachojadiriwa ni uhalali wa hizo makato. Mapato hayo hayo hayawezi pitia kodi na tozo.

Itabidi ifikie hatua sasa kila mtumishi ama yeyote yule apate malipo mkononi, ili liwe jukumu lake sasa la kuweka benki ama kwenye simu.

Hizi vitu zinaweza leta bank crisis ambayo itapelekea hata financial crisis.

Fikiria tu 40% wapunguze kutumia bank hali itakuwaje.

Mtu mwenye 1m bank ataona heri aitoe yote akaitunze nyumbani tu. Ni kwa kiasi gani bank zinaenda kukosa hela za kukopesha.
 
Lipa tozo ya uzalendo
Ile ya vitambulisho vya wanachonga iliitwa hivyo hivyo "kodi ya uzalendo" kumbe ulikuwa wizi mtupu...

Mzalendo wenye kodi/tozo hizi kata na "kodi ya uzalendo" wake...

Ghafla kajitokeza Mwigulu Nchemba na msamiati huohuo wa ki - Magufuli kwa kumzunguka huyu mwanamke dhaifu asiye na lolote lakini anajiita eti "Rais" wa nchi....!!

Nakuambia hivi, akifa Mwigulu leo na huyu mama yenu, atakuwa ameondoka na wizi wake huu...!!
 
Sina hakika kama huyu The Sunk Cost Fallacy anaweza kukuelewa...

Yuko hapa kutetea ujinga na siyo mantiki...!

Na watu wa dizaini ya The Sunk Cost Fallacy hutetea hata wafunuliwe kweli yote machoni pao, wanaweza kuyakana hata majina yao...!!
 
Suala la tozo si la nchi bali ninla Tanganyika isiyo na uongozi wala msemaji wa kuwatetea watanganyika. Ukiona mambo yamezidi nenda Zanzibar, huko mambo ni shwari kabisa.
 
Ile ya vitambulisho vya wanachonga iliitwa hivyo hivyo "kodi ya uzalendo" kumbe ulikuwa wizi mtupu...

Mzalendo wenye kodi/tozo hizi kata na "kodi ya uzalendo" wake...

Ghafla kajitokeza Mwigulu Nchemba na msamiati huohuo wa ki - Magufuli kwa kumzunguka huyu mwanamke dhaifu asiye na lolote lakini anajiita eti "Rais" wa nchi....!!

Nakuambia hivi, akifa Mwigulu leo na huyu mama yenu, atakuwa ameondoka na wizi wake huu...!!
Ule ulikuwa wizi ila tozo ina sheria na miongozo na iko specific kwa inachoenda kufanya.
 
Sina hakika kama huyu The Sunk Cost Fallacy anaweza kukuelewa...

Yuko hapa kutetea ujinga na siyo mantiki...!

Na watu wa dizaini ya The Sunk Cost Fallacy hutetea hata wafunuliwe kweli yote machoni pao, wanaweza kuyakana hata majina yao...!!
Uamzi wowote unaofanywa na Serikali sikivu ya awamu ya 6 unakuwa umefanyiwa tathmini ya athari zake vs faida..

Hakuna mtu anaweza kukata salary ya mfanyakazi kwa hivyo mnavyosema nyie,acheni kujitungia mambo ambayo hayana realistic Ili kutetea uzembe.
 
Ili nchi iendelee inahitaji.
Watu
Siasa safi
Utawala Bora.
Sisi hatuna watu hivyo tumekosa vyote.
 
IMG-20220821-WA0277.jpg
 
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za serikali. Hii ni kanuni mama ya kodi.

Kanuni kuu ya pili, mapato yaliyokwishalipiwa kodi, tozo au ushuru hayastahili kulipishwa tena kwa mara ya pili. Double taxation inazuiwa.

Wizi ni kuchukua kitu chochote ambacho siyo stahili yako. Wizi huu unaweza kuwa wa mtu mmoja dhidi ya Serikali, taasisi, mtu mwingine au kikundi au serikali dhidi ya wananchi wake au dhidi ya mwananchi mmoja.

Serikali inapomtoza mwananchi kodi zaidi ya kiwango halali au zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, huo ni wizi wa dola dhidi ya mwananchi.

Maswali muhimu ya kujiuliza:

1) Kwa mfano, mfanyakazi au mfanya biashara amepata mshahara au pesa ya mauzo, ameilipia kodi tayari, ikawekwa benki, benki amelipia gharama ya huduma, na benki inalipa kodi kwa mapato yanayotokana na utoaji huduma, huyu mteja anapotaka kuichukua pesa yake, akatozwa tena na serikali, ni mapato gani ameyapata kule benki?

2) Kwa mfano, mfanyakazi, kwenye mshahara wake amekatwa PAYE, pesa imeenda benki, anatoa kwenye ATM, anakatwa kodi kwa mara ya pili, anaweka kwenye simu, pesa ile ile anaituma kwa mama yake kijijini anakatwa kodi, mama yake anaenda kwa wakala kuchukua ile pesa, anakatwa kodi.

Pesa siyo chakula, lazima huyu mama ataitumia, anaenda kununua chumvi anakatwa kodi. Yaani makato mara 5 kwa mapato yale yale, hii ni halali? Lakini ikumbukwe kwamba, benki kutokana na mapato yake yanayotokana na utoaji huduma imekatwa kodi, mtandao wa simu kutokana na mapato ya utoaji huduma ya usafirishaji fedha, nao umekatwa kodi, na muuzaji wa chumvi naye amekatwa kodi.

Tax regime ya Tanzania ni lazima iangaliwe upya. Siyo regime rafiki kwa wananchi wala wawekezaji.

Siku zote kodi utitiri au kubwa huua uwekezaji. Hakuna nchi hata moja duniani iliyokuwa maskini ambayo iligeuka kuwa tajiri kwa haraka kwa kuwa na kodi utititiri au kodi kubwa.

Dubai, ilipata maendeleo makubwa, na kubadilika kabisa ndani ya miaka 15 tu kwa kufuta kabisa kodi nyingi na kubakia na kodi chache sana. Mpaka leo Dubai ni kituo cha biashara duniani.

Anayehamasisha Tanzania kuwa na kodi utitiri na kodi kubwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu.

Nchi hii inahitaji sana uwekezaji ili watu wetu wapate ajira, na serikali iwe na vyanzo vingi vya mapato, na siyo kuongeza kodi kwa vyanzo vile vile.

Wazalendo wa nchi hii, wanaoitakia mema Tanzania tukatae mambo yote yanayoua uwekezaji katika taifa letu.

Tukiwa na sera na sheria ambayo inachochea uwekezaji kivitendo, kama uwekezaji utasababisha japo watanzania milioni 15 kupata ajira za uhakika, na hao milioni 15 angalau kila mmoja kwa wastani akalipa kodi ya sh milioni 4 kwa mwaka, PAYE pekee yake itaipatia Serikali 4,000,000×15,000,000 = 60,000,000,000,000 (trillion 60).

Haya ni mapato ambayo ni karibu 50% ya makusanyo ya serikali kwa sasa. Na haya ni mapato ambayo serikali itayapata, na huku mlipa kodi akifurahi kwa kuwa ana ajira inayompa kipato cha uhakika
tatizo ni kuwa na viongozi walemavu wa fikra,walianza na tozo za simu wakaona haitoshi,wakaja na tozo za luku,wakaona haitoshi sasa wamekuja na tozo za miamala ya kibenki ,tunapoelekea bidha moja inaweza kutozwa kodi mara nyingi,kunamsemo usemao usipotawanya huwezi kukusanya,huu ndio mzizi wa fitina wa uchumi wetu,watawla hawaja tawanya ,hawawekezi kwa wanachi ila wanataka kuchukua kodi inatoka wapi?,sasa inawalizimu wahamie kwenye vyanzo vya uporaji wa kidola ili kujinusuru na aibu ya kuangusha uchumi.,hizi sio tozo bali ni uporaji.viongozi wanapaswa kuwa wachumi na sio makada kama wengi wao walivyo,sekta nyeti wanapewa makada,wasomi feki wa kukariri,mtu anabay hajato jasho kwenye biashara yake binafsi hawezi kuwa mchumi mzuri
 
Watanzania tutaendelea kulipa tozo na pia tunaishauri Serikali kuangalia kama kuna njia nyingine ya kuchangia maendeleo yetu basi tupo tayari kabisaa.
Chini ya Rais wetu Mama Samia tunaona matumizi ya fedha zetu, tunaona miundombinu inajengwa, maji safi, afya n.k.
 
Hata wawekezaji watakimbia sasa....
Kampuni yenye wafanyakazi 100 inapoteza zaidi kila inapomlipa mfanyakazi mshahara sababu ya tozo ya kutuma mshahara,
 
Kwa hiyo Chadomo mkiongoza Nchi hautachukua loan? 😁😁.

Kuna Nchi haichukui loan Dunia hii?

Nakupa mfano mdogo,Tzn ina jumla ya km za barabara za TanRoads na Tarura zaidi ya 160,000 Kati ya hizo lami ni km 12,000 tuu Sasa tukisema tuende kwa Kasi hii ya kujenga km 600 za lami kwa mwaka sasa unategemea hizo barabara zitafikiwa lini?

Sasa iko hivyo across sectors na mahitaji yanazidi kuongezeka kwa sababu ya ongezeko la watu so loan zinasaidia kupunguza makali ya Kodi in short term na pia kutatua shida za dharura.
Kila mtu ni chadema au sio wewe kenge
 
Mpuuzi tu wewe,kwa hio wanaolalamika kuhusu tozo ni chadema na sukuma gang tu?Nicampoomp
Mbaolalamika ni joblesa wa mitandaoni huko kitaa watu wako busy na biashara zao na wamejaa banks kama kawaida isipokuwa nyie konokono WA humu mitandaoni sasa.
 
Back
Top Bottom