Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Ndugu The Sunk Cost Fallacy nani anatetea uzembe hapa? Ni mimi na wenzangu au wewe...?

Sisi tunakemea uzembe wa viongozi wa serikali yako ya CCM wa kutotumia akili zao vyema ktk kubuni njia sahihi za kuingizia mapato halali nchi kwa ajili ya maendeleo na badala yake wanatumia njia za wizi wa kidola kwa kuwaibia wananchi wake hela zao kwa jina la kodi au tozo kwa kisingizio cha "..ni kwa maendeleo ya wananchi..."

Tuna rasrimali nyingi sana. Lakini viongozi wa serikali yenu ya CCM akili zao zimekufa, hazifanyi kazi tena kwa sbb ya kulewa madaraka...

Hawajui ni kwa njia gani wanaweza ku - exploit rasrimali hizi, kisha ziwe converted kuwa fedha ili wazitumie kwa matanuzi yao ya anasa na familia zao...

Badala yake, wameamua kutumia "u - Magufuli" kuwaibia wananchi wao vihela kwa njia "double taxation...."

Hii siyo sahihi wala si haki. Hii haikubaliki ndugu The Sunk Cost Fallacy...!

Jaribu kuelewa hata kwa leo tu kisha jiunge na sisi ili kukemea tabia hii mbaya ya serikali hii...

Acha kujilambia asali itakayokwisha kesho na kusahau kesho kutwa na kizazi chako...!!

Think Big. Think about your children and grandchildren's future. Usidhani kuwa, kwa sababu wewe unashiba leo, basi na watoto wako watakuwa ktk hali hiyo. Never.

Kemea na pinga ubaya leo ili usiwaathiri watoto wa watoto wako huko mbeleni...!!
 
Ku extract rasilimali inatakiwa pesa na pesa ndio hizi zinapatikana kwa njia nyingi ikiwemo tozo..

Acheni ubinafsi na upuuzi usio na msingi lipa tozo Kazi iendelee
 
Hivi hivyo vituo vya afya vimejengwa wapi?
Mbona huku nilipo nimetembelea kata tano na zote hazina vituo vya afya?
 
Hivi hivyo vituo vya afya vimejengwa wapi?
Mbona huku nilipo nimetembelea kata tano na zote hazina vituo vya afya?
Huko wapi? Kutaje Ili tuone kwenye list..

Hata hivyo Tanzania ina kata zaidi ya 3,950 na Kati ya hizo vituo vya afya kwa ujumla wake havizidi 1,200 Nchi nzima so hapo unaweza ona kwamba zaidi ya nusu ya kata hazina so Kazi bado kubwa ya kufanya.

Ila cha kufahamu ni kwamba hakuna Jimbo ambalo hakuna Kituo Cha afya walau kimoja au viwili vinajengwa..

Mfano soma hapa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220812-104841.png
    268.4 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220812-104856.png
    259.9 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220723-121202.png
    107.8 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220719-085937.png
    143 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220713-194118.png
    155.5 KB · Views: 2
Ku extract rasilimali inatakiwa pesa na pesa ndio hizi zinapatikana kwa njia nyingi ikiwemo tozo..
Mimi ni mkristo ndugu The Sunk Cost Fallacy. Sijui wewe ni dini gani...

Katika biblia 1 Yoh. 5:17 imeandikwa hivi..

"..kila LISILO HAKI ni dhambi, na iko dhambi isiyo ya mauti..."

Ni sawa wanapata pesa. Lakini wanaipata kwa njia ya haki...?

Unajua ukiniibia mimi pesa, utakuwa umepata pesa na utaitumia kwa mambo yako na utatamba mitaani kuwa umeula, umetajirika...

Lakini unapotamba umejenga nyumba lakini kwa fedha ya wizi, wewe mwenyewe ktk nafsi yako utakuwa unajisikiaje...?

Ni wazi utakuwa unahukumiwa, au siyo. Utakuwa una nyumba, NDIYO....

akini hukuipata kwa njia halali. Umeipata kwa wizi. Utaudanganya umma lakini nafsi haidanganyiki...!!

Ndicho inachofanya serikali yako. Inaibia wananchi wake kwa hoja kuwa ni kwa maendeleo yao...

Hii siyo HAKI. Ni laana kuwaibia wasionacho na masikini..


Acheni ubinafsi na upuuzi usio na msingi lipa tozo Kazi iendelee
Wewe na wenzako huko serikalini ndiyo muache ujinga, upuuzi na uzembe wa kutofikiri vyema...!

Tumieni akili zenu alizowapa Mungu bure kabla hajawanyang'anya hizo akili ndogo mlizobakisha kabisa pamoja na vyote kurekebisha makosa haya...

Mungu anawaona eti. Mungu hajalala eti. Msifikiri Mungu hawezi kuweka watu wengine kuiongoza nchi hii na watu wake..

Waambie wenzake, wasije kulalamika kuwa hatukuonywa...!
 
ilimradi maendeleo tanayaona hakuna shida kabisaaa......tozo iendelee tena nashauri ziangaliwe njia nyingine za kuchangia maendeleo yetu, badala ya kuchangia harusi na masharehee mengine sasa tunaweza kuchangia 1200 maendeleo ya barabara zetu, hospitali, maji n.k

Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.
tusitegemee kujengewa nchi yetu na mataifa mengine.

wala tusifikirie eti jinsi awamu ya 1 hadi ya 6 walivyo ongoza lazima ifanane na awamu hii ya 5, kila kiongozi anamaono yake ya kutuletea maendeleo.

Tutaendelea kulipa tozo bila shida yoyote.
 
Kwa hizi facts, Kibatala & co. wangekuwa wazalendo wangeiburuza serikali mahakamani ili kuwatetea watu wa kipato cha chini waliotoa jasho la damu kuwawezesha kupata hiyo elimu ya sheria waliyo nayo.
 
Madhara ya hii tozo ya benki bado kidogo tu yataanza kuonekana Sasa hivi wengi wanatoa pesa zao benki wanapeleka nyumbani na wenye frdha nyumbani hawapeleki benki fedha zinaondoka kwenye mzunguko baadae benki zitaathirika kwani kazi ya benki ni kutunza hela na kuzifanyia biashara na kutoa gawio kwa Serikali in the long run madhara yatakuwa wazi
 
Hii nchi ina laana.
Akili ndogo ndio wanaopanga mikakati ya nchi na watanzania tukiwa tumelala. Sisi si tulikubali kuwa wanyonge. Tutaendelea kunyonywa
Sio lazima kusoma uwe kiongozi ,ishu kubwa Ni talanta ya kuingiza Basi. Sasa saivi hatutaki wenye elimu kubwa hata cheti Cha fomu Foo vya miaka mitatu kwa pamoja vinakubalika.
Kila mwaka c zako na d ama na f kadhaa balansi zinajumlishwa kwa pamoja
 
Mkiambia serikali hii haifai mnamsifia eti ana upiga mwingi!!!! Seriously?
 
Nashauri Kodi ziongezeke zaidi kwani ni kwa Maendeleo yetu wana wa nchi
 
Nashauri Kodi ziongezeke zaidi kwani ni kwa Maendeleo yetu wana wa nchi
Kodi inabidi ziwe rafiki,ziwafanye watu walipe
Ukiweka makodi ambayo yatamuumiza mfanyabiashara/watu
Utafanya watu waingie kwenye kufanya mambo ndivyo sivyo
We unafikiri kwanini watu wanafanya biashara za magendo!

Kingine,unaweza mtoza watu kodi za biashara zao,wakati wao hawana uwezo wa kulipa kiasi cha kodi ulichowapangia...mwisho wa siku anaacha biashara,sasa hapo utakuwa umemjenga au kumbomoa

Hao wanaolipisha makodi na matozo je wanafanya nini kuwainua watu kiuchumi wawe na fedha,je wanafanya hilo

Ova
 
Nimekerwa na serikali hii kwa tozo za benki.
 
Mtapiga makelele wewe ila come 2025 mtakapokuta kila Kijiji kina maji,kina barabara,kina Zahanati na vituo vya afya ,kina umeme nk mtajua kwamba kumbe mlikuwa wajinga.
Maisha ni leo siyo mwaka 2025. Wengi wanatafuta kuishi leo siyo kesho. Tozo zaidi ya 1% kwa muamala siyo sahihi. Benki nyingi za biashara zinatoa asilimia 4 tu- huku pesa yako imekaa mwaka mzima. Lazima watu wenye uwezo mdogo wasaidiwe na serikali kupunguza ukali wa maisha - vitu vingi vimepanda bei. Watu wana njaa leo siyo 2025. Huu mtazamo wa 2025 bila kujali maisha ya leo - si sahihi.
 
Mjadala wa tozo umefungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…