Kocha Ramovich ameanza kuipata timu, leo kapanga timu vizuri ila nimemkubali sana kwa sub alizofanya na kafanya sub kwa wakati sahihi, sio kuingiza wachezaji dkk ya 80 wakashangae tu, nimefurahi sana hakujali jina wala muda wa kumtoa nje mchezaji yoyote. Sub walipata muda wa kutosha kupambana. Safi sana kocha.
Mbele za Mungu nasema niliona goli la kusawazisha baada ya sub ya Dube, maana yake kiufundi timu iliingiza nguvu mpya tano na kuwapa zaidi ya nusu saa kuzoea mechi na kupambana , unakosaje goli hapo? Keep it up kocha Ramovich umeanza kuisoma timu. Ingiza sub haraka kuanzia dkk ya 46 hadi 60 sio waingie dkk ya 85 huko ni ujinga mtupu.
Ila Ramovich alipaswa kumuanzisha Nondo maana goli tumefungwa la kichwa mshambuliaji kamzidi urefu beki akafunga kwa kichwa kirahisi . Wakati mwingine kocha aangalie urefu pia. Walio karibu yake wamwambie. Timu inayokupa matokeo mazuri ndio ya kwenda nayo!