TP Mazembe huenda likawa daraja la Simba SC Klabu Bingwa Afrika

TP Mazembe huenda likawa daraja la Simba SC Klabu Bingwa Afrika

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya TP Mazembe baada ya kutoka sare na CR Belouizdad ya Algeria, mchezo uliopigwa nchini DRC, TP Mazembe imeendelea na kukumbwa na mzimu wa sare ya pili mfululizo baada ya Jana February 24, 2021 kulazimishwa sare ya kutofungana na Al Hilal SC ya Sudan katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

Kwa sasa ni dhahir kuwa mpira umebadilika sana na kila zama na watu wake, ubora umepungua kwa Klabu ya TP Mazembe kwa msimu huu tofauti na miaka iliyopita kwasababu walikuwa na uwezo wa kushindana na kupambana mpaka ushindi hatimaye kushinda ubingwa.

Mechi...2
Ushindi...0
alama..2
Kupoteza..0
Goli...0

Msimamo wa kundi B klabu bingwa Afrika.

1. Mamelodi> mechi 1 alama 3
2. TP Mazembe> mechi 2 alama 2
3. CD Belouizdad> mechi 1 alama 1
4. Al Hilal Omdurman> mechi 2 alama 1

Kwa sasa maji yamekorogeka TP Mazembe na inashtua kuona sare ya pili mfululizo na huenda likawa daraja la Simba SC kuvuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu, endapo watakutana kwenye hatua ya robo fainali.
 
Hebu tudadavulie hapo, huyo mamelodi mechi moja alama 2 amezipataje
 
Kama Simba tunatakiwa kufocus kwenye kuvuka makundi shughuli ambayo hatujaimaliza bado....hizo habari za kufuatilia timu nyingine na kuanza kujilinganisha nazo as if tumeshavuka makundi ni kujipotezea concetration na mara nyingi hufanywa na malimbukeni wa mpira wasiojua ukatili wa matokeo ya football.

Let Mazembe alone tu focus kwenye game zetu na Al Marehk.
 
Kama Simba tunatakiwa kufocus kwenye kuvuka makundi shughuli ambayo hatujaimaliza bado....hizo habari za kufuatilia timu nyingine na kuanza kujilinganisha nazo as if tumeshavuka makundi ni kujipotezea concetration na mara nyingi hufanywa na malimbukeni wa mpira wasiojua ukatili wa matokeo ya football.

Let Mazembe alone tu focus kwenye game zetu na Al Marehk.
Hakuna la ajabu hapo ila kwa yule ambaye hajui Football, Klabu lazima kufuatia Ligi yote na matokeo hasa ukizingatia TP imekuwa kikwazo cha Simba kuvuka hatua inayofuata, hata kama kwa sasa jicho kwanza lipo kwa Al Merrikh.
 
Na kama ni hivyo mechi ya mamelod na waarabu hapo taifa jumapili sio ya kukosa..
Kabisa, hasa ukizingatia Mamelodi Sundowns wameomba sana support kutoka kwa Watanzania hasa mashabiki wa Simba..!
 
Endapo Timu ya Algeria Belouzdad na Tp-mazembe mmojawapo akakutana na Simba robo fainali, naiona kabisa Simba ikifuzu nusu fainali.
Hili kundi (B) Mamelod kapata mserereko na ana uwezekano wa kujikuaanyia points 14-18
 
Mwamedi fc akicheza kwa kiwango kama kile alichokionesha uwanja wa Taifa dhidi ya Al Ahly kiasi cha kuwafanya kupoteana uwanjani, basi anaweza kufika hata nusu fainali.

Muhimu tu wasiingie na PAKA uwanjani. Kwenye hii mechi ya juzi kama wangeurudia ule umbumbumbu wao walioufanya kwenye ile mechi na FC Platinum, hakika dunia yote ingetuponda, kutudharau na pia kuliongelea zaidi hilo tukio badala ya ushindi walio upata.
 
Kocha wa TP mazembe analaumiwa kwa kosa la kuwaacha kuwachezesha wachezaji wazoefu na badala yake ana deal na vijana wakina Mputu na wengine wa zamani wanasugua benchi, hilo ndilo kosa ambalo linaifanya timu isipate matokeo mazuri uwanjani
 
Back
Top Bottom