Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Klabu ya TP Mazembe imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) mwaka huu baada ya kufungwa bao 1-0 na MC Alger katika mchezo uliochezwa usiku wa Januari 10.
Timu hiyo ya DR Congo kwa sasa ina alama 2 baada ya mechi 5, na haina nafasi yoyote ya kusonga mbele hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho.
Msimamo Kundi A
Huku pia Klabu ya Yanga ikikabiliwa na mechi ngumu ugenini siku ya Jumapili, Januari 12 dhidi ya Al Hilal SC waliokata tiketi ya kucheza robo fainali katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Stade de la Capitale huko Nouakchott, Mauritania saa 4:00 Usiku.
Wananchi wanatakiwa kushinda mbele ya Wababe hao wa Sudan ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu Robo Fainali CAF kabla ya kukutana na MC Alger, Benjamin Mkapa Januari 18 kwenye mechi ya mwisho ya kujua hatma yao.
Pia, Soma: FT: MC Alger 1-0 TP Mazembe | CAF Champions League | Stade de 5 Juillet | 10.01.2025
Msimamo Kundi A
Pia, Soma: FT: MC Alger 1-0 TP Mazembe | CAF Champions League | Stade de 5 Juillet | 10.01.2025