TP Mazembe waomba kufundishwa football management na Yanga

Kumbe TPL iliwahi kuwa na idadi ya mechi 49 kwa misimu miwili (2016/2017) tu, na Makolokolo SC ikaweka rekodi ya unbeaten run? Kweli hata vichaa huona Watu timamu ni vichaa [emoji848][emoji38]

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Matusi hayo,Hamna hata nusu kikombe cha Africa wao wanacho,hamna hata uwanja wao wanao kisha waje kujifunza kwa mbumbumbu?
Football club nyingi za Africa zinazomilikiwa na mtu binafsi zina matumizi mabaya ya pesa. Hali hiyo hupelekea kuyumba kwa mmiliki wa timu na kuamua kuitelekeza kama ambavyo Mo amefanya mara kdhaa na baadae hurudi kwa mapenzi yake. Timu nyingi hazijiendeshi kitaasisi kiasi kwamba mmiliki akipitia changamoto na timu inakuwa kwenye changamoto kama ilivyokuwa kwa Moses Katumbi na Mazembe.

Yanga imepitia hali hizo pia. Mfadhili alipopitia misukosuko na timu ilipitia wakati mgumu sana mpaka alipopatikana GSM. Jambo zuri GSM alipata ushauri mzuri mapema wa namna ya kuzitumia pesa zake . Lakini wazo kuu likawa kufanya transformation wa namna ya kuendesha timu tofauti na utaratibu wa kijima uliozoeleka ambao haukuwa na faida kwa zaidi ya kuifanya kuwa ombaomba.

Kwenye eneo la kiuongozi Yanga imefanikiwa sana kuwa transformed. Na matokeo ya transformation hiyo ya uongozi yameonekana uwanjani hata kama timu haijachukua kombe.

Kunapokuwa na matokeo mazuri uwanjani lazima yataonekana tu. Kupitia mafanikio hayo imekuwa rahisi kwa Rais wa Yanga kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa vilabu baroni Africa. Mnafikiri imekuja kwa bahati tu? Hapana. Kuna jambo limefanyika. Iliwahi tokea wakati Simba ikifanya vizuri CEO wake Babra aliteuliwa kuwa mmoja wa wanakamati za CAF.

Mazembe wanahitaji transformation ya kuendesha timu kutoka kwenye kutegemea maamuzi ya mtu mmoja na kuwa na proper structure ya uongozi. Na hii itaisaidia Tp Mazembe kwa miaka mingi. Mazembe hawana mashabiki waliowasajiri kidigitali na kama wapo ni kwa idadi ndogo sana na hili wanalipitia pia Mamelodi, hili pia wanaweza kujifunza kutoka kwa Yanga kwa kuwa ndio timu iliyofanikiwa kwenye kipengele hicho kwa ukanda huu hata kama sio kwa kiwango kikubwa lakini mapato yanaonekana.

Mambo ni mengi ambayo Tp Mazembe wanaweza kudesa toka kwa Yanga ili waweze kujiendesha hapo baadae Moses Katumbi atakapokuwa hayupo. Na huenda desa hili likawanufaisha zaidi Mazembe kuliko Yanga yenyewe.

Mazembe ni kubwa kimafanikio kuliko Yanga kimataifa na kipesa huenda. Lakini hatuna uhakika kama ikitokea sheria ya Financial fair play ikaja Africa kama Mazembe, Yanga na timu nyingine zitaweza kujiendesha. Ndio maana kunahitajika Transformation mapema sana.
Inasemekana Nigeria walichukua desa la makao makau yao kutoka ramani ya Dodoma na haimaanishi Tanzania ilikuwa imefanikiwa kuliko Nigeria
 
kule champion leuge awamu hii hata wale waliotudhulumu tutawavunja ngoko na hata viuno wasisubutu kujaribu kutuzuia tena kwa dhuluma
Kule CAFCL hatukudhurumiwa ndugu, Yanga haina wapigaji wazuri wa penati na hiyo ndiyo sababu iliyotufanya tuishie robo.

Ni vyema viongozi wakafanya usajili wa maana ili CAFCL ijayo tutwae kombe kabisa
 
Wanafundishwa jinsi ya kutuma miamala kwa marefa
 
Nilikua Borgsburg naangalia mpira Wazambia na Wapopo walikuwepo nifurahi kuona wanaipa Heshima Yanga maana huku Dzonga walikua wanatudharau sana toka tumewakimbiza Mamelodi wametupa heshima yetu..
 
Kule CAFCL hatukudhurumiwa ndugu, Yanga haina wapigaji wazuri wa penati na hiyo ndiyo sababu iliyotufanya tuishie robo.

Ni vyema viongozi wakafanya usajili wa maana ili CAFCL ijayo tutwae kombe kabisa
Goli la key 🔑. Lililochinjiwa baharini na V.A.R na referee akashindwa kuhakiki na kutoa haki🤔
 
Goli la key 🔑. Lililochinjiwa baharini na V.A.R na referee akashindwa kuhakiki na kutoa haki🤔
Huyo huyo key 🔑alipopewa nafasi ya kwanza kwenye kupiga penati alimpasia tu Williams badala ya kushusha shuti la nguvu ili kurudisha goli lake alilodhurumiwa.

Tukubali tu Yanga hatuna wapigaji wazuri wa penati, viongozi wetu wafanye sajili za maana ili kuzlrekebisha kasoro zilizo tokea pale Pretoria zisijirudie kwa msimu ujao wa CAFCL.
 
Nilikua Borgsburg naangalia mpira Wazambia na Wapopo walikuwepo nifurahi kuona wanaipa Heshima Yanga maana huku Dzonga walikua wanatudharau sana toka tumewakimbiza Mamelodi wametupa heshima yetu..
Yanga ni kama maji mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…