ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Tp mazembe nayo imeisha..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dogo kaangalia mbele. Nina uhakika hata Samata alianza hivyo mdogo mdogo na thamani yake ikapanda baada ya kuonyesha uwezo.TP Mazembe imesajili mshambuliaji wa Mbeya City kwa dau la milioni 50 kwenda Mbeya city. Ambokile amesajiliwa kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib aliyegoma
Ambokile aliefunga goli 10 mzunguko wa Kwanza wa ligi kuu Tanzania ambapo mzunguko wa pili alienda kwa mkopo Black Leopard ya South Africa ambapo hakucheza kutokana na kukosa kibali kwa wakati.
Ambokile amesaini mkataba wa miaka 3 na nusu, ataanza kuitumikia Mazembe kwenye michuano ya Cecafa Huku Simba na Yanga zikijitoa
View attachment 1132264
Tp mazembe nayo imeisha..
Hahahaha, Mazembe waishe ? Ngoja uone visu vitakavyochomolewa AFCON ,na hivi Anko Moise Katumbi yuko , huyo Dogo kusajiliwa usidhani Mazembe wazembeTp mazembe nayo imeisha..
Eliud Ambokile ni mchezaji mzuri sana tena ana umri mdogo na ndicho tim kubwa huangalia.Kwanza nimtakie kila la heri kijana wa nyumbani Tanzania kwa kupata fursa ya kucheza mpira kwenye timu kubwa Kama TP Mazembe. Akakaze azidi kufanikiwa zaidi kimpira na kimaisha kwa maslahi yake, familia na taifa.
Lakini nina swali kidogo kwa wenye kuijua TP Mazembe, labda mimi naipa ukubwa usioistahili (na exaggerate), Hivi kwa ukubwa wa timu ile, ni kweli wanasajili wachezaji aina ya Ambokile toka nchi nyingine ? Au wako desperate.... mimi nilikua nawaza kwamba TP wanatakiwa kuchukua wachezaji ambao ni the finest katika nchi husika hasa kutoka nchi kama Tanzania.
Ambokile ni mzuri sawa lakini mimi naona TP ni kubwa mno kwake. Kwa mfano, kwenye kikosi cha timu ya taifa cha wachezaji wa ndani Ambokile asipoitwa hakuna anayeweza kushangaa.
TP wamemchukua kwa madhumuni yapi, kwamba Congo mtu wa uwezo sawa na Ambokile hakuna ?
My take:
Nadhani timu zote za Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara wana tatizo linalofanana kwenye suala la recruitment ya wachezaji wa nje, nadhani Scouting sio nzuri sana.
Sijui wenzangu mna maoni gani ?