TP Mazembe yamsajili Ambokile wa Mbeya city

TP Mazembe yamsajili Ambokile wa Mbeya city

TP Mazembe imesajili mshambuliaji wa Mbeya City kwa dau la milioni 50 kwenda Mbeya city. Ambokile amesajiliwa kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib aliyegoma

Ambokile aliefunga goli 10 mzunguko wa Kwanza wa ligi kuu Tanzania ambapo mzunguko wa pili alienda kwa mkopo Black Leopard ya South Africa ambapo hakucheza kutokana na kukosa kibali kwa wakati.

Ambokile amesaini mkataba wa miaka 3 na nusu, ataanza kuitumikia Mazembe kwenye michuano ya Cecafa Huku Simba na Yanga zikijitoa

View attachment 1132264
Dogo kaangalia mbele. Nina uhakika hata Samata alianza hivyo mdogo mdogo na thamani yake ikapanda baada ya kuonyesha uwezo.
 
Kwanza nimtakie kila la heri kijana wa nyumbani Tanzania kwa kupata fursa ya kucheza mpira kwenye timu kubwa Kama TP Mazembe. Akakaze azidi kufanikiwa zaidi kimpira na kimaisha kwa maslahi yake, familia na taifa.

Lakini nina swali kidogo kwa wenye kuijua TP Mazembe, labda mimi naipa ukubwa usioistahili (na exaggerate), Hivi kwa ukubwa wa timu ile, ni kweli wanasajili wachezaji aina ya Ambokile toka nchi nyingine ? Au wako desperate.... mimi nilikua nawaza kwamba TP wanatakiwa kuchukua wachezaji ambao ni the finest katika nchi husika hasa kutoka nchi kama Tanzania.
Ambokile ni mzuri sawa lakini mimi naona TP ni kubwa mno kwake. Kwa mfano, kwenye kikosi cha timu ya taifa cha wachezaji wa ndani Ambokile asipoitwa hakuna anayeweza kushangaa.
TP wamemchukua kwa madhumuni yapi, kwamba Congo mtu wa uwezo sawa na Ambokile hakuna ?

My take:
Nadhani timu zote za Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara wana tatizo linalofanana kwenye suala la recruitment ya wachezaji wa nje, nadhani Scouting sio nzuri sana.

Sijui wenzangu mna maoni gani ?
Eliud Ambokile ni mchezaji mzuri sana tena ana umri mdogo na ndicho tim kubwa huangalia.
Unaposema ulidhan wanasajili mchezaj ambaye ni the finest ktk nchi basi pasipo kujua ulikuwa unamtaja Eliud Ambokile. Huyu ni mshambuliaji aliyecheza round ya kwanza tu ktk ligi tena kutoka tim ya kawaida Lakini alifunga goal 10.

Utamfananisha Ambokile na straika gan mzawa aliyecheza bongo msimu uliopit? Ambokile angecheza round zote mbili angeweza kufunga hata goal 18 au 20 kabisa. Utamfananisha na nani huyu?

Bila kupata changamoto kule south Africa bila shaka Ambokile angekuwepo na stars AFCON.
 
Back
Top Bottom