Kwanza nimtakie kila la heri kijana wa nyumbani Tanzania kwa kupata fursa ya kucheza mpira kwenye timu kubwa Kama TP Mazembe. Akakaze azidi kufanikiwa zaidi kimpira na kimaisha kwa maslahi yake, familia na taifa.
Lakini nina swali kidogo kwa wenye kuijua TP Mazembe, labda mimi naipa ukubwa usioistahili (na exaggerate), Hivi kwa ukubwa wa timu ile, ni kweli wanasajili wachezaji aina ya Ambokile toka nchi nyingine ? Au wako desperate.... mimi nilikua nawaza kwamba TP wanatakiwa kuchukua wachezaji ambao ni the finest katika nchi husika hasa kutoka nchi kama Tanzania.
Ambokile ni mzuri sawa lakini mimi naona TP ni kubwa mno kwake. Kwa mfano, kwenye kikosi cha timu ya taifa cha wachezaji wa ndani Ambokile asipoitwa hakuna anayeweza kushangaa.
TP wamemchukua kwa madhumuni yapi, kwamba Congo mtu wa uwezo sawa na Ambokile hakuna ?
My take:
Nadhani timu zote za Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara wana tatizo linalofanana kwenye suala la recruitment ya wachezaji wa nje, nadhani Scouting sio nzuri sana.
Sijui wenzangu mna maoni gani ?