TPA elezeni ukweli juu ya mapungufu yenu na mkwamo wa serikali kuboresha mitambo na ufanisi wa bandari ya dar es salaam bila kuuma maneno

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
240
Reaction score
267
Nimeleta uzi huuu baada ya ile hotuba ya Rais Samia Alipokuwa akipokea Riport ya CAG na TAKUKURU..na Taarifa ya Tarehe 1/4/2022 iliyotolewa kwa wafanyakazi Wa TICS kuvunja rekodi kwa mwezi huu wa 3/2022

"Kwa siku Thelathini na moja zilizopita (31 ) kuanzia tarehe 1 - 31 Machi 2022, Kontena 61 ,236 ziillzoshughulikiwa kwa meli zllizoondoka mwezl Machi ndiyo idadi kubwa zaidi iliyowahi kushughulikiwa na meli kukamilika tangu kuanzishwa TICTS mwaka 2000.
Kwa kufikia malengo ya bajeti yaliyowekwa ya ubebaji wa kontena na NMPH kwa mwezi wa Machi 2022, kwa kuvunja rekodi ya kontena 61,236 TEU's , ambayo ni mara ya kwanza kubeba zaidi ya kontena 60,000 kumaliza TEU’s,ambayo ni hatua muhimu inayopaswa kusherebekewa.

Taarifa hii inaendelea na kunitafakarisha juu ya kile kinachohubiliwa na viongozi wetu, Nimesikia Sauti ya Edward John Urio Rais wa Chama cha Maforodha Tanzania akihojiwa EFM Radio,Ndani yake ameonyesha kwamba Rais kapotoshwa na ukweli halisi juu ya Bandari na kile alichokisema meli kukaa siku 2 TPA na siku 28 TICS,Urio ameenda mbali na kusema kuwa Kwa miaka mingi TICS inachangia kwa 85.5% ya Mapato yote ya Bandari,Na ni nini kinashushwa TPA na TICS na Kwa nini Wateja wanakimbilia TICS na si TPA

Tatizo la TPA na Serikali linaanzia hapa Tarehe 24 July 2021Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari na kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mizigo yote inayopitia bandarini inapakuliwa katika kipindi cha muda mfupi. ili kuvutia idadi kubwa ya watumiaji zikiwemo nchi za ukanda wa Maziwa Makuu. Ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho, Mkurugenzi wa Bandari, TASAC, TBS, TMDA, Kamishna wa Forodha pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya usafirisha

Ni kwamba hata baada ya kukamilika kwa Berth 5-7 za Mita 563 na Kina cha Mita 14 Makosa makubwa yalifanywa bila kufanya manunuzi ya vifaa vyenye thamani ya Dola mil 25.7 kwa maana nyingine hadi leo Upande wa TPA hauna vifaa vya Ushushaji mizigo hakuna uhakika wa mfumo wa Umeme wa kuendeshea QC Quay Cranes mpya acha mifumo ya kisasa ukusanyaji Data na upangaji mizigo.TPA semeni Ukweli juu ya kushindwa kufanya Intergration na Berths nyingine na kutokamilika kwa SGR bandarini,Hali hii na mnajua wateja wengi wanaweka foleni hata kwa siku 28 alizosema Rais kusubili mizigo yao ipakuliwe kwa usalama na TICS.

Mwambieni Rais Ukweli kuwa kwa mwaka 2021 handling Capacity yenu (TEU) ni 15.5% yaani 118,000 tu ukilinganisha na makadilio ya 400,000 ikiwa ni tofauti na TICS 85.5% ya makadilio ya TEU 660,000 kwa mwaka na wamefikia 642,000.

Haya ni mapungufu ya mitambo ambayo ujio wake labda mid mwakani

Mwambieni Ukweli Rais wa Nchi atatue tatizo kubwa lililopo TPA la mifumo Duni ya kielektronik na wataalamu,
Maswali haya yajibiwe mara moja Kwanini Waziri hajakutana na Wadau hadi leo? kwa nini kama TICS ni wazalishaji wa Pato la Bandari kwa 80% na wamewekeza pakubwa Berth 8-11 hawajakutana na Rais Kama wawekezaji wakubwa bandarini na kuweka mikakati ya pamoja na mkwamo wa serikali? kwa nini tuna tafuta mchawi wa matokeo makubwa ya Bandar wakati mchawi ni serikali yenyewe?
Kaka Erick Hamisi vunja nazi juu yakichwa cha mtu.. na iambie ukweli Mamlaka juu ya uzembe wa maamuzi ya manunuzi

Siwatetei TICS lakini kila mmoja wetu anajua Uwezo ulioundwa wa kushughulikia wa Berths 8 hadi11 ulikuwa 400k TEU kwa mwaka, lakini Uwekezaji unaoendelea wa TICTS katika teknolojia na vifaa hivi umeongeza uwezo wa kushughulikia hadi 700k TEU kwa mwaka..Serikali yetu hadi Leo imechelewa kuagiza QC labda hadi 2023 Daa inasikitisha.

TUNAKWAMA WAPI
Kwa mujibu wa Central Corridor Transport Observatory Report (CCTOR), Wasafirishaji wa mizigo wanaotumia bandari ya Dar es salaam wanatumia fedha kidogo zaidi kuliko bandari nyingine yoyote. Mfano, Msafirishaji anayetumia Bandari ya Dar es Salaam ataepuka gharama ya dola za kimarekani 1.18 kwa kila kilometa kwa kontena la mizigo ambalo angesafirisha kupitia bandari nyingine kama vile Bandari ya mombasa.

Ubora wa miundombinu Nchini Tanzania ni kichocheo kikubwa cha urahisi na gharama nafuu ya usafirishaji wa mizigo kutumia bandari ya Dar es salaam, Serikali imewekeza zaidi ya dola milioni 60 kwaajili ya kuboresha bandari hii ambayo kwa sasa ndio lango kuu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani kwanini tulisuasua kufanya manunuzi kabla uboreshwaji haujafika hata 60% ?

Wastani wa gharama ya kusafirisha mzigo kwa kilomita moja kwa kotena moja kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigali nchini Rwanda ni Dola za Kimarekaani 1.9 wakati mzigo huo utatumia Dola za Kimarekani 2.1 kwa kutumia bandari ya Mombasa.Hii ni fulsa pana na inapaswa kuchangamkiwa kwa nguvu zote

MH RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, WAITE WADAU WOTE HAWA MEZA MOJA, UTAPATA SULUHISHO LENYE MAFANIKIO MAKUBWA MNOOO YA BANDARI HII YA DAR ES SALAAM,UKIWEZA ANZA NA HAWA HUTCHISONPORTS WENYE UBIA NA TICS.

Katika hili LAZIMA NISEME, TPA MNAZINGUA PAKUBWA.
 
Unatwanga maji kwenye kinu wewe, serikali iko mikonon mwa wapigaji, sasa wanafanya figisu ili TICS aondolewe apewe kandarasi mtu mwingine na ikiwezekana bandari pia ibinafsishwe kwa hyo kampuni , safari za dubai hazikuwa za bure mkuuu…. Tukae kwa kutulia tu nchi imerud kwaoo..
 
Mmmmh
 
Moja ya vitu vilivyowekwa duniani ili kuongeza ufanisi huwa ni outsourcing, outsourcing kwa maana ya kugawa kazi kwa contractor na kumpa pressure kufikisha target unazozitaka..

Mashirika mengi yameonyesha kutushinda kuyaendesha watanzania kama watanzania ni vyema sasa tukaangalia namna ya kuoutsource hizi biashara na kuwapa wenye uwezo na sisi kuweka target tu ili kila mwaka tukusanye mapato yetu na watu waajiriwe ili wasukumwe kama punda kufikia target...

Bandari inapaswa kupewa mtu kama contractor maana sisi imetushinda kabisa, yatafutwe makampuni makubwa yenye uzoefu wa kurun port business kama MAERSK na MSC wapewe hilo libandari sisi tukae pembeni tuangalie show inavyopigwa....ikiwezekana wapewe bandari zote kuanzia Dar, Tanga na Mtwara... Sisi tubaki watazamaji na kupewa mapato yetu.. tuachana na vikampuni uchwara vya kizushi zushi vya wahindi/waarabu na madalali wao wapewe hiyo kazi giants MAERSK au MSC...

Kwa asili Watanzania ni wavivu, wajinga na wezi, hii tabia haiwezi kuisha ukiwapa mashirika makubwa kama haya wakae wenyewe baadala yake wawe waajiriwa tu chini ya management za mabeberu ndio watafanya kazi na kuzibiwa mianya otherwise ni ufala tu kila siku...suluhu pekee ni kuoutsource kila mahala tunapoona panashida na waliokuwa mameneja wote piga chini wengine wabaki waajiriwa wa Contractor halafu uone kama wataleta huo ujinga..

Mtanzania analaumu Kiongozi mkubwa kama waziri kwa wizi wakati mwenyewe ni mhasibu yuko TPA naye ni mwiz, au yuko pale kwenye pantoni feri kila siku anaiba mafuta, au ni gate man pale bandari kila siku anapiga dili kuruhusu dili au ni cleane pale TPA kila siku anatoka na jack za magari...Mtanzania huyuhuyu anayelaumu akina Kinana, Makamba na JK naye ni muajiriwa huko kwenye kampuni binafsi pia ni mwizi, mtoro kazini, mfitini, mnafiki, mchawi nk..

NJIA PEKEE YA KUINUSURU TPA NA KUIFANYA IWE PRODUCTIVE NI KUIBINAFSISHA KWA MAKAMPUNI BINAFSI MAKUBWA KAMA MAERSK AU MSC, NA IKIWEZEKANA HAYO MAKAMPUNI YAAJIRI UPYA NA WALIOPO WOTE WAFUKUZWE, SERIKALI ISET MFUMO WA KODI UTAKAOKUWA CONTROLLED NA VYOMBO VYA USALAMA NDANI YA TRA AMBAVYO VITAREPORT IKULU MOJA KWA MOJA..
 
Moja ya vitu vilivyowekwa duniani ili kuongeza ufanisi huwa ni outsourcing, outsourcing kwa maana ya kugawa kazi kwa contractor na kumpa pressure kufikisha target unazozitaka....
Umesema mashirika mengi yametushinda kuendesha hivyo Ni kuyabinafsisha ili yaendeshwe vizuri tuchukue mapato.

Tulifanya hivyo kwenye mashirika mengi, hebu tuambie ni lipi tulilofanikiwa baada ya kubinafsisha?
 
Tulishaanza kuwa kwenye right direction. Kudeal na maluhani wa kitanzania ni kuwaongoza kama vile uko gereza la vichaa. Uafrica ni gharama kubwa. Leo kiongozi unaruhusu watu wale na kauli za and I am serious about that eeee utegemee matokeo bora toka kwa maluhani weusi ????
 
Umesema mashirika mengi yametushinda kuendesha hivyo Ni kuyabinafsisha ili yaendeshwe vizuri tuchukue mapato.
Tulifanya hivyo kwenye mashirika mengi, hebu tuambie ni lipi tulilofanikiwa baada ya kubinafsisha?

inategemea unabinafsishaje, kama ubabinafsisha kwa kuwapa tu wahindi waendeshe wanavyotaka kama alivyofanta BWM lazima ile kwako..

Nazungumzia contracting au outsourcing, unatangaza contract ya kurun bandari na kuweka target zako unataka nini na taratibu zako kisheria kama kukutana na contractor wako kila quarter ya mwaka kumpima utendaji wake...

Huo ubinafsishaji unaousema ulikuwa sandakalawe amina, unampa mtu kiwanda bila target zaidi ya kusubiri kodi anayolipa based anachofanya...

Hapa tunazungumzia kuoutsource au contract kwa mtu ukiwa umempa targets za makusanyo unayataka na productivity unayotaka huku kodi zoote za serikali zikilipwa pia..
 
Kama Nchi tulianza kwenda vizuri, tatizo ni tumeanza kurudia matapishi sasa hapo usitaraji ustawi
 
Mkuu yapo yaliyofanywa sandakalawe na yapo yaliyokuwa outsourced kwa kuwapa watu target.
Achana na wakati wa BWM
Kipindi Cha JK tulifanya hivyo kwenye mashirika mfano mojawapo ni ATCL, hebu tuambie nini kilitokea?
 
Mhhh hakuna kitu hapo. Mlibinafsisha relwe ikawashinda sembuse bandari. Hakuna kitu hapo
 
Kama Zuhura yunus au Mama mwenyewe anasoma hapa mchangiaji hapo juu ulifakiwa upewe zawadi na wakuite uwasaidie kuona mapungufu kwani uliyaongea ni ukweli halisi wa kinachoiangisha TPA.

TPA haina progressive maintanance ya maana kwa ukiritimba wa kupata pesa toka serikalini. Menejimenti ya TPA pia ina walakini sana katika kufikiria a way forward ni kununua mitambo na maintanance ya maana.

Huyu Urio ni mtu mnafiki sana wakati mwingine huwa anashindwa kusemea matatizo anasubiri ahojiwe na redioni au kwemye TV ndio anabainisha makosa. Kwenye vikao na waziri kwanini asitoe mapungufu yafanyiwe kazi.

Kuna shida kati ya menejiment ya TPA na serikali. Lazima wabadilike na lazima watumie gharama kuleta mitambo mipya ya kupakia kupakua na kusafirisha mizigo.

Ingekuwa tuna akili nzuri menejiment ya TPA ilibidi waletwe hata foreigners kuondoa ukiritimba
 
Mkuu yapo yaliyofanywa sandakalawe na yapo yaliyokuwa outsourced kwa kuwapa watu target.
Achana na wakati wa BWM
Kipindi Cha JK tulifanya hivyo kwenye mashirika mfano mojawapo ni ATCL, hebu tuambie nini kilitokea?

ATCL haikuwahi kupewa contractor, bali tulikodi ndege maana tulikuwa hatuna ndege...ile ndege tuliyokodi ilikuwa operated na wenyewe waliotukodisha...

Ninachozungumzia ni kuicontract ATCL kwa kampuni binafsi tukimpa ndege na kumuwekea target zetu lakini all operation anafanya yeye at the end anapaswa kumeet target zetu ambazo tumekubaliana kwenye contract...

Mfano hapo mtoa maada, amezungumzia TICS wanavyomeet target, Tics ni contractor tu hapo na anafanya kazi kwa big push maana anajua lazima ameet target na asipomeet target anaweza kunyang'anywa kazi na kupewa contractor mwingine..
 
Nimeamini maneno yako wajanja,wapigaji wameanza Rasmi mkakati wa kuleta wawekezaji wa Bandari,kwanza wanatumia mbinu za kuichafua bandari kwa kuandaa machapisho na makala katika vyombo vya habari vya kimataifa,unaambiwa genge hili linajukumu la kumwaminisha Rais na viongozi wa juu kwamba Bandari yetu inamatatizo makubwa ya ufanisi na sasa kunahitaji la mwekezaji... Wapigadili hawa wakiongozwa na maafisa wa TPSF tayari wamefanya mazungumzo na mashirika na matajiri wa Uarabuni kuichukua bandari ya Dar es Salaam

East Africa’s largest and Kenya’s Port of Mombasa is experiencing substantive transshipment business as more ships evade berthing delays and waiting at the neighboring Port of Dar es Salaam in Tanzania.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…