LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 240
- 267
Nimeleta uzi huuu baada ya ile hotuba ya Rais Samia Alipokuwa akipokea Riport ya CAG na TAKUKURU..na Taarifa ya Tarehe 1/4/2022 iliyotolewa kwa wafanyakazi Wa TICS kuvunja rekodi kwa mwezi huu wa 3/2022
"Kwa siku Thelathini na moja zilizopita (31 ) kuanzia tarehe 1 - 31 Machi 2022, Kontena 61 ,236 ziillzoshughulikiwa kwa meli zllizoondoka mwezl Machi ndiyo idadi kubwa zaidi iliyowahi kushughulikiwa na meli kukamilika tangu kuanzishwa TICTS mwaka 2000.
Kwa kufikia malengo ya bajeti yaliyowekwa ya ubebaji wa kontena na NMPH kwa mwezi wa Machi 2022, kwa kuvunja rekodi ya kontena 61,236 TEU's , ambayo ni mara ya kwanza kubeba zaidi ya kontena 60,000 kumaliza TEU’s,ambayo ni hatua muhimu inayopaswa kusherebekewa.
Taarifa hii inaendelea na kunitafakarisha juu ya kile kinachohubiliwa na viongozi wetu, Nimesikia Sauti ya Edward John Urio Rais wa Chama cha Maforodha Tanzania akihojiwa EFM Radio,Ndani yake ameonyesha kwamba Rais kapotoshwa na ukweli halisi juu ya Bandari na kile alichokisema meli kukaa siku 2 TPA na siku 28 TICS,Urio ameenda mbali na kusema kuwa Kwa miaka mingi TICS inachangia kwa 85.5% ya Mapato yote ya Bandari,Na ni nini kinashushwa TPA na TICS na Kwa nini Wateja wanakimbilia TICS na si TPA
Tatizo la TPA na Serikali linaanzia hapa Tarehe 24 July 2021Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari na kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mizigo yote inayopitia bandarini inapakuliwa katika kipindi cha muda mfupi. ili kuvutia idadi kubwa ya watumiaji zikiwemo nchi za ukanda wa Maziwa Makuu. Ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho, Mkurugenzi wa Bandari, TASAC, TBS, TMDA, Kamishna wa Forodha pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya usafirisha
Ni kwamba hata baada ya kukamilika kwa Berth 5-7 za Mita 563 na Kina cha Mita 14 Makosa makubwa yalifanywa bila kufanya manunuzi ya vifaa vyenye thamani ya Dola mil 25.7 kwa maana nyingine hadi leo Upande wa TPA hauna vifaa vya Ushushaji mizigo hakuna uhakika wa mfumo wa Umeme wa kuendeshea QC Quay Cranes mpya acha mifumo ya kisasa ukusanyaji Data na upangaji mizigo.TPA semeni Ukweli juu ya kushindwa kufanya Intergration na Berths nyingine na kutokamilika kwa SGR bandarini,Hali hii na mnajua wateja wengi wanaweka foleni hata kwa siku 28 alizosema Rais kusubili mizigo yao ipakuliwe kwa usalama na TICS.
Mwambieni Rais Ukweli kuwa kwa mwaka 2021 handling Capacity yenu (TEU) ni 15.5% yaani 118,000 tu ukilinganisha na makadilio ya 400,000 ikiwa ni tofauti na TICS 85.5% ya makadilio ya TEU 660,000 kwa mwaka na wamefikia 642,000.
Haya ni mapungufu ya mitambo ambayo ujio wake labda mid mwakani
Mwambieni Ukweli Rais wa Nchi atatue tatizo kubwa lililopo TPA la mifumo Duni ya kielektronik na wataalamu,
Maswali haya yajibiwe mara moja Kwanini Waziri hajakutana na Wadau hadi leo? kwa nini kama TICS ni wazalishaji wa Pato la Bandari kwa 80% na wamewekeza pakubwa Berth 8-11 hawajakutana na Rais Kama wawekezaji wakubwa bandarini na kuweka mikakati ya pamoja na mkwamo wa serikali? kwa nini tuna tafuta mchawi wa matokeo makubwa ya Bandar wakati mchawi ni serikali yenyewe?
Kaka Erick Hamisi vunja nazi juu yakichwa cha mtu.. na iambie ukweli Mamlaka juu ya uzembe wa maamuzi ya manunuzi
Siwatetei TICS lakini kila mmoja wetu anajua Uwezo ulioundwa wa kushughulikia wa Berths 8 hadi11 ulikuwa 400k TEU kwa mwaka, lakini Uwekezaji unaoendelea wa TICTS katika teknolojia na vifaa hivi umeongeza uwezo wa kushughulikia hadi 700k TEU kwa mwaka..Serikali yetu hadi Leo imechelewa kuagiza QC labda hadi 2023 Daa inasikitisha.
TUNAKWAMA WAPI
Kwa mujibu wa Central Corridor Transport Observatory Report (CCTOR), Wasafirishaji wa mizigo wanaotumia bandari ya Dar es salaam wanatumia fedha kidogo zaidi kuliko bandari nyingine yoyote. Mfano, Msafirishaji anayetumia Bandari ya Dar es Salaam ataepuka gharama ya dola za kimarekani 1.18 kwa kila kilometa kwa kontena la mizigo ambalo angesafirisha kupitia bandari nyingine kama vile Bandari ya mombasa.
Ubora wa miundombinu Nchini Tanzania ni kichocheo kikubwa cha urahisi na gharama nafuu ya usafirishaji wa mizigo kutumia bandari ya Dar es salaam, Serikali imewekeza zaidi ya dola milioni 60 kwaajili ya kuboresha bandari hii ambayo kwa sasa ndio lango kuu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani kwanini tulisuasua kufanya manunuzi kabla uboreshwaji haujafika hata 60% ?
Wastani wa gharama ya kusafirisha mzigo kwa kilomita moja kwa kotena moja kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigali nchini Rwanda ni Dola za Kimarekaani 1.9 wakati mzigo huo utatumia Dola za Kimarekani 2.1 kwa kutumia bandari ya Mombasa.Hii ni fulsa pana na inapaswa kuchangamkiwa kwa nguvu zote
MH RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, WAITE WADAU WOTE HAWA MEZA MOJA, UTAPATA SULUHISHO LENYE MAFANIKIO MAKUBWA MNOOO YA BANDARI HII YA DAR ES SALAAM,UKIWEZA ANZA NA HAWA HUTCHISONPORTS WENYE UBIA NA TICS.
Katika hili LAZIMA NISEME, TPA MNAZINGUA PAKUBWA.