Rais William S. Ruto arejesha huduma za bandari Mombasa
Hiyo ni baada ya baadhi ya huduma zilizokuwa vikitolewa pwani kupelekwa bara, Naivasha. Hali hiyo ilisababisha zogo kubwa baina ya serikali ya Uhuru Kenyatta na washika-dau (stakeholders) kama kampuni za clearing and forwarding, wananchi wa pwani waliokuwa wanafaidi mnyororo wa fedha kutokana na shughuli kuwepo pwani
13 September 2022
Rais William Ruto amesema ahadi yake ya kurejesha shughuli za utaratibu wa kutoa bidhaa katika bandari ya Mombasa.
Ruto amefichua kwamba atatoa maagizo zaidi kuhusu utendakazi wa bandari ya Mombasa ili kuwezesha urahisi wa kufanya biashara na kuinua uchumi wa Mombasa.
Uhamishaji wa shughuli za bandari hadi Bandari Kavu ya Naivasha ilikuwa ajenda kuu wakati wa kampeni.
"Mchana wa leo, nitakuwa nikitoa maagizo ya kuondoa bidhaa na majukumu mengine ya kiutendaji katika bandari ya Mombasa kama nilivyotoa ahadi kwa Wakenya. Hii itarejesha maelfu ya kazi katika jiji la Mombasa," alisema.