Pilot boat ni boti inayotumika kumpeleka pilot kwenye meli na iwe na uwezo wa kuhimili hali ya dhoruba nje ya eneo la bahari ili inapokuwa kwenye zoezi la kumpandisha pilot na kumshusha kuwe na usalama.
Pilot boat inatakiwa urefu kuanzia mita 10 mpaka 25 kadri ya uelewa wangu. Mita zaidi ya 25 inakuwa ni matumizi mabovu ya rasilimali.
Tug boat ni boti ambayo hutumika kusukuma meli kubwa (push,pull,tow) inapo ingia bandarini na kupaki kwenye gari kutokana na meli kubwa kutokuwa na uwezo wa kugeuka haraka au kupaki (Manoeuvre). Tug boat lazima iwe na uwezo mkubwa wa manoeuvre,injini yenye nguvu hapa unakutana na 600Hp mpaka 20,000Hp.Tug boat inauwezo wa kuvuta meli iliyokwama au kuvuta barges (Teshali) za mizigo.
Pia tug boat inaweza kutumika kama Pilot boat endapo kuna dharura.Ila Pilot boat haiwezi kufanya kamwe kazi ya tug boat.
Tofauti kuu ya pilot na tug ni kuanzia matumizi mpaka kwenye nguvu.
Sorry kwa kujibu kwa kiswahili.