TPA yapeana tender nyingine kwa SECO Engineering ya Kenya

TPA yapeana tender nyingine kwa SECO Engineering ya Kenya

Pilot boat ni boti inayotumika kumpeleka pilot kwenye meli na iwe na uwezo wa kuhimili hali ya dhoruba nje ya eneo la bahari ili inapokuwa kwenye zoezi la kumpandisha pilot na kumshusha kuwe na usalama.

Pilot boat inatakiwa urefu kuanzia mita 10 mpaka 25 kadri ya uelewa wangu. Mita zaidi ya 25 inakuwa ni matumizi mabovu ya rasilimali.

Tug boat ni boti ambayo hutumika kusukuma meli kubwa (push,pull,tow) inapo ingia bandarini na kupaki kwenye gari kutokana na meli kubwa kutokuwa na uwezo wa kugeuka haraka au kupaki (Manoeuvre). Tug boat lazima iwe na uwezo mkubwa wa manoeuvre,injini yenye nguvu hapa unakutana na 600Hp mpaka 20,000Hp.Tug boat inauwezo wa kuvuta meli iliyokwama au kuvuta barges (Teshali) za mizigo.
Pia tug boat inaweza kutumika kama Pilot boat endapo kuna dharura.Ila Pilot boat haiwezi kufanya kamwe kazi ya tug boat.

Tofauti kuu ya pilot na tug ni kuanzia matumizi mpaka kwenye nguvu.

Sorry kwa kujibu kwa kiswahili.

Asante mkuu
Kwanini Baharia yaani Captain asitumie helikopta anapotaka kuabiri meli kuu?
 
Asante mkuu
Kwanini Baharia yaani Captain asitumie helikopta anapotaka kuabiri meli kuu?
Pilot lazima atumie pilot boat.

Pilot ni Captain aliye ajiriwa na bandari ambaye ana uzoefu wa muda mrefu kufanya kazi katika meli.Pia analijua vyema eneo la bandari,maboya yaliyopo na maeneo yote ya kuchukua tahadhari.

Pilot akipanda kwenye meli kazi yake ni kutoa maelekezo ya sehemu sahihi za kupita wakati wa kuingia na kutoka bandarini.

Kumpeleka Captain na helicopter melini itakuwa jambo gumu na gharama.

Ugumu unakuja meli inayopokea Helicopter lazima iwe na sehemu maalumu ya helicopter landing na si kila meli inayo. Helicopter ikitaka tua katika meli lazima iandaliwe team kwa ajili ya usaidizi.

Gharama za kuhudumia helicopter kumpakia pilot ni kubwa kwa ajili ya kumtoa na kumrudisha pilot.
 
Kuna shida gani kampuni ya kenya ikipata tender moja miongoni ya ma-tender mengi sana tanzania ya kujenga meli? Watu wawache ufala, makandarasi wa tanzania wamejenga meli an boti nyingi tangu uhuru na bado wata peana kandarasi kwa wazawa na kwa nchi zingine pia
Kama gani nyingine ispokuwa Big brother Kenya?
 
Mbona Wachina wanajengea barabara wakati nyinyi ni nchi ya wiwanda?

Isikuumize akili, taratibu Wakenya wanazidi kurithi utaalam wote na hivi karibu ndio watakua wnaitwa kufanikisha haya mambo ukanda wote huu, hebu angalia kwa ilivyo geothermal, wataalam wetu wanaitwa kote kote.
 
hongera zetu mazeee....waswahili maneno mengiiii ila utekelezaji zeroooo kabisaa....😂 wajengewe tu .maana hawajiwezii
 
Isikuumize akili, taratibu Wakenya wanazidi kurithi utaalam wote na hivi karibu ndio watakua wnaitwa kufanikisha haya mambo ukanda wote huu, hebu angalia kwa ilivyo geothermal, wataalam wetu wanaitwa kote kote.
Yaani hizo boti tu ndo mnazipigia kelele. Hamuoni madude tunayojenga huku?
 
Back
Top Bottom