TPDC kushirikiana na Kampuni ya China kuwekeza kwenye Gas

TPDC kushirikiana na Kampuni ya China kuwekeza kwenye Gas

Haya na wanafunzi kutoka Sudan wamewanyonya nini mbona imekua kero?
Kuna uzi ulitembea kuhusu bongo zozo kujipenyeza Tz, sikuwahi ona udini mle ndani, lakini mtu akihoji kuhusu wasudani hamtaki waguswe.

Acheni upumbavu

Jadilini hoja na sio kuleta huruma za kijinga
 
China ni afadhali kidogo kwanza walitujengea reli ambayo mataifa yote ya Magharibi na mashirika yao yalikataa
China ya akina Bruce Lee na akuna Bolo Yeung siyo China hii ya sasa. Hii ya hivi sasa ni maumivu tu. Sijui China hii imefanyiwa crossbreeding na India au sijui taifa gani hata sielewi!!? Lakini ambacho nina uhakika nacho ni kwamba, China hii siyo ile.
 
Mfuko wa Uwekezaji wa China Africa Development Fund (CADFUND) umeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya Nishati kwa kushirikiana na Makampuni ya China na Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Beijing katika Mkutano wa Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba ambaye yupo ziarani nchini China na Mwenyekiti wa CADFUND Ndugu Song Lei. 

Mfuko wa CADFUND wenye mtaji wa Dola za Kimarekani Bilioni 15 ulianzishwa na Serikali ya China kwa madhumuni ya kuwekeza katika miradi uwekezaji barani Afrika ambapo nchini Tanzania mfuko huo umewekeza katika sekta ya kilimo (Uzalishaji wa Mkonge), sekta ya viwanda (uzalishaji wa Saruji) na sekta ya mawasiliano.

Aidha Kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) zimekubaliana kushirikiana katika uwekezaji katika sekta ya gesi nchini ambapo kampuni ya CNOOC imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine katika uwekezaji wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga.
 
Kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Shirika la TPDCTZ kushirikiana katika uwekezaji katika sekta ya gesi nchini.

Aidha, Kampuni ya CNOOC imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine katika uwekezaji wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Beijing wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nishati January Makamba na Mwenyekiti wa Kampuni ya CNOOC Ndugu WANG Dongjin uliofanyika leo jijini Beijing.
Ule wa trillion 70 umeshaafika wapi
 
Jamaa wanachuki binafsi na waarabu
Tuache kuangalia range na dini
Tuangalie concept
Unaongea nini bro. So hapo Djibouti nao walikuwa na chuki nao sio. Acheni kuonyesha upunguan wenu. Kwani shida iko wap mtu akikuambia rekebisha mkataba kwa maslah ya nchi
 
Back
Top Bottom