TPDF ilipozima jaribio la mapinduzi Seychelles

Mkuu Asante kwa kurejea jamvini. Nchi yetu ina historia kubwa mno lakini haiandikwi na mbaya zaidi mashujaa wenyewe wanapukutika.
Nilimtembelea kijana wamgu yuko huko kaniambia hakuna popote palipoandikwa kuwa wanajeshi wa JWTZ walihusika kuzuia jaribio hilo wakati sisi tulikuwa kwenye Operation hiyo tupo.Fikiria na sisi tukifa who will know this??? Tanzania kuna sehemu tumejisahau sana!!.
 
Mkuu tunakushukuru sana kwa huduma yako kwa Taifa. Hongera sana.
 
Historia nzuri Sana hii japo inasikitisha haikuandikwa.
 
Ndio uandike sasa
 
inawezekana huyu jamaa alishakufa!
 
#Echolima. Simulizi ya Operation Mahe imeshatoka?
#mshana jnr,#kalamu
 
Mozambique alienda kama kiongozi tena? Gen. Hassan Ngwilizi(Rip)

..Brigadier General Hassan Ngwilizi [ r.i.p] ndiyo aliongoza askari waliokwenda kusaidiana na majeshi ya Msumbiji na Zimbabwe kupambana na magaidi wa Renamo.

..askari hao walikwenda Msumbiji muda mfupi baada ya kifo cha Raisi Samora Machel baada ya hali ya usalama nchini humo kuwa mbaya.

..Operation aliyoongoza Brig.Gen.Ngwilizi ilipewa jina " Operation safisha. " Raisi Kikwete kabla hajastaafu alitoa nishani kwa askari walioshiriki operation hiyo.
 
Mkuu una vitabu umeandika khs hizo historia za operesheni ulizoshiriki ? Naomba uniambie vinapatikana wapi?

MTC | 101| [emoji769]
 
Hawa jamaa wakienda mbele za haki history itapotea maana hakuna maandishi
 
Hawa jamaa wakienda mbele za haki history itapotea maana hakuna maandishi

..Hassan Ngwilizi amefariki.

..Imran Kombe aliuawa.

..Muhidin Kimario amefariki.

..Ahmed Kitete alipata ajali akafariki.

..James Luhanga almetangulia.

..Rowland Makunda ametutoka.

..kweli HISTORIA inatutoka.

..na jambo lingine tunakosea kwamba hatuipi SIKUKUU YA MASHUJAA uzito inaostahili.
 

Haya mambo waliofanya, ingekuwa kwa wenzetu wangeandika na kutengeneza documentaries za kutosha. Kwanini hatuoni umuhimu wa kufanya hivyo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae?
 
Loo!!! post hii ndiyo nimeiona leo kweli hata mimi mwenyewe ninasikitika sana!!!Mambo ni mengi sana katika kutafuta rizki ya kila siku!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…