Habari za siku nyingi wakuu!! Nimepigiwa simu asubuhi hii ya leo na kutaarifiwa kuwa yule Mtemi wa Pointe La Rue keshatutoka katangulia mbele ya haki kwa kweli kifo hicho kimenistua sana ninaposema Pointe La Rue ni jina la uwanja wa ndege wa MAHE huko kwenye visiwa vya Seychells ambako usiku wa Nov,25,1981 wanajeshi wetu nikiwemo mwenyewe
Echolima tulitua kwenye uwanja mdogo wa mpira wa shule kwa kutumia ndege yetu DHC-5 Buffalo(Najua sasa hivi ndege hiyo imeshakuwa-Retired from military oprations)Kisa cha safari hiyo ilikuwa kusaidia jahazi lisizame baada ya Mamluki kutoka uliokuwa utawala wa kibaguzi wa afrika kusini kutaka kumuondoa madaraka Rais Rene wa visiwa vya Seychells,Operation hiyo haiwezi kukamilika bila kumtaka Mtemi wa Pointe La Rue Marehemu Brigadier.Hassan Ngwilizi Baada ya kuzima Jaribio hilo mimi na wezangu tulirejea nyumbani Dec,29,1981.
Ni kweli niliahidi kutoa historia yangu ya Operation hiyo lakini kutokana na mambo mbalimbali ya Ki-maisha sikuweza kufanya hivyo lakini kikubwa Namshukuru sana Mungu kwa kutuweka hai mpaka sasa hivi ili kuweza kuyasimlia haya yote kwangu binafsi ni bahati sana maana wengi wetu wamepoteza maisha kutokana na Post traumatic stress disorder (
PTSD) na tulio hai inabidi kumshukuru sana Mungu.Kuna msemo wa Kijeshi unasema Mwanajeshi hafi maana hata akifa Matendo yake yanaishi!!!Kwa maana hiyo Matendo na Operation alizozifanya Brigadier.Hassan Ngwilizi huko Msumbiji walipokuwa wanapambana na Renamo na baada huko kwenye Visiwa vya Seychells matendo hayo hayafutiki bali yanaishi hata leo!!!!.
Gamba la Nyoka
JokaKuu
Mdau
Nicholas J Clinton
majeshi 1981