TPDF ilipozima jaribio la mapinduzi Seychelles

Loo!!! post hii ndiyo nimeiona leo kweli hata mimi mwenyewe ninasikitika sana!!!Mambo ni mengi sana katika kutafuta rizki ya kila siku!!!
Haya sasa.

Ulikuwa unafukunua nini hadi ukafika huko wakati huu mkuu 'Echolina'!

Uzuri wa JF ndio huu. Hata uchelewe miaka mingapi, habari utaikuta tu, na ukitaka kuchangia kwa wakati wako unajimwaga tu.
 
Halikufanywa siri, bali labda watu hawakulifuatilia tu. Kuna mtanzania mmoja aliwahi kuwa mtawala wa Seychells kwa muda mfupi wakati wa mapinduzi yale na ilijulikana waziwazi tu. Ni kwa vile Seychells haikuwa high octane story ndiyo maana haikuvuma sana. Hata Nyerere aliwahi kukiri hadharani kabisa kuwa alipeleka jeshi kwenda kumsaidia msoshalisti mwenzake kule Sychells. Ni kutokana na opereshini ile ndiyo maana Seychells ilikuwa na maafisa waandimizi wengi kutoka Tanzania; kwa mfano mwanasheria mkuu wa Seychelles kwa muda mrefu alikuwa ni mtanzania.
 
Umekatisha story mkuu...unaweza kututajia hao watanzania japo kwa uchache??
 
Umekatisha story mkuu...unaweza kututajia hao watanzania japo kwa uchache??
Siwakumbuki majina yao ndugu yangu; ila kulikuwa na wapare/wachaga kadhaa waliokuwa na nafasi za juu sana serikalini. Nadhani Kanali Ngwilizi, kabla hajawa brigedia, alitawala Seychelles kwa siku moja
 
Mh,HISTORIA ni ya muhimu Sana ingawa Watanzania hatuoni umuhimu wa somo Hilo.
 
Watanzania hatupendi kuandika..inabaki historia ya kusimulia kwa mdomo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…