TPL: kutoka uwanja wa Taifa Yanga SC vs Mwadui FC

Hivi kwanini machi ya kumalizia Ligi kati ya Azam na Yanga imerukwa.
Na watakutana lini ?
Lengo langu ni kuuona huu mpambano ambao nadhani utakuwa mzuri.
Maana kwakweli sasa hivi Yanga wanaupiga mpira mwingi sana na Azam pia.
Ni hamu ya kuwaona wakikipiga pale kwa Mchina.
Sisi Simba tuko kimataifa kwanza.
Tunakuombeni nyote mtuombee tufike fainali na kunyakua Kombe la Club Bingwa wa Africa.
Kwa faida yetu na yenu na taifa kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ratiba imewasaidia Azam maana wametoka kucheza juzi wana uchovu tungewafunga vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamati ya masaa 72 ya TFF imepanga kuwaita wachezaji wa Yanga na kuwahoji iwapo ni kweli timu hiyo ina njaa au wanakula kwa siri. Hatua hiyo ni baada ya wachezaji wa Yanga kufunga magoli kwa umbali wa zaidi ya mita 40 yakiwa na mwendo kasi wa 160KM/HR. Magoli yaliyoiponza Yanga mpaka kufikishwa kwenye kamati hiyo ni magoli ya Ibrahim Ajib na lile la Faisal Salum kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Mwadui Fc. Na pia kamati hiyo ya masaa 72 inatafakari goli la tambwe baada ya kuruka juu na kukaa kama dk moja na kupiga kichwa kilisababisha kipa wa mwadui kutaka kuvunjika nyonga na kuacha mpira uende nyavuni🤣🤣🤣🤣🤣
Ha haaaa.....nimechekaje?
 
Ahsante Mwl Kashasha. 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom