TPL: Simba SC vs Yanga SC - Sept 30, 2018 (FT: 0-0)

TPL: Simba SC vs Yanga SC - Sept 30, 2018 (FT: 0-0)

Kumbuka mpaka sasa Mnyama mkali kafungwa vigoli 2 tu, pamoja na kucheza mechi kibaoooo.. Moja kati ya hayo magoli tulifungwa na Mbao kwa nguvu ya sayansi ya kiafrika.
Kwa ile beki yenu iliyooza lazima MK14 awageuze geuze anavyotaka.. Hapo bado kuna CR7 toka Uganda.. Kuna Kichuya.. Kuna Mo.. Kuna Super Sub Salamba.. n.k
Kwa kifupi leo pona yenu msiingize timu uwanjani.. Kama mnabisha, ingizeni timu uwanjani muone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umezungumzia mbao eeeh?.
Ok safi sana kama unawakumbuka mengine ya sayansi ya kiafrika hayanihusu japo yananifanya nimkumbuke aliyewaita mbumbumbu
 
Uimara wa safu za ulinzi mpaka sasa
1. Simba SC kafungwa vigoli viwili tu
2. Yanga SC kafungwa magoli manne

Ikumbukwe mpaka sasa Simba SC kacheza mechi nyingi ukilinganisha na Ndala.
Impacts ya vigoli viwili tu na magoli manne kwenye msimamo upoje?nmependa ulivyotumia ngeli ya KI-VI (vigoli viwili),unazi tabu kweli kweli
 
Umezungumzia mbao eeeh?.
Ok safi sana kama unawakumbuka mengine ya sayansi ya kiafrika hayanihusu japo yananifanya nimkumbuke aliyewaita mbumbumbu
Nipo Taifa Stadium hapa.. Kuna shabiki wa Simba anapiga dua hapa..

"Yalaa Mungu atunusuru, kipigo tutakachowapa Vyura si cha kibinadamu kabisa, Mungu tunusuru"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Impacts ya vigoli viwili tu na magoli manne kwenye msimamo upoje?nmependa ulivyotumia ngeli ya KI-VI (vigoli viwili),unazi tabu kweli kweli
Impact yake iko hivi;
1. Ndala mna ukuta mbovu saana, ambao MK14, Okwi, Kichuya, Salamba n.k kila mmoja ataondoka na goli zaidi ya 1
2. Ukuta wa Mnyama unaweza kuufananisha na ule wa Berlin.. haupitiki kabisa.. Kwa kifupi Ajibu, Mama Kambo hawana uwezo wa kuvunja mnyororo unaoenda kutengenezwa na.. Kapombe, Nyoni, Wawa na Tshabalala
3. Kuhusu msimamo, tunaenda kuwashusha leo.. Na si tunawashusha tu, bali hili zoezi litaambatana na kipigo kizito tutakachowashushia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kila mtu anajiongelea la kwake lolote kuhusu mechi ya leo, tusubiri mechi ikiisha ili tupime kwa kila mtu kama kilicho kuwa kinasemwa kabla ya mechi ni pumba au mchele,?
 
Matokeo ya Msimu uliopita.. Hizi timu zilipokutana

28/10/2017: Yanga SC 1-1 Simba SC

29/04/2018: Simba SC 1-0 Yanga SC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahaaaa et simba ushindi yan mbao washamvunja miguu sisi twaenda malizia kata kichwa tuu mana awezitembea now nackia et
 
Haya ni baadhi ya magazeti 01/10/2018 baada ya mechi ya Leo.

Championi
KAGERE HASHIKIKI
- Awapangua mabeki wa yanga Kama anachambua mchele..
-Zahera amsifia, atapa kulipa kisasi February..
Mashabiki WA yanga wazimia, walazwa muhimbili na temeke.

Mwanaspoti
SIMBA GARI IMEWAKA
- Yaichakaza yanga 3:1
- Yanga watafuta mpira kwa tochi
- Kagere awa gumzo

Nipashe
TENI AGOMEA WAANDISHI WA HABARI
- Ni kufuatia kipigo cha Jana.
- Mzee Akili Mali aujia juu uongozi wa yanga.

Majira
KAGEREEEEEEEEEEE
- Avunja rekodi ya kibaden
- Apiga hat trick, yanga walia na mwamuzi.

Uhuru
SIMBA RAHA SANA
- Yacheza mpira wa majuu
- KAGERE awindwa na timu za ulaya
- Magoli yake si ya nchi hii.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uimara wa safu za ulinzi mpaka sasa
1. Simba SC kafungwa vigoli viwili tu
2. Yanga SC kafungwa magoli manne

Ikumbukwe mpaka sasa Simba SC kacheza mechi nyingi ukilinganisha na Ndala.
Tena vigoli vyenyewe kamoja kapenati hapo ndio ujue safu yetu ya ulinzi ilivyo imara
 
Uimara wa safu za ulinzi mpaka sasa
1. Simba SC kafungwa vigoli viwili tu
2. Yanga SC kafungwa magoli manne

Ikumbukwe mpaka sasa Simba SC kacheza mechi nyingi ukilinganisha na Ndala.

Nimependa hayo maneno vigoli na magoli😀😀😀
 
Back
Top Bottom