TPLB yamfungia Kocha wa Yanga Nabi mechi 3 na faini laki 5 huku Simba SC, Azam FC, Coastal wakilimwa 1ml

TPLB yamfungia Kocha wa Yanga Nabi mechi 3 na faini laki 5 huku Simba SC, Azam FC, Coastal wakilimwa 1ml

Hawa wanalogea jezi
Hawa wanalogea siku ya tukio..
Tuchekana sasa [emoji23][emoji23][emoji23]
Mchezo ni kuwahiana tu.
Umeona eee hakuna vita hapa tupambane tupate walozi wazuri baaaasii 😀 😀 😀 😀 maana huyo mlozi wa Gadiel katulisha droo
 
Kocha wa Yanga Nabi Nasreddine amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba kwenye mchezo ambao Yanga walipigwa 2-1 dhidi ya Ihefu FC.

Kamati ya usimamizi wa Ligi Kuu TPLB imeitoza Klabu ya Simba Shilingi 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la baadhi ya wachezaji wake kuingia uwanjani kwa kupitia milango isiyokuwa rasmi kwenye mchezo ambao Simba SC walitoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Mbeya City.

Mchezaji Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kulazimisha kuingia uwanjani saa 4: 25 asubuhi kwa kile alichoeleza alitaka kukagua Uwanja kuelekea mchezo wa Mbeya City dhidi Simba SC.

View attachment 2433526View attachment 2433527View attachment 2433528
20221202_210344.jpg
 
Hivi huwa wanazipeleka wapi hizi hela? Yaani matumizi yake yakoje, baada ya kulipwa?
We unadhan lile tumbo la karia linatoka wapi, pesa ndio hiz, hapo kuna zaid ya milion 5 na bado kila siku makosa ni yale yale, kupita mlango wa nyuma, ushirikina n.k
 
Kocha wa Yanga Nabi Nasreddine amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba kwenye mchezo ambao Yanga walipigwa 2-1 dhidi ya Ihefu FC.

Kamati ya usimamizi wa Ligi Kuu TPLB imeitoza Klabu ya Simba Shilingi 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la baadhi ya wachezaji wake kuingia uwanjani kwa kupitia milango isiyokuwa rasmi kwenye mchezo ambao Simba SC walitoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Mbeya City.

Mchezaji Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kulazimisha kuingia uwanjani saa 4: 25 asubuhi kwa kile alichoeleza alitaka kukagua Uwanja kuelekea mchezo wa Mbeya City dhidi Simba SC.

View attachment 2433526View attachment 2433527View attachment 2433528
Hivi Simba huu upumbavu mnaodanganyana mara kuingia lango lisilo rasmi, mara kuwanga usiku, mara kuwasha moto uwanjani....halafu unaambulia Sare sare maua!..... huwa hamjifunzi? .... mnajidanganya sana aisee! nasimitika sana huu upmbavu haifai!
 
Aibu sana kwa Yanga na Simba kuendekeza haya mambo ya kishirikina, kwangu mimi sina simile kabisa na ushirikina wote wanaoendekeza mambo haya ni wapumbavu kabisa
Nadhani kukomesha haya ni adhabu kuwa maradufu ya hii, si kutegemea kupigwa faini tu ambapo Klabu au mchezaji ana uwezo wa kulipa.

Adhabu iongezwe kuhusu mambo haya.
 
Nadhani kukomesha haya ni adhabu kuwa maradufu ya hii, si kutegemea kupigwa faini tu ambapo Klabu au mchezaji ana uwezo wa kulipa.

Adhabu iongezwe kuhusu mambo haya.
Adhabu ikiwa kukatwa point hakuna mtu atafanya huu upuuzi kwani wanafanya hivyo kwa imani potofu kuwa watapata ushindi na kujiongezea point sasa adhabu ikiwa kukatwa point watakoma kabisa haya maujinga yao.
 
Hizi faini kwa mkupuo namna hii haijawahi kutokea, haya sasa ndo mavuno kwa TFF.

1. Kocha Nabi laki tano.
2. Gadiel Michael laki tano.
3. Simba SC, milioni moja.
4. Azam FC milioni moja.
5. Coastal Union milioni moja.
6. Ruvu Shooting laki tano.
7. Mbeya City laki tano.
8. Mchezaji wa Coastal laki tano.
Azam kafanya nini?
 
Azam kafanya nini?
Kwasababu ya shabiki wa Azam FC aliyekuwa amekaa jukwaa maalumu kurusha chupa ya maji baada ya Coastal Union kusawazisha bao la pili kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union
 
Back
Top Bottom