TRA, E-filing System inarudisha nyuma kasi ya uchumi wa Biashara

TRA, E-filing System inarudisha nyuma kasi ya uchumi wa Biashara

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
2,348
Reaction score
3,038
Straight to the point, mfumo wa taarifa za marejesho (e-filing System) unarudisha nyuma kasi ya maendeleo ya uchumi na kuikosesha serekali mapato kwa wakati.

Mfumo huo umezidiwa nguvu na umekua kero kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya uchumi wa biashara hasa kwa wafanyabiashara wadogo

Inamlazimu mtu kuacha shughuli zote kwa siku kadhaa kwa ajili ya kufaili return moja ambayo ilapaswa kufanywa kwa dakika 5, kwa sababu mfumo umekuwa sio rafiki na hauna nguvu ya kupokea marejesho kwa wakati

Lakini pia mfumo huo umekua sababu ya dhuluma kwa wafanyabiashara Kwa sababu ya adhabu ya ucheleweshaji wa marejesho licha ya kuwa makosa ni ya mfumo wenyewe na mamlaka imeshindwa kuboresha mpaka sasa

TRA chukueni hatua au mturudishe kwe utaratibu wa zamani huu wa sasa unauwa uchumi wa nchi Kwa sababu mambo hayaendi kwa wakati mnatutesa na mnatuonea pia.

Kibaya zaidi kila unapojaribu kuwasilisha tatizo la mfumo kwa maofisa wa TRA unajibiwa jaribu link nyengine katika link tatu zilizopo mwisho wa siku hakuna suluhisho lolote linalopatikana zaidi ya kupoteza muda tu na kupoteza mapato kwa sababu hizo link zote ni yaleyale

Ndg. Kamishna tafadhali chukua hatua mfumo wako unaua uchumi wa nchi.

Wafanyabiashara tupaze sauti tutaishia kuumia bila suluhisho haya ni maumuvu makali tuungane kuliongelea hili vinginevyo itakua mazoea
 
Kuturudisha nyuma hapana. Waboreshe. Najua inawezekana wanaangalia utunzaji wa mfumo kulinganisha na mapato wanayokusanya, lakini wasiwe bahili sana. Hayo ndo maendeleo.
 
adapt to the prblems find a solution. for me huwa nafile kabla ya tar 5 ikiwa sambamba na statutory zote za mwezo uliopita sababu pia lazima nisubmiy MIS Kabla ya date 10. why wait till near deadline to file?
Sasa wote wakirudi tarehe 5 tatizo litakuwa halijatatuliwa. Mfumo unatakiwa uhimili idadi. Umesema mwisho tarehe 7 basi hata watu wakileta tarehe 7 mfumo uwe rafiki.

Kazi ni nyingi, mhasibu hawezi kuacha kazi za reconcilliation tarehe za mwanzo wa mwezi akaanza kupambana na efilling ambayo ina siku 15 mbele. By the way, inaanza reconcilliation ndo filling ifuate.
 
Sometimes nahisi labda huo mfumo wanafanya makusudi usiwe unafanya kazi,ili tushindwe kufanya filing watupige hela.

Huduma mbovu mbovu sana.,yani unatamani hata kufunga biashara aise.
 
Adapt to the prblems find a solution. for me huwa nafile kabla ya tar 5 ikiwa sambamba na statutory zote za mwezo uliopita sababu pia lazima nisubmiy MIS Kabla ya date 10. Why wait till near deadline to file?
Nafikiri hilo sio lengo la mfumo, kufuatilisha mapungufu yake yaani shughuli za kila siku ziakisi mfumo kutokana na mapungufu yake hilo sio lengo na huo uzebe.

Kumbuka shughuli za utendaji wa kila siku kibiashara zinaweza tu kufuata mapungufu ya maumbile ya binadamu Kwa sababu kaumbwa na Mungu, lakini sio kufuata mapungufu ya mfumo uliotengenezwa na binadamu huo utakua ni ufala.

Yanatakiwa yafanyike maboresho ya makusudi kuendana na Kasi ya Biashara na sio Kasi ya Biashara iufutushe mfumo mbovu hatutokwenda mbele tutachekwa na nia aibu kutuma return kwa kuvizia eti uendane na Hali haitakiwi kuwa hivyo Bro
 
Sometimes nahisi labda huo mfumo wanafanya makusudi usiwe unafanya kazi,ili tushindwe kufanya filing watupige hela.

Huduma mbovu mbovu sana.,yani unatamani hata kufunga biashara aise.
Inawezekana kabisa au labda kuna hujuma mbadala kisiasa au kiuchumi mamlaka zinatakiwa ziliangalie hilo
 
Adapt to the prblems find a solution. for me huwa nafile kabla ya tar 5 ikiwa sambamba na statutory zote za mwezo uliopita sababu pia lazima nisubmiy MIS Kabla ya date 10. Why wait till near deadline to file?

Huo mfumo ambao ukifika mwisho wa mwezi unakuwa mzito ni mfumo wa kijima. Watu tunagoogle na kupata taarifa zozote muda wowote wao wanakwama wapi? Kwanini wasihost hiyo mifumo yao kwenye server zilizofast huko duniani? Au hizo server za TRA zinasimamiwa na wazee waliostaafu, maana hao ndio hawana haraka.
 
Waswahili wanasema ukishangaa ya Mussa utastaajabu ya Firaunia, kumbuka hicho ni chombo chenye mamlaka ya kitaifa kusimamia mapato ya nchi

Ritani ya kufanya dakika 5 unahangaika nayo siku 5 tena hapo umeacha kila kitu unahangaikia hilo tu ukisema uingize mambo mengine basi ujue mwezi unakutana na kiporo cha ritani ya mwezi ulio pita
 
Wengi hawajui huu mfumo wa e-filing. Kweli ni changamoto sana. TRA wafanye mabadiliko haraka sana.
Hata wafanyabiashara wengi hawajui ni kiasi gani unaumiza muda Kwa sababu wameajiri watu lakini unakuta mtu anadedicate time kwenye jambo hilo tu na mengine ya lala inakera sana tena sana
 
Adapt to the prblems find a solution. for me huwa nafile kabla ya tar 5 ikiwa sambamba na statutory zote za mwezo uliopita sababu pia lazima nisubmiy MIS Kabla ya date 10. Why wait till near deadline to file?
Wengi wanafanya wakati wa deadline halafu mfumo ukizidiwa wanalalamika.
 
Wengi wanafanya wakati wa deadline halafu mfumo ukizidiwa wanalalamika.
Wewe si mfanyabiasha hujui usemalo.huu mfumo hakuna cha tarehe 5 wala tarehe 15 ni majanga matupu.tuna fill SDL,Paye & VAT kwa tarehe tofauti tofauti lkn bado utatumia muda mwingi sana ktk zoezi hilo.

Suala la muda wala halina maana kwasababu kodi nazo zina muda wake tofauti tofauti.tumeajiri watu si kwamba hatujui lkn lazima utumie muda mwingi sana na wakati mwingine unajikuta unapambana kulipa fine si kwasababu ya uzembe hapana bali huo mfumo wa karne ya 17.
 
Wengi wanafanya wakati wa deadline halafu mfumo ukizidiwa wanalalamika.
Kaka STROKE sio kila jambo lazima uchangie. Yale mambo usiyoyajua au usiyokuwa na uzoefu nayo au ambayo hayagusi au kuhusika na mapito ya maisha yako ya kila siku sio lazima uchangie unayaacha yapite tu

Vinginevyo ukilazimisha kuchangia utaonekana kama mwenda wazimu ni sawa na leo hii umlaumu dereva wa Ndege (Pilot) wa Precision Air iliyopata ajali Bukoba kuwa mwendo kasi ndio ulisababisha ajali

We jamaa sijawahi kukuelewa kabisa mara nyingi nahusisha hiyo Avatar yako na comment zako katika mada mbalimbali humu ndani, huwa vinafanana sana yani copy to right. Ahsante [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Wengi wanafanya wakati wa deadline halafu mfumo ukizidiwa wanalalamika.
Kwahiyo, huo mfumo unataka watu wafile kwa makundi? Tupigiane simu kuwa leo anzeni nyie kesho tutafile sie?
 
Wewe si mfanyabiasha hujui usemalo.huu mfumo hakuna cha tarehe 5 wala tarehe 15 ni majanga matupu.tuna fill SDL,Paye & VAT kwa tarehe tofauti tofauti lkn bado utatumia muda mwingi sana ktk zoezi hilo.

Suala la muda wala halina maana kwasababu kodi nazo zina muda wake tofauti tofauti.tumeajiri watu si kwamba hatujui lkn lazima utumie muda mwingi sana na wakati mwingine unajikuta unapambana kulipa fine si kwasababu ya uzembe hapana bali huo mfumo wa karne ya 17.
Watanzania wapo hivyo kufanya jambo siku ya deadline.

Mfumo unazidiwa wanashindwa.

Kila mara watu wanasubiria extension ya kufanya jambo.

Hii imeshazoeleka.
 
Kaka STROKE sio kila jambo lazima uchangie. Yale mambo usiyoyajua au usiyokuwa na uzoefu nayo au ambayo hayagusi au kuhusika na mapito ya maisha yako ya kila siku sio lazima uchangie unayaacha yapite tu

Vinginevyo ukilazimisha kuchangia utaonekana kama mwenda wazimu ni sawa na leo hii umlaumu dereva wa Ndege (Pilot) wa Precision Air iliyopata ajali Bukoba kuwa mwendo kasi ndio ulisababisha ajali

We jamaa sijawahi kukuelewa kabisa mara nyingi nahusisha hiyo Avatar yako na comment zako katika mada mbalimbali humu ndani, huwa vinafanana sana yani copy to right. Ahsante [emoji120][emoji120][emoji120]
Usinipangie cha kuandika mkuu.

Nitaandika navyojisikia katika mada yeyote bila kujali wewe au mtu mwingine yeyote ana mtazamo gani juu ya nilichoandika. So long as i believe nilicho andika.

Hiyo ndio kanuni yangu. Hutaki kunywa sumu.

Mjinga wewe.

Unaleta mada halafu unapangia watu nani achangie na nani asichangie.

This is a public forum and everyone is invited to air his/her comment at his/her disposal.

Kama vipi ungewapigia simu TRA.

Mpumbavu nanusu.

Na siku nyingine usiandike mada ya kijinga kama hii.
 
Back
Top Bottom