TRA fanyeni kazi yenu kwa ufanisi! Watu hawaombi risiti na wenye maduka hawatoi risiti kikamilifu!

Haya mambo aliyaweza Magufuli. Now enzi za jakaya zimerudi tuendelee kula bata. Si mlitaka maisha mepesi haya sasa yamerudi


Lakini ushauri wa bure ni bora wakalipa kodi stahiki kwa wakati na kufanya compliance zote kwa mujibu,
Wakiacha kufanya hivyo atakuja kiongozi Mkuu mwingine mwenye kaliba ya JPM akataka kuanzia nyuma yaani sasa na kuanza kufukua makaburi nakwambia kuna watu watapoteza maisha kabla ya wakati wao!

Hapo task forces zitakapoanzishwa heeee sipati picha .

Tulipe kodi bila shuruti kwa mujibu kwa maendeleo ya Taifa letu .

Nyakati kama hizi kuna wengine hawachukulii maanani swala la kulipa kodi na compliances kwa mujibu maaana si wameambiwa tra wasiwabughudhi ?!

Sawa lakini?!
 
Umeeleweka sana mkuu
 
Eh Mungu msamehe huyu mtu hajui alitendalo.
 
Hii ni changamoto sana na ni ngumu kuidhibiti kwakutumia sheria ama taratibu zinazoendelea kutumika sasa.

Hapa kuna anayehitaji Pesa na anayehitaji mahitaji, kama hawa wataelewana unadhani kuna atakayetamani kumshtaki mwenzake maadam hakuna anayeamini kadhurumiwa. Kumbuka mtaka pesa yuko radhi asikupe mzigo kama unataka risiti, chukulia umeshausafiria huo mzigo na gharama za hapa na pale je utauacha?

Tutauimba uzalendo mpaka verse zitaisha ila bila kumpa motisha huyu mzalendo mtamlaumu bure.


#NAPENDEKEZA :
TRA wawe wanafilisi mali papo hapo inapobainika haijatolewa risiti na Fain juu
Iwe kwa mteja ukiwa na ushahidi wa kuuziwa bidhaa bila risiti au risiti iliuyoandikwa bei pungufu na uliuoitoa, unawajulisha TRA wanafika Dukani, unarudishiwa hela yako na mzigo unaondoka nao, na muuzaji atashtakiwa kwa kukwepa kodi ama kumuibia mteja.

Na kama muuzaji utakua una una ushahidi wa mteja ajataka risiti, ukitoa taharifa akakamatwa mzigo unarudi dukani na unashtakiwa kwa wizi.

Huo ndio ushauri wangu unaotokana na njaa ya mchana huu.
 
Hata ukitoa risiti kwa haki kodi hatuoni inacho fanyia kazi bora ibaki kwetu tu
 
#NAPENDEKEZA :
TRA wawe wanafilisi mali papo hapo inapobainika haijatolewa risiti na Fain juu
Hili pendekezo ni zuri kwa pesa ya haraka na kukomoana ila halina going concern. Ukishamfilisi mtu anafunga biashara halafu unapata pesa hapo hapo ila unapoteza nyingine za mbele. Piga faini andika kwenye assesment alipe.
 
Huyo mfanyakazi wa TRA akikuta mzigo hauna risiti anapewa elfu 10 anaachia mzigo.

Hii ndio Tanzania karibu sana
 
Tuwe makini yasije yakatukuta Yale ya Sirilanka ambayo mpaka sasa wameshindwa hata kununua mafuta ya kuendeshea mitambo, magari na matumizi ya kila siku...
 
Yapo maduka kibao hasa yale yasiyobebeleza mteja ukitaka rist wanakwambia machine mbovu au anayetoa rist hayupo, bado wanakuuliza kwahiyo???, kazi inabaki kwako ununue au uache, ukiacha hiyo bidhaa hauipati kwingine.
 
we nawe sijui wa wapi! mawaziri wanaishi maisha ya kifahari kwa kutumia hizo hizo kodi na bado hushtuki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…