Masurura yetu
Member
- Dec 3, 2021
- 14
- 30
Mimi ni mjasirilismali,nina duka la matairi ya magari huku Mwanza.
Nilielekezwa kwenye hiyo kampuni tajwa hapo juu kuwa wanauza matairi ya jumla,basi nikafunga safari mpaka dar nikawatafuta mpaka ofisini kwao,ofisi zao ziko mikocheni sehemu inaitwa njia panda ya mawaziri.
Nilivyofika nikaandika order yangu nikalipia wakanipa risiti ya malipo tu,wakaniambia mzigo wangu wataupeleka wenyewe kwa transporter wangu na documents zote watampa transporter,nami sikuona ni tatizo kwani documents zinatakiwa ziambatane na mzigo njiani ili kuepuka usumbufu.
Kweli mzigo walipeleka kwa transporter lakini bila documents zozote, na mbaya zaidi siku hiyo TRA walikuwa na ukaguzi maeneo hayo ya Ilala hivyo mzigo wangu ukakamatwa na TRA, transporter akanijulisha hilo suala,nikawapigia wahusika kwa kutumia hizi number 0713174... na 0763235... ili kujua kulikoni. Hiyo number ya kwanza ni ya mtu niliyeambiwa anaitwa Sylvester ndiye meneja wa hiyo kampuni,huyo jamaa baada ya kumueleza shida yangu alichonijibu ni kuwa wao mzigo ukishafika kwa transporter hauwahusu tena na ana majibu mabaya sana utadhani sio Mtanzania. Sasa TRA wamenipiga fine ya 1.5m kwa makosa yaliyosababishwa na hao wapuuzi.
Nimejaribu kufanya uchunguzi kwa baadhi ya jamaa zangu Kariakoo kuhusiana na hii kampuni,wengi wanasema hawa jamaa ndiyo michezo yao hiyo,hawatoi risiti kwa wateja na mzigo ukikamatwa wao hawakusaidii chochote.
Wito wangu kwa TRA ifuatilieni hii kampuni kwa ukaribu muwachukulie hatua za kinidhamu kwa sababu wanafanya biashara za kihuni.
Nimeambatanisha risiti ya malipo waliyoniandikia ofisini kwao kama ushahidi.