Hakuna shida ila muwe mnaweka na sheria husika hii ni kutokana na finance act ya mwaka gani, ili kila mtu ajue uwezo wake wa kutumia huko kutokana na kodi za Tanzania, atunze receipts na adai kurudishiwa hizo kodi airport huko halipo kwa uelewa akija Tanzania atadaiwa.
Kwanini nauliza definition ya kuingiza ina mkanganyika. Vipi abiria wanaotoka kutembea nje ya nchi hawaruhusiwi ata kujinunulia ki begi kimoja cha nguo surely inatakiwa kuwe na amount ya vitu mtu ambavyo anaruhusiwa kuingia navyo for personal use, vikizidi ndio utata.
Siamini kama sheria inaweza kuwa general kiasi hiki busara ni kuweka hiyo finance act wote tuone, lazima kuwe na amount fulani inaruhusiwa especially kwenye bidhaa za bei ndogo and for personal use. Ipo hivyo duniani kote kuna leeway ukizidisha kile wanachodhani for personal use ndio kodi na sidhani kama Tanzania itakuwa kuna tofauti.
Ukiingia na mikufu mikubwa ume nunua sijui dola elfu ngapi huko hapo sawa kodi ata kwa mkufu mmoja.
But then na huyo mtu anaingia na vitu vya thamani bila ya kudai kurudishiwa VAT airport huko alipotoka ni ujinga wake huku akijua akifika Tanzania atadaiwa.
Lakini kibegi cha nguo kukikagua airport kudai kodi mtu katoka holiday, dah huo sasa uonevu.
Likewise na TRA iwe tayari kuwarudishia watu VAT airport wanapotoka nje ya nchi kwa bidhaa walizonunua Tanzania; mambo kama hayo huwa yana pande mbili.