TRA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya makadirio mapema

TRA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya makadirio mapema

TRA Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
128
Reaction score
370
makadirio  kumbuka.jpg
 
Tatu, mnapotuandikia barua na ku-quote vifungu vya Sheria, havitusaidii kabisa zaidi ya kututisha, huenda ndio lengo lenu. Ni lini kumeshawahi kuwa au kutolewa kwa Elimu ya mlipa kodi? Nina KAZI Ngapi? Nifanye biashara kisha nikariri na vifungu vya Sheria??
 
Nyie TRA mlikuja ofisini kwangu mkanidai withholding tax, nikawaambia baba mwenye fremu yule pale kamdaini mkanijibu bunge ndio limetunga sheria mnidai mimi kwahiyo nimwambie mbunge wangu akabadilishe sijui sheria au kanuni, mnatutesa wafanyabiashara
 
Ila TRA Tanzania mngejitahidi kupunguza mlolongo wa kodi, kuna kodi nyingine ni kichekesho. Kila kitu kingekua covered na Kodi moja, sasa Unatoa Huduma moja unakutana na utitiri WA Kodi! Eti kuna kodi inaitwa SDL, WHT, VAT, sijui na nini tena......!
Ngugu yangu kodi zimetofautishwa ni sawa huwezi sema anayekula wali maharage alipe sawa na anayekula wali kuku. SDl nijuavyo ni kodi ambayo mtu mwenye wafanyakazi kumi na zaidi ndiye anayelipa sasa kama huna wafanyakazi au unao chini ya hapo huwezi lipa.

WHT yenyewe inatozwa kwenye baadhi ya huduma mfano umepanga jengo au frame utasikia wanaita rental yaani inakatwa abla ya mpokeaji pesa kupewa pesa yake, au wale wanaotuuzia huduma za mawasiliano mawakala huwa nao wakiwa wanalipwa kamisheni wanakatwa wht hata wafanyakazi ile wanaita paye ni WHT.

VAT ni kodi ambayo uki google utaona ni kodi ambayo anayelipa ni mnunuzi wa huduma flani na bidhaa na anayelipa ni mnunuzi siyo mfanyabiashara, ni kodi ya mlaji yaani anayetumia huduma au bidhaa hiyo. Sasa huwezi changanya sababu kila kodi inatozwa kwa eneo lake na viwango havilingani . SDL ni 3.5%, VAT ni 18% rental na mawakala wa simu wht ni 10% paye kuna 8%,20%,25% na 30%
 
Ndugu ............. (E?), TIN ........., Tumekagua mwenendo wa mapato yako ya mauzo kuanzia Januari 2023 hadi leo na kugundua kuwa Taarifaya kodi inayostahili kulipwa kwa awamu (SETPI) inahitaji marekebisho ya kuongezwa zaidi- marekebisho haya ni kwa mujibu wa kifungu cha 89(5) cha sheria ya kodi ya Mapato , kuepuka adhabu na riba, Tafadhari fanya marekebisho haraka iwezekanavyo.Asante.
Pamoja Tunajenga Taifa Letu.
 
TRA Tanzania Nina hasira balaa..
Mwaka Jana mlinikadiria Kodi nikalipa; makadirio, WH, Stamp Duty, na Billboard.
Mkaniambia makadirio ya robo 3 ya mwaka nikanunue EFD mkanipa control number ya kulipa hiyo robo moja.
Ndani ya huo mwezi nikalipa control number, nikalipia na EFD.
Nikawaandikia barua ya kuomba kupunguziwa kodi.

Mwaka huu nikapata majanga na kupata loss ya mil 4 ile tu mwaka unaanza.
Nikaandika barua kuwaelezea loss nika-attach proof na kila kitu.

Ile siku naenda kuchukua Malibu ya barua yangu naambiwa "natakiwa kulipa laki 4 ya mwaka Jana" Sababu "nilichelewa kuomba msahama wa kodi"

Tunabishana, mkanijibu nirudi tarehe 03/04 kuendelea na malumbano yangu.

Sasa hiyo tarehe 03/04 nayo rudi mkiniletea ujinga Yule afisa Nam record na kumpost kila sehemu na LIWALO NA LIWE.

NIMEMALIZA.

#YNWA
 
Back
Top Bottom