TRA Jiridhisheni na kipato cha Mwijaku

Ningumu kumuamini chawa
Kwanza ungeleta ushahidi kuwa nyumba niyake kweli.
Lakini mwijaku kwakuwa ambassador wa makampuni mbalimbali means mshahara unapitia benki so ningumu kukwepa Kodi
At least unanipa tip kuwa yawezekana nyumba siyo ya Mwijaku, nakuelewa
 
Usichanganye mambo yasiyofanana. Naongelea issue ya Mwijaku kumiliki nyumba ya thamani ya Tsh 1.3 Bilion wakati vyanzo vyake vya mapato ni vya "mashaka"
 
Kwa vile ameitangaza nyumba yake kwenye vyombo vya habari, kuijadili siyo wivu. Bali kila mwenye akili sawa sawa lazima ajiulize maswali kuhusu vyanzo vya mapato yake.
 
Usichanganye mambo yasiyofanana. Naongelea issue ya Mwijaku kumiliki nyumba ya thamani ya Tsh 1.3 Bilion wakati vyanzo vyake vya mapato ni vya "mashaka"
Ungewaita kwanza watu wa valuation kujiridhisha na hiyo value. Mwijaku ni mtu wa media, kelele mingi mingi zinaweza zisiwe na uhalisia.
 
Nyumba ya mwijaku ni nyumba ya kawaida sana wala haihitaji uchunguzi.

Nyumba iko kwenye kiwanja cha 20x20, ngorofa la kawaida kabisa lile, haizidi 200m.

Kile kiwanja kigamboni haizidi 30m

Kama ana contract ya clouds ya kumlipa hata 4m na endorsements nyingine kwa miaka 3 ama 4 anajenga.
 
Huu sasa ni wivu wa kijinga kabisa.

Jamaa anajitoa akili, anagalagala mabarabarani ili tu ajitoe akili azoe mamilioni.

Hivi kweli kama upo mitandaoni huoni jamaa anavyojivua nguo mbele ya matajiri?? Hata wewe ungekua tajiri na maarufu na jamaa anakusifu kila kukicha usingekosa kumpooza mkikutana.

Jitoe akili kama yeye uone kama hutajiriki kesho tu.
 
CC
CHAWA, ChawaWaMama, chawa wa mama, Lucas mwashambwa
 
Acheni izo bhana hii bongo watu wengi tu wanatoboa kwa janja janja. Uyo mwijaku alivyokua hana kitu mliziambia izo mamlaka zichunguze umasikini wake?
 
Wewe bado kuanzia fikra mpaka maisha

Unawafundisha tra kazi au sio
au kiroho mbaya tu kinakusumbua
Huyo mwijaku ana connection kubwa sana nchi hii hawezi kusumbuliwa kwa chochote awe analipa hizo kodi au halipi
 
Kujitoa ufahamu kama wa huyu jamaa siwezi kwa kweli
 
Acheni izo bhana hii bongo watu wengi tu wanatoboa kwa janja janja. Uyo mwijaku alivyokua hana kitu mliziambia izo mamlaka zichunguze umasikini wake?
NENDA kasome sheria ya Mamlaka ya Mapato kwanza haihusiki na kuchunguza maskini. Pili inaitwa Mamlaka ya Mapato na siyo Mamlaka ya Mafukara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…