Tetesi: TRA Kitengo cha makadirio ya kodi ndio mnyama mkali na katili

Tetesi: TRA Kitengo cha makadirio ya kodi ndio mnyama mkali na katili

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Mh Rais ulisema jana watu wajilipuwe ila wengi walishindwa maana Uwenda kwa hasira ulio nayo juu ya uzembe na ubadhirifu kikao kingebadilika na unge weza hata taman upeleke mahakaman watu na adhabu yao iwe kunyongwa mpaka kufa.

Mh. Rais mambo kitengo cha makadirio na kile cha ukaguzi wa ndani wa mlipa kodi wanafanya nisawa nakuweka sumu ndani ya mto mkubwa ambao unategemewa na watu kwa maji yao binafsi na malisho. Kwa hakika Nadhan kile kitatokea ni kifo kwa kile kizazi na kansa zisizoisha. Yani kifo cha uchungu.

Mh. Rais watu wameumizwa, na watu wamefunga biasha baada tu yakukutana na mnyama mkali TRA kitengo cha makadirio. Wale jamaa ni wababe na wakishakuandikia makadirio yako kama Huna imani hata nyumbani hufiki.

Hivi kweli Unapomwambia mtu ukalipe figure hii na kam hutaki basi tutaonana. Anamanisha nini? Mh. Rais watu wamepata magonjwa ya moyo na wengine wamepoteza maisha.

Mbaya zaidi kile umekuona pale Kariakoo ndio Tanzania nzima mlipa kodi anavyopata shuruba. Unaweza fikiri wameambiwa wafanye hivyo au Wamepewa elimu moja tu kuwabambika watu makadirio ya juu ya kodi.

Kijana mmoja siku moja nilimkuta anasimulia yaliyomkuta alipoenda lipa kodi; jamaa alijaza form kwa uaminifu ila kichapo chake nadhani alijiuliza nifunge au nikimbie nchi? Huwezi kuamini kuna watu wamekimbia nchi kwa hii kodi, yani amepewa makadirio yake na ameyaona ni makubwa ameshikwa kabali lazima alipe mwisho mzee wa watu anaamua kula kona.

Wafanyabiashara wadogo ambao tungeweza kusanya hata laki laki na wapo tayari Wamepewa bils kubwa kiasi wengi wao wamefunga biashara.

Shida ipo wapi Labda?

Mh. Rais, tuna kizazi kina tamaa kuliko tamaa yenyewe. Yani kijana kwa muda mfupi anataka awe na maisha ya mtu aliyefanya kazi zaidi hata ya miaka 20. Jambo hili limewasukuma wengi kuwa magaidi na watu wasio kuwa msaada wa Taifa ila dhahma kwa Taifa.

Uwazi ktk kukokotoa makadirio ni mdogo sana, jambo ambalo watu wengi wanashindwa pambana na mnyama huyu mkali wa makadirio.

Elimu kwa mlipa kodi bado ni shida. Na hili ni lazima niseme mlipa kodi anapewa elimu ya Kwanini alipe kodi ila sio analipaje kodi na apambane vipi kujitetea asiumizwe na huyu mnyama mkali (TRA kitengo cha makadirio).

Rushwa iliyoota mapembe: Mkuu hapa asikudanganye mtu, yaani kama kuna taasisi Rushwa imewashinda ni TRA. Why? Ni kwa sababu hakuna anachopata mtoa taarifa sana sana wakikujua ndio wanakufilisi kabisa na hamna njia nzuri za kupeleka malalamiko kwa siri na yakafanyiwa kazi. Wanaokula Rushwa ambao ni maafisa wa TRA ukikaa hata kwenye vijiwe wanajulikana, ila sasa kwakuwa hakuna njia salama na maafisa wengine wanajua kula na wenzao hili limekuwa shida kuwaondoa.

TRA kama TRA kuwa taasisi inayofanana na JKT au TISS badala ya kuwa taasisi ya kuwajali wateja wao maana mlipa kodi ni mteja kama wateja wengine na ni mtu wa thamani sana kwa taifa. Kwanini anachukuliwa kama muhalifu au jambazi pindi anaingia ktk ofisi ya TRA? Ikumbukwe mataifa mengine mlipa kodi ni mfalme kiasi kila raia ana akaunti na TRA kama sehemu ya kuonyesha returns zake na kupata refunds.

TRA kutokuwa na muundo wa kisasa na udhibiti wa ndani ulio na kazi za ndani tu pasipo kutoka nje. Mfano ni kwanini auditor asafiri aje amkabe mteja X kwa kulipa kodi while kuna wahusika ktk Wilaya ile na mbaya zaidi akifika anaanza kusema huyu kapendelewa na kumuadhibu mteja badala ya kumuadhibu mfanya makadirio? Mimi nadhani wakaguzi wangewaadhibu watu wa ndani badala ya wateja, heshima na adabu ingekuwepo. Yaani siku hizi wilayani unakuta maofisa from mkoani HQ wamekuja na unaambiwa kabisa hawa wamekuja kukusanya za sikukuu; Yaani ina maana TRA kuna kitu hakipo sawa.

Ukaaji wa maofisa TRA ktk eneo moja na kuwa mabwana badala ya watumishi wa watu ikumbukwe afisa wa TRA ni mtumishi wa umma Wala sio vingine hivyo waishi utumishi wao.

Mifumo ya kutoa taarifa iwe ya siri zaidi kuweza kuwataja hawa wanyama wakali ndani ya TRA. Ikumbukwe sio wote ni maofisa wabaya ila wachache ni wakatili sana.

Mkuu usiishie kutengua ila ni muda muafaka kuisafisha TRA maana wamefanya jambo baya sana kuwanyanyasa raia wenzao ktk ofisi za serikali bila sababu yoyote.

Muda umefika kuimulika TRA kwa jicho la tatu na kuweka mdhibiti ndani ya TRA au kuongeza Uwazi zaidi na kuondoa vikwazo na urasimu. Naamini inawezekana kwanini ni TRA yetu tu kwani wenzetu wanafanyeje? Na kwanini tushindwe?

Mwisho hizi ni tetesi na maoni unaweza kuchunguza kwa kupata ukweli.

Asante
 
Mimi niliamua kufunga biashara baada ya kuona Maofisa wakadiriaji wa TRA wanakupiga kodi kubwa bila sababu.

(Yaani unampigia mtu mahesabu mara unamiliki gari,mara bili ya maji,umeme,ni ngapi,mara mnakula kilo ngapi nyumbani).

Sasa mimi nashindwa kuelewa kwa nini wasikubaliane vizuri ili watu walipe kodi stahiki.
 
Mkuu ulichoongea nikweli pasi na shaka. Kuna rafiki yangu wakalibu anakontena mwezi wa 2 sasa ameshindwa kulipia ushuru TRA wanataka alipe milion 25 tsh.

Ushuru ambao ni mkubwa mno, hata kama atauza vitu vyote atakua amepata hasara achilia mbali gharama alizotumia mpaka contena kufika hapo bandarini.
 
Kwanini neno ' kukadiria kodi'?

Tengeneza formula ambayo ni rahisi ambyo mfanyabiashara anaweza kuitumia kujua kiasi Cha kodi anachodaiiwa.

Kitengo Cha IT, Develop app then wafanyabiashara witumie kujikadiria na kulipa Kodi.

Vunja kitengo Cha ‘kukadiria kodi' weka kitengo Cha kuhakiki, tengeneza mfumo ambao si rahisi kwa watumishi wa chini kukutana na wafanyabiashara moja kwa moja
 
Mkuu ulichoongea nikweli pasi na shaka. Kuna rafiki yangu wakalibu anakontena mwezi wa 2 sasa ameshindwa kulipia ushuru TRA wanataka alipe milion 25 tsh.

Ushuru ambao ni mkubwa mno, hata kama atauza vitu vyote atakua amepata hasara achilia mbali gharama alizotumia mpaka contena kufika hapo bandarini.
Ndio hapo bidhaa zinapopandishwa bei maana huyo mwenye container itabidi auze bidhaa zake kwa bei ya juu.

Hawa watu wa TRA ni wanyama kabisa. Hao ndio wanao ua biashara na nchi hatimae ndio inapo onekana serikali ya Magufuli ni hovyo na mbaya.
 
Nilipita dukan kwa rafk yangu mhindi anauzaga malonya lonya na zagazaga viungo vya mezani nkakuta duka jeupe, kuuliza anasema kontena iko bandarini kodi ni 5 folds. Kachemsha hajui alitoe au aliache
 
Kwanini neno ' kukadiria kodi', tengeneza formula ambayo ni rahisi ambyo mfanyabiashara anaweza kuitumia kujua kiasi Cha kodi anachodaiiwa. Kitengo Cha it develop app then wafanyabiashara witumie kujikadiria na kulipa Kodi. Vunja kitengo Cha kukadiria kodi' weka kitengo Cha kuhakiki, tengeneza mfumo ambao si rahisi kwa watumishi wa chini kukutana na wafanyabiashara moja kwa moja
Hivyo ndivyo inavyo takiwa kwa kweli na mfanya biashara atafahamu mapema kiasi cha kodi kinachotakiwa kulibwa na hapo ndio atakua na uamuzi aendelee na hiyo biashara au atafute kitugingine kabla hajapoteza hela zake
 
Kwanini neno ' kukadiria kodi'?

Tengeneza formula ambayo ni rahisi ambyo mfanyabiashara anaweza kuitumia kujua kiasi Cha kodi anachodaiiwa.

Kitengo Cha IT, Develop app then wafanyabiashara witumie kujikadiria na kulipa Kodi.

Vunja kitengo Cha ‘kukadiria kodi' weka kitengo Cha kuhakiki, tengeneza mfumo ambao si rahisi kwa watumishi wa chini kukutana na wafanyabiashara moja kwa moja
Umeongea kitu cha msingi sana, sijui wanakwama wapi, mbona ktk magari wameweka calculator ambayo mtu unaweza kuangalia kodi ya gari hata kabla hujaagiza gari, ukiona kodi kubwa unaacha utafuta gari la saizi yako.

Hili la kukadiria limeua, limefirisi na kupoteza watu wengi sana. Mtu amepata kiinua mgongo chake milioni 50 anataka kuanza kibiashara anaagiza mzigo wa milioni 30 China, unafika bandarini anaambiwa kodi milioni 40 wakati yeye alidhani kodi haitozidi milioni 20.

Halafu walivyo washenzi, yaani hawana huruma wanakwambia kama hutaki acha. Yaani unaona mzigo wako unafirisiwa hivi hivi. Bora hata wangekuwa na huruma wakupe mzigo wako ukauze uwatafutie hiyo kodi yao, lakini wanataka CASH kama huna mzigo unauzwa utafikiri na wao walitoa pesa wakati wa kuagiza huo mzigo .
 
MAWAZO YANGU: Hawa vijana wa TRA siyo wazalendo... hivyo wachunguzwe hata uraia.... wao. Isije kuwa wanafanya hayo kwa makusudi ili kuikwamisha Serikali..... na taifa kwa ujumla. Vita ya Uchumi ipo... ndani na nje ya taifa ili mataifa jirani yapate soko la bidhaa zao..... "NI MTAZAMO WANGU.."
Huenda wanaamriwa kukusanya kiasi kikubwa kutoka kwa wafanyabiashara na ndio maana mwisho wa siku wao wanafukuzwa na wakubwa wanabakishwa
 
TRA ifanyiewe reforms from the scratch...hadi jina lenyewe libadilishe Kitu kikishaitwa AUTHORITY lazma uone miguvu mingi inatumika...waiite TANZANIA REVENUE SERVICE...ambapo sasa from the word service ndo tutaona hata wanatoa elimu kwa walipa kodi vizuri na pia wana wa service walipakodi na sio kuwafanyia authority authority
 
Lakini mimi huwa nashangaa sana. Wakati uongozi huu unashika hatamu, watu wengi walieleza humu jamvini jinsi biashara zinavofunga, na watu wengi wakaja na yao kuwa wengi wa wanaofunga ni wapiga deal, tena mpaka mkuu wetu alifikia huko. Sasa ni wakati wa kufikiria upya. Na sio biashara tu, turnover ya PAYE tuangalie je ist climbing or declining. Kuna tatizo kubwa sana kwenye hii nchi. Uchumi unashrink na haihitaji PhD kujua hili.
 
Tatizo ni sheria na mifumo tunayo iga badala ya kubuni yakwetu kwaajili ya tamaduni zetu na mazingira tulionayo na teknonoligia iliyopo kwasasa hata hivyo wengi wao hawana elimu ya ujasiamali ''Entrepreneurship skills”
 
Back
Top Bottom