Tetesi: TRA Kitengo cha makadirio ya kodi ndio mnyama mkali na katili

Mh Rais ulisema jana watu wajilipuwe ila wengi walishindwa maana Uwenda kwa hasira ulio nayo juu ya uzembe na ubadhirifu kikao kingebadilika na unge weza hata taman upeleke mahakaman watu na adhabu yao iwe kunyongwa mpaka kufa.

Mh. Rais mambo kitengo cha makadirio na kile cha ukaguzi wa ndani wa mlipa kodi wanafanya nisawa nakuweka sumu ndani ya mto mkubwa ambao unategemewa na watu kwa maji yao binafsi na malisho. Kwa hakika Nadhan kile kitatokea ni kifo kwa kile kizazi na kansa zisizoisha. Yani kifo cha uchungu.

Mh. Rais watu wameumizwa, na watu wamefunga biasha baada tu yakukutana na mnyama mkali TRA kitengo cha makadirio. Wale jamaa ni wababe na wakishakuandikia makadirio yako kama Huna imani hata nyumbani hufiki.

Hivi kweli Unapomwambia mtu ukalipe figure hii na kam hutaki basi tutaonana. Anamanisha nini? Mh. Rais watu wamepata magonjwa ya moyo na wengine wamepoteza maisha.

Mbaya zaidi kile umekuona pale Kariakoo ndio Tanzania nzima mlipa kodi anavyopata shuruba. Unaweza fikiri wameambiwa wafanye hivyo au Wamepewa elimu moja tu kuwabambika watu makadirio ya juu ya kodi.

Kijana mmoja siku moja nilimkuta anasimulia yaliyomkuta alipoenda lipa kodi; jamaa alijaza form kwa uaminifu ila kichapo chake nadhani alijiuliza nifunge au nikimbie nchi? Huwezi kuamini kuna watu wamekimbia nchi kwa hii kodi, yani amepewa makadirio yake na ameyaona ni makubwa ameshikwa kabali lazima alipe mwisho mzee wa watu anaamua kula kona.

Wafanyabiashara wadogo ambao tungeweza kusanya hata laki laki na wapo tayari Wamepewa bils kubwa kiasi wengi wao wamefunga biashara.

Shida ipo wapi Labda?

Mh. Rais, tuna kizazi kina tamaa kuliko tamaa yenyewe. Yani kijana kwa muda mfupi anataka awe na maisha ya mtu aliyefanya kazi zaidi hata ya miaka 20. Jambo hili limewasukuma wengi kuwa magaidi na watu wasio kuwa msaada wa Taifa ila dhahma kwa Taifa.

Uwazi ktk kukokotoa makadirio ni mdogo sana, jambo ambalo watu wengi wanashindwa pambana na mnyama huyu mkali wa makadirio.

Elimu kwa mlipa kodi bado ni shida. Na hili ni lazima niseme mlipa kodi anapewa elimu ya Kwanini alipe kodi ila sio analipaje kodi na apambane vipi kujitetea asiumizwe na huyu mnyama mkali (TRA kitengo cha makadirio).

Rushwa iliyoota mapembe: Mkuu hapa asikudanganye mtu, yaani kama kuna taasisi Rushwa imewashinda ni TRA. Why? Ni kwa sababu hakuna anachopata mtoa taarifa sana sana wakikujua ndio wanakufilisi kabisa na hamna njia nzuri za kupeleka malalamiko kwa siri na yakafanyiwa kazi. Wanaokula Rushwa ambao ni maafisa wa TRA ukikaa hata kwenye vijiwe wanajulikana, ila sasa kwakuwa hakuna njia salama na maafisa wengine wanajua kula na wenzao hili limekuwa shida kuwaondoa.

TRA kama TRA kuwa taasisi inayofanana na JKT au TISS badala ya kuwa taasisi ya kuwajali wateja wao maana mlipa kodi ni mteja kama wateja wengine na ni mtu wa thamani sana kwa taifa. Kwanini anachukuliwa kama muhalifu au jambazi pindi anaingia ktk ofisi ya TRA? Ikumbukwe mataifa mengine mlipa kodi ni mfalme kiasi kila raia ana akaunti na TRA kama sehemu ya kuonyesha returns zake na kupata refunds.

TRA kutokuwa na muundo wa kisasa na udhibiti wa ndani ulio na kazi za ndani tu pasipo kutoka nje. Mfano ni kwanini auditor asafiri aje amkabe mteja X kwa kulipa kodi while kuna wahusika ktk Wilaya ile na mbaya zaidi akifika anaanza kusema huyu kapendelewa na kumuadhibu mteja badala ya kumuadhibu mfanya makadirio? Mimi nadhani wakaguzi wangewaadhibu watu wa ndani badala ya wateja, heshima na adabu ingekuwepo. Yaani siku hizi wilayani unakuta maofisa from mkoani HQ wamekuja na unaambiwa kabisa hawa wamekuja kukusanya za sikukuu; Yaani ina maana TRA kuna kitu hakipo sawa.

Ukaaji wa maofisa TRA ktk eneo moja na kuwa mabwana badala ya watumishi wa watu ikumbukwe afisa wa TRA ni mtumishi wa umma Wala sio vingine hivyo waishi utumishi wao.

Mifumo ya kutoa taarifa iwe ya siri zaidi kuweza kuwataja hawa wanyama wakali ndani ya TRA. Ikumbukwe sio wote ni maofisa wabaya ila wachache ni wakatili sana.

Mkuu usiishie kutengua ila ni muda muafaka kuisafisha TRA maana wamefanya jambo baya sana kuwanyanyasa raia wenzao ktk ofisi za serikali bila sababu yoyote.

Muda umefika kuimulika TRA kwa jicho la tatu na kuweka mdhibiti ndani ya TRA au kuongeza Uwazi zaidi na kuondoa vikwazo na urasimu. Naamini inawezekana kwanini ni TRA yetu tu kwani wenzetu wanafanyeje? Na kwanini tushindwe?

Mwisho hizi ni tetesi na maoni unaweza kuchunguza kwa kupata ukweli.

Asante

Umesema kuwapa wakusanya kodi nguvu ya wenyewe kuwa wakadiriaji ni tatizo. Kodi zinatakiwa ziendane na risiti za mauzo itapunguza rushwa
 
Alafu atakuja mjinga mjinga atakuambia biashara zilizokufa ni za wapiga dili,,ukweli ni kwamba TRA sio rafiki wa mfanyabiashara,TRA iangaliwe kwa jicho la tatu,serikali inapata lawama nyingi kutoka kwa wafanya biashara kwasababu ya ujinga wa TRA.
 
Maslai yako yameguswa siku hizi umekuwa Na akili,umepata jibu sasa Ben 8 Na TL uliowaumiza hawakustahili
 
Kodi 1m kwa mwaka, ili ulipe chini ya hapo kulingana na kujitetea kwako anakwambia rekebisha laki4 ili ulipe laki5 kwa mwaka...hawa jamaa ni funza ndani ya miili ya watu
 
Kuwasingizia TRA Na Matrafiki walivotugeuza ng'ombe wa maziwa ni kuwaonea wao wao ni loudspeakers tu.Wamekuwepo awamu hata zilizopita kwann walaumiwe awamu hii. Wao wanatii maagizo ya ilani ya Kusomesha watu no ili waishi kama mashetani.
 
Mm inaniuma sana kukamuliwa kodi then watetezi wa wanyonge wakiishi kama malaika Kwa kodi yangu,wanamiliki Magari makali,mijengo hatari Kwa kodi yangu,ambao hata nipige kazi miaka 1000 siwafikii
 
Mtanzania Leo anakwenda nunua bidhaa mfano nguo Uganda bei nafuu hali zinapita bandarini kwetu,Zambia dizeli Lita sh 1200 Na yanapita bandarini kwetu,kulipia ushuru wa GARI Tz ni ghali kuliko gharama ya kutengeneza GARI Japan. Thus tunanunua second end nikiichoka namuuzia mwingine hivo hivo mafundi wote mjini washakorokochoa.Wenzetu GARI ikisumbua wanauza screpa.Kodi kubwa makusanyo kiduchu,wenzetu kodi ndogondogo kidogo Lkn wanakusanya kingi mara kumi zaidi yetu,kodi ikiwa kidogo ni aibu kuikwepa siwezi kimbizana Na TRA talipa,ikiwa kubwa lzm tukutane bar tuyajenge,matokeo yako serikali inakosa kodi.
 
Huenda wanaamriwa kukusanya kiasi kikubwa kutoka kwa wafanyabiashara na ndio maana mwisho wa siku wao wanafukuzwa na wakubwa wanabakishwa

Wawatue mizigo matrafiki pia wanawapa malengo makubwa sana Kwa siku thus trafiki akikukosa Na kosa ananuna.Wanakwenda speed sana wamejikita kwenye kukusanya zaidi kuliko kuelimisha ili watimize malengo,
 
Kufungia biashara za watu kwa hila ni kosa la uhujumu uchumi. Kama biashara zikifungwa, kodi zinapatikanaje?
Tuende mbali kwenye kuhakikisha haki za wote zinalindwa. Kama kuna waliokuwa wanatumia nafasi zao za kuwa TRA kunyanyasa wafanyabiashara kwa kudai na kupokea rushwa, nao wawajibike. Kila mtu apimwe kama anachomiliki kinaendana na kipato chake. Vinginevyo hili tatizo halitaondoka
Hawa jamaa wako na mbinu nyingi...biashara zao hazitumii majina yao...kama ni pesa wanapokea ofisini na sio nje...wako na bahasha zao kama hukuwa na bahasha ulikotoka....yaani basi tu jamani
 
TRA wakiweka system ya kueleweka mianya ya Rushwa automatically itapungua, kama serikali walivyofanya uhamiaji kwenye utoaji wa passport mpya, kila kitu ni system unakutana na immigration officer kwenye finger print na kuverify forms hiyo rushwa wataomba saa ngapi

Tatizo serikali yetu wapo too manual ndio maana Rushwa haziwezi kuisha

By the way wakiweka system za kueleweka kwenye idara za serikali mambo yataenda faster hata Idadi ya wafanyakazi itapungua mishaara na posho wanazolipwa for doing nothing zitaenda kujenga Taifa
 
Kinachonishangaza ni kwa nini tukadirie badala ya kuwa na mfumo wa kukadiria ambao huwapa nafasi hawa wafanyabiashara kuwabambikia kesi wafanyabiashara ili baadaye wawadai rushwa.
 
They're not being "facilitators" as they say they are.

Back
Top Bottom