TRA kudhamini Ndondo CUP, Pesa hizi wanatoa wapi?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Nimeona leo TRA wamekuwa wafhamini wa ndondo cup.. watasema sijui wanataka kujitangaza?

TRA wanafanya biashara gani? Pesa za walipa kodi ndio wanatumia kwa upuuzi huu?

Sijasema ndondo cup ki upuuzi lakini Mil 40 zinajenga zahanati 1 kijijini?

Kazi ya TRA ni moja tuu, kukusanya mapato na kuyapeleka hazina .
 

Attachments

  • Screenshot_20240820-130437_Instagram.jpg
    464.3 KB · Views: 4
Nssf
Tra
Psssf
Biashara yao wanafanya kwenye mifuko yenu mnashangaa nini wakuu.....
 
Hivi Ile kesi ya mfanyakazi wa TRA kukutwa na pesa bilioni saba nyumbani kwake anazilalia iliishia wapi?Au ndiyo hizi ameamua adhamini mdondo cup?
 
Mleta tuma account yako nikutumie 40m ujenge zahanati kijijini kwenu. Halafu tambua pia zamani mashirika karibu yote yalikuwa na timu za mpira kwahiyo TRA kudhamini mashindano sio kesi. Ni jambo la maendeleo
 
Mleta tuma account yako nikutumie 40m ujenge zahanati kijijini kwenu. Halafu tambua pia zamani mashirika karibu yote yalikuwa na timu za mpira kwahiyo TRA kudhamini mashindano sio kesi. Ni jambo la maendeleo
11123457425 NMB
 
JIFUNZE:
TRA ina kitengo cha elimu kwa umma na kina bajeti yake, ndio maana huwa unasikia matangazo yao kwenye vyomba vya habari (Inawezekana ulidhani wanatangaza bureπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€) au pengine hulipi kodi na hujawahi kukutana na tangazo la TRA so sikulaumu. Kutoka kitengo hicho TRA wanatumia mbinu kadhaa kufikia wananchi ikiwemo hii ya kwudhamini michezo ikiwemo NDONDO Cup,

Tena MILIONI 40 ni pesa ndogo sana

Karibu kwa maswali zaidi
 
Hujui TRA wanapotoa pesa? Like seriously?
 
Mbona hatuoni digital content za TRA, wakihikiza tulipe kodi, hapa kuna upigaji
 
hayo ni makusanyo ya kijana mmoja hapo kwa miezi miwili yanayoishia mfukoni mwake
 
Walipanga bajeti mapema kwa ajili ya kujumuika na jamii/kuileta karibu,kutoa elimu ya kulipa kodi,kuiburuidisha jamii,kukuza michezo na kuirudishia jamii kile wakiingizacho/fedha kutokana na walipakodi.
 
Wakati wanamiliki Timu ya Bandari pesa walikuwa wanatoa wapi?

KMC wanatoa wapi pesa? Mbeya City Je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…