Lazima kuwe na sera ya kuwainua wananchi kiuchumi kwa kupunguza Kodi na usumbufu ili wawe matajiri na hatimaye taifa au nchi iwe tajiri.
Fikra za kimasikini za kuwaongezea Kodi na usumbufu wafanyabiashara wazawa huendeleza umasikini huku zikiongeza wageni kumiliki uchumi.
Kwanza kabisa ni lazima ieleweke kwamba, nchi haiwezi kuwa tajiri kama wananchi ni masikini.
Kwa dunia ya sasa, wezesha wananchi, bana wageni wasifanye biashara kama za kariakoo, waruhusiwe tu kwenye viwanda na baadaye wabanwe baadaye ya wananchi kuiga teknolojia, ili tumiliki uchumi wetu wenyewe.