TRA Kufungua duka Kariakoo

TRA Kufungua duka Kariakoo

Bandarini kama kawaida tu wakiona vipi wanavusha
Hivyo hawatopata uhalisia wa mfanyabiashara anaefuata taratibu wanazo taka azifuate huku wao hawatoweza kuufuata utaratibu huo, hivyo kwa kifupi TRA badala la kupambana na wahujumu uchumi basi wao ndio watakua wahujumu uchumi wenyewe
 
Hahahah, yaani mpishi wa chakula awe anajipakulia yeye chakula ili aone ukweli wa malalamiko ya wanafunzi kutoshiba?! 😂😂😂😂😂😃😃😃

Kwani matumbo yana size sawa?
 
Na jeshi la polisi lifanyaje ili wapate experience ya malalamiko ya raia wanaobambikiwa kesi na vipigo vya mbwa mwizi pindi wanapowekwa chini ya ulinzi?!
 
Imefikia hatua hiyo ili iweze ku experience kile ambacho wafanya biashara wengi wanakilalamikia ili kujiridhisha
Inabidi nao wakwepe kodi , wasitoe risiti na wawe na stoo ya mafichoni ili wapate experience ya maisha ya wafanya biashara wa kariakoo
 
Magifuli alifanya biashara nyingi kuhamia store Kwa store, kwan kuwa na fremu ni kujitafutia matatizo.

Hatimaye viduka kwa nje vikawa vidogo na machinga soko Zima, huku wadosi wakiuza kutokea store
Alikuwa mwehu sana!
Kariakoo inapotential kubwa sana ya kuwa hub ya shopping tourism!
Sema mamlaka, taasisi, idara na vitengo vya serikali Kuna watu hawana ubunifu
 
Lazima kuwe na sera ya kuwainua wananchi kiuchumi kwa kupunguza Kodi na usumbufu ili wawe matajiri na hatimaye taifa au nchi iwe tajiri.
Fikra za kimasikini za kuwaongezea Kodi na usumbufu wafanyabiashara wazawa huendeleza umasikini huku zikiongeza wageni kumiliki uchumi.
Kwanza kabisa ni lazima ieleweke kwamba, nchi haiwezi kuwa tajiri kama wananchi ni masikini.
Kwa dunia ya sasa, wezesha wananchi, bana wageni wasifanye biashara kama za kariakoo, waruhusiwe tu kwenye viwanda na baadaye wabanwe baadaye ya wananchi kuiga teknolojia, ili tumiliki uchumi wetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom