TRA kuvunja rekodi dhidi vifo vya biashara na viwanda,tujitafakari na kujirekebisha


Unadhani malalamiko ni wafanyabiashara wa Kkoo pekee?

Tuendelee kuisaidia nchi Kwa kutoa ushauri na mapendekezo yenye kujenga..

Maafisa kodi wengi wakifukuzwa ama kustaafu kisha kuanzisha biashara hawafiki miaka mitatu wanafunga na wengine kufa..

Tujitafakari na kujenga uchumi imara..Haya malalamiko yapo kila kona si Kwa Wahindi,Waarabu,Wazungu,Waswahili..Yamkinihawana Kwa kunena kero zao..

Hatupaswi kumlaumu Mh Rais Kwa haya..Turekebishe sheria,kanuni,mitazamo kisha kuwekeza kwenye Elimu Kwa kina ..
 
Ni shida kwakweli nakubaliana na wewe.

Jinsi wanavyofanya nchi za wenzetu wafanyabiashara wengi ambao awawezi mwajiri accountants full time. Kuna sole proprietor registered accounting firms, ambao wanawatumia kuwafanyia hesabu.

Sasa biashara zote ndogo zilizojaa Tanzania na wenye biashara wengi maswala ya kodi yanawapiga chenga unashanga hakuna qualified accountants wanao ona hiyo fursa.

Wakati ukiwakusanya hao kama 300 hivi kila mtu akulipe 250,000-500,000 kwa mwaka, siasa za nini. Binafsi nimeshaeleza sana hivi wewe qualified accountant uoni hiyo fursa.

CPA kama hajui tax hiyo ni shida, I don’t know mitahani yao huku kijijini kwetu professional body ni ACCA, pamoja na hivyo sidhani kama kuna proffesional body ambayo inakosa mtihani wa kodi. Maana ya kuwa proffesional accountant lazima ujue maeneo yote auditing, tax, financial accounting na management account; na mambo ambayo unasoma kwa miaka mitatu ya degree yako. Sasa itakuwa maajabu kama graduate hajui kodi achilia mbali qualified accountants kama CPA.

Na kodi zinabadilika kila mwaka hata qualified accountants nao wakawaida nchi za wenzetu kuwa updated kuna vitabu ambavyo vinasaidia kuelezea how to compute new taxes kama kuna changes kutokana na finance bill ya mwaka husika. Au website ya serikali (tax administrator) itaelezea.

Ila shida zaidi ni kwamba wafanyabiashara wa Tanzania wao hata concept ya VAT tu wengi inawasambua sasa udhani kama registered wanatumia hiyo fursa kudai vat ya mafuta kwenye magari ya biashara na sehemu zingine za matumizi ya biashara ambayo they are entitled to claim.
 
Maafisa wa kodi wengi sio wahasibu wao wanakuwa trained kudai kodi tu, the higher (seniors) wanapata training zaidi mwisho uwezo wa kufanya tax investigation.

Hesabu za biashara ni complicated zinahitaji mtu ambae kasomea uhasibu kwa ujumla. Sasa sio ajabu maafisa wa TRA biashara kuwashinda.
 
Tunakataa kodi kandamizi, mfano, leo hii nikiandika invoice kudai mahali popote pale nakatwa 2% pamoja na service levy, hiyo 2% niliyokatwa itaingia kwenye mfumo wa TRA na kwenye akauti yangu ya TRA hivyo natakiwa kukiri kwa kukatwa hiyo 2% nisipofanya hivyo napigwa penati 250,000 sasa jiulize hii penati ni kosa gani ? Nimedai hela yangu nimekipwa pungungufu halafu eti haujakiri kukatwa hiyo hela kwahiyo uilipe TRA 250,000 huoni huo kuwa ni unyanyasaji? leo unaambiwa ukinunua dai rist na kama wewe ni mtu wa VAT nunua kwa mwenye VAT mwenzako lkn mwisho wa siku wasilisha return udai hicho kiasi kilichoongezeka na wewe kama mwananchi mtiifu unafanya hivyo lkn baadae TRA wanakugeuka kuwa rist nyingine hazina sifa ya kuwepo kwenye return kwani wewe hujajisajiri kufanya hiyo biasgara ukiyonunua.Ndugu unataka uwe mtumwa kiasi gani hapo??
 
Reactions: K11
Tra imejaa wezi, vilaza, wanatabia kama wale mgambo waliokuwa wanakusanya Kodi ya kichwa enzi za Mwalimu, miaka ya 80+
Ass hole, cock suckers watupu
 
Reactions: K11
Liangaliwe hili
 
This is not a story but root causes
 
Muuza duka kariakoo ana mtaji wa M500 anajua huu mzigo ukiisha napata M570 matumizi ni 1,2,3 nabakiwa na M30 kodi zote ni 5M nabakiwa na M25. Hizo ndo hesabu zao, mambo ya DR, CR sijui Balance sheet hawataki kusikia wanalazimishwa tu na ukiangalia kwa makini ni kweli wanalazimishwa tu, wapigwe kodi kama presumptive tu wahasibu watafute kazi kwenye makampuni sio maduka ya wakinga.
 
Mzigo wa tsh 500 million halafu kodi zote tsh 5 million. VAT pekee za consumer goods nyingi 18% ukijakukaguliwa TRA watakupa estimate ya deni la tsh 90 million.

Halafu mfanyabiashara anafikiria gross profit ya tsh 70 million, hata VAT ailipi kwa mzigo alionao.

Sasa mtu kama huyo shida ni TRĄ au ni hesabu zake za biashara, poor business plans and kutokuwa na realistic targets.
 
Reactions: Tsh
VAT analipa mteja boss.
 
Mfanyabiashara ila analipa tofauti ya alicholipa na alichopokea.
Wakae chini kujifunza hesabu za biashara au serikali ianze kuhamasisha certified accountants kuanzisha huduma za kodi.

Yaani wewe CPA upate mshahara wa million mbili kwa mwezi wakati kuna fursa ya kuwakusanya wafanya biashara kwa fees ndogo na kutengeneza zaidi ya million 100 kwa mwaka kama ‘sole proprietor’ na target ya income ya billion ni possible kabisa.

Shida kubwa ni business plan za wafanyabiashara na uelewa wao mdogo wa maswala ya kodi.
 
Reactions: Tsh
Sasa hivi hii yaVAT Wala haitajiki CPA. Certificate ya account tu hizi VAT unafile. Hata form 4 anafile maana system inareconcile mauzo na manunuzi yenyewe. Inakuletea manunuzi unasema next, mauzo unasema next inakuletea assesment unasema send kwisha. Kama kununua kifurushi cha simu.
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=xEU5GWcrF_A
Umesikiliza mwenyekiti wenu wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Kariako ‘Martin Mbwana’ baadhi ya malalamiko anayotoa. Anadai TRA inafuta input tax zao, halafu wakitoka hapo wanakuja kwenye biashara na kutaka kuona receipt za manunuzi, ku-check remaining na kutaka kuona receipt za mauzo.

Analalamika huo utaratibu ni usumbufu na unyanyasaji, sasa anadhani hao TRA ni wajinga uwape input vat kubwa kuliko output vat; halafu wakulipe tu kurahisi bila ya kuhakiki.


Kufanya hesabu za VAT ni rahisi kuelewa shughuli za TRĄ kwa mujibu wa sheria na majukumu yako ya kutunza ushahidi wa kibiashara kwa mujibu wa sheria chances are ni ndogo, lakini accountant kwenye masomo yake ya kodi anajua lazima kuna ‘VAT Act’ inayo orodhesha biashara inatakiwa kutunza nini na kwa sababu gani za kihasibu.

Sasa basi ‘Part IV’ ya hiyo sheria hapo nikiyokuwekea inaelezea maswala ‘Documents and Records’ hayo mambo hayajawekwa ili sheria iwe ndefu tu ni matakwa ya mfanyabiashara kufanya hivyo na TRA wanaruhusa ya kufanya random audit anytime, na ukijaribu kuwaongopea wakashuku hesabu zako ni sawa na kuwakaribisha.

Halafu wakija unalalamika wanataka kuona vitu ambavyo unatakiwa kutunza kwa mujibu wa sheria wewe huna unaita huo ni uonevu. Ndugu nchi zingine huna huo ushahidi records mziki unaofuata sio wa kitoto utajuta. Wakati mtanzania ambae hana huo ushahidi anafunga safari kwenda Dodoma kumlalamikia waziri (tells you ignorance ya wafanyabiashara).

Uwezi jiwekea kodi za output VAT ukadhani huko TRA kumejaa wapuuzi au bila ya kuelewa hiyo sheria msingi wake ni IFRS na auditing standards za kutunza ushahidi. Well uwezi jua msingi wa mambo kama hayo kama wewe sio accountant.

Ni hivi sehemu kubwa ya malalamiko ya wafanyabiashara huwa ni uelewa wao mdogo tu wa maswala ya kodi na poor business plan. Hapo ndio kwenye shida.

Solution ya kudumu hapo ni tax services za kuhudimia biashara ambazo aziwezi ajiri accountant full time, wafanyabiashara hawana elimu ya kodi hapo ndio kwenye tatizo.
 
Kama unafutiwa input huo ni wizi. Nimenunua na kupewa risiti halali unasema sijanunua ww si mwizi? Unless nimenunua kwa risiti fake, risiti yangu ni deni la VAT kwako.
 

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3cz
 
Kama unafutiwa input huo ni wizi. Nimenunua na kupewa risiti halali unasema sijanunua ww si mwizi? Unless nimenunua kwa risiti fake, risiti yangu ni deni la VAT kwako.
Ndio uweke ushahidi sasa wa records unazotakiwa kuwa nazo ili wakulipe, hawana mamlaka ya kukataa kukulipa ndio maana kuna baraza la kodi unaweza wapeleka huko.

Sio unaweka madai ya VAR wakija kuhakiki kumbe huna huo ushahidi mnaaza hadithi za kuonewa ohoo wanataka kukagua remaining stock, sijui kuona receipt za manunuzi etc with audit za kujiridhisha kwa kufuata sheria.

If anything nchi nyingine mambo kama hayo ni fraud ukijaribu huo mchezo wakija tax officers kukukagua kumbe utunzi hata records za biashara kuna mtu anaweza ishia jela sio swala la mzaha kabisa. Tanzania mfanyabiashara anaefanya upuuzi huo anadhani yeye ndio anaonewa.

Shida kubwa ni uelewa mdogo wa maswala ya kodi, taratibu za kihasibu katika biashara (hasa umuhimu wa kutunza records) na mipango rahisi ya biashara.
 
Hilo la kufutiwa input nina mashaka nalo, ts either risiti ni fake au uliyenunua kwake mashine yake haijatuma report.

Ukifuta manunuzi yangu ina maana umefuta mauzo ya aliyeniuzia. Unakuwa umefanya nini? Hapo TRA si atakuwa anajaza maji kwenye gunia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…