Kwa Mtazamo wangu
TATIZO LA KARIAKOO NI ZAIDI YA WAFANYABIASHARA,WACHUUZI..LETS BE SERIOUS.
Tatizo la kariakoo haliwezi Kwisha ikiwa total supply chain ya mizigo inayouzwa kariakoo isiporekebishwa au kudhibitiwa kupitia maamuzi magumu na kutooneana haya wala aibu..
Bidhaa nyingi zinazouzwa kkoo zinaingizwa (Imported) toka China,India,Uturuki,Thailand,Vietnam,Zambia,Uganda,etc..Mfumo wa uingizaji na ulipiaji kodi wa mizigo husika ndio mzizi wa shida na tatizo lililopo na litakalokuwepo..
Cartel inayoratibu Logistics na supply chain ya mizigo ya wafanyabiashara wa karikoo isipodhibitiwa kila nyakati tutaona fukuto na migomo isiyohitaji siasa Bali utashi wa maamuzi magumu kudhibiti wahujumu uchumi tunaowalinda..
Mathalani,Mfanyabiashara akiagiza mzigo wa viatu Kwa kontena na kulipa ushuru stahiki kisha kuwa na nyaraka zote Za kikodi (Import duties,Port charges,Wharfage,VAT) inamgharimu milioni 45….NOTE:- Ila akiagiza mzigo huo huo kwa kutumia Logistics Cartels inamgharimu Milioni 15 tu pasipo nyaraka zozote lakini Ana uhakika wa kufikishiwa mzigo dukani au warehouse kwake pasipo usumbufu..
Sasa wale wafanyabiashara waliokuwa wakikomaa na kufuata taratibu stahiki wamejikuta wakishindwa kushindana ktk soko na kufirisika ama kufa kibiashara sababu ya ughali wa bidhaa dhidi ya wale wanaotumia Logistics Mafia..
On the other hand wanaotumia huduma za logistics cartel au mafia inawawia Vigumu sana kufanya compliance za kikodi sababu ya kukosa nyaraka muhimu kussuport mapana ya stock zao..Mauzo yao,returns zao..Hapa ndio kwenye shidaa haswaa…Wengi wana stock kubwa kuliko vielelezo vya manunuzi ya stock husika..Wamegeuka wachuuzi..Wanaouza ambacho hawana nyaraka Za wametoa wapi..SHIDA.
Logistics Cartel/Supply chain Mafia:-Ni kundi hatari lenye nguvu kupitia wanasiasa wakubwa waliopo na wastaafu..Wana ukwasi mkubwa na umaarufu mkubwa ktk Kiwango cha kuogopeka na Wakubwa wa TRA,Polisi,Etc..Wana nguvu mnooo ya kufanya wakubwa ktk mamlaka Za kodi watumbuliwe,Wafanyakazi wahamishwe,Wawe demoted..Wapate Stroke..Nina hakika hata CG wa TRA anawaogopa..Hana la kuwafanya..Inasemekana baadhi ya viongozi ni marafiki wakubwa..
Cartels hizi zimehodhi Supply chain Za uagizaji bidhaa,usafirishaji,Ulipaji kodi,Udanganyifu (under declaration&Falsa Declarations),Uzungushaji mizigo (Taarifa Za kampuni Za tracking devices Za mizigo ya transit zina mengi)..Wanamiriki makampuni ya uagizaji,Usafirishaji,Bonded Warehouses,ICD’s,CFS..yaani acha tu..
Kwa hakika tunapoteza kodi nyingi sana zinazoingia mifukoni mwa wachache tunaowaimbia mapambio ya utajiri na ubilionea huku wachache wakikamuliwa hata kuzirai kibiashara..Bila maamuzi magumu na dhabiti tutaendelea kukwama na kuumiza wasiostahili..
Tukiamua Tunaweza..Viongozi wenye dhamana Simameni kwenye haki na ukweli..